Huduma ya muziki kwenye Treni ya Delux Kigoma - Dar ni kero

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,235
874
kwa safari ya kigomA dar kewa njia ya train Kuna train za aina mbili kihuduma kama sijakosea . kuna train inaitwa ordinary na ingine ni luxury. ukiwa unatoka kigoma train hii ya deluxe nafikiri ndiyo luxury, ilikuwa inapendwa sana kwa sababu iliaminishwa kuwa inasimama vituo vikubwa tu . Aidha kwa sasa naona hilo halitekelezeki sana. offcourse kibiashara lazima mabadiliko ni lazima

Hoja yangu kwa sasa ni Huduma inayotolewa ndani ya train hii . Kuna huduma ya music . kwa kweli nikisafiri na hii train naona ile miziki inayopigwa mule ndani ya tarin , aidha speaker si nzuri au muongozaji anapandisha sana sauti na kuwa kero . TRC wanatakiwa watambue kuwa , ndani ya train ni sehemu ya kumpumzika pia .unakuta muziki unapigwa mpaka saa saba usiku , kwe;li hii si sawa na hata wakipiga mida ya mchana bado sauti inakuwa juu mno na nyimbo zenyewe zinakuwa za vijana wakati train hii ni ya makundi yote.

Ushauri wangu, waondoe huo muziki na kama wakiacha iwe ni sauti ndogo sana na watu waweze hata kusikilizana katika simu . Ikibidi watuwekee kitu cha kuweza kuzima na kuwasha kwa kila behewa. Juzi kati nilifanya tafiti katika behewa la second nililokuwepo . Niliuliza watu , hivi wanaonaje huu muziki . Behewa zima walionyesha kutokukubali upigaji wa muziki Ndani ya behewa . Mtu mmoja alidiriki hata kusema , kwa kuwa tunasimu na charge system ndani ya train ni nzuri sisi tunanyimbo zetu unaweka earphone unaendelea kuburudika .

Tafadhali uongozi wafanyiwe kazi hili, wengine ni wagonjwa wanaenda mahospitalini
 
Tofaut ya naul kati ya luxury na ordinary ipoje?

Kuna huduma ya kulipia chumba?
 
Sawa, Pia nakukumbusha kwamba Shirika la Reli Tanzania – TRC laibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika Maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara maarufu SABASABA na kupata Tuzo katika sekta ya Usafirishaji nchini, wakati wa hafla ya kufunga maonesho hayo jijini Dar es Salaam Julai 13, 2023.
 
Siyo hilo la mwisho wa reli tu hata la kuja chuga nalo ni tatizo kubwa sana.

Nililipanda aseee, yule sijui DJ kuku anafanya vizuri sana kutangaza hatuw kwa hatua au maeneo mageni, mapya au penye shida kwa njia ya reli ila kelele ni za muziki ni nyingi sana.

Kwenye issue ya Deluxe na Ordinary train, kweli afrika hatuna mifumo, sisi ni bora maisha yaende tu sababu wanaanzisha mambo mazuri alafu baada ya muda wanavuruga huo utaratibu.
 
Sawa, Pia nakukumbusha kwamba Shirika la Reli Tanzania – TRC laibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika Maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara maarufu SABASABA na kupata Tuzo katika sekta ya Usafirishaji nchini, wakati wa hafla ya kufunga maonesho hayo jijini Dar es Salaam Julai 13, 2023.
Yaani hoja mzito hii umeijibu kirahisi sana..kazi tunayo..hiyo tuzo mmechukua tu kwa sababu watu/ abiria hawana mbadala.
 
Sawa, Pia nakukumbusha kwamba Shirika la Reli Tanzania – TRC laibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika Maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara maarufu SABASABA na kupata Tuzo katika sekta ya Usafirishaji nchini, wakati wa hafla ya kufunga maonesho hayo jijini Dar es Salaam Julai 13, 2023.

kushika nafasi ya kwanza sio sababu ya kutatua kero waliwapa hiyo nafasi hawajashuka chini kuwauliza wananchi huduma zao zipo vipi
 
Back
Top Bottom