Muungano wa Serikali 3 ni bora Sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano wa Serikali 3 ni bora Sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tenende, Aug 13, 2012.

 1. t

  tenende JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Serikali 3 ni bora sana kwa sababu zifuatazo:
  (i) Ni muarobaini wa malalamiko ya kuonewa au kumezwa;
  (ii) Ni balance nzuri ya uwiano serikalini - 50 kwa 50 katika uwakilishi na gharama;
  (iii) Hujuma za kuingiliana ktk chaguzi na kulazimisha chama kimoja kiongoze pande zote mbili zitadhibitiwa kirahisi;
  (iv) Hoja ya muunda wa serikali kuwa sera za vyama tutakuwa tumeimaliza;
  (v) Gharama za uendeshaji zitapungua kwa zaidi ya 50%. Mfano mmoja, serikali ya Muungano (serikali 2) kwa sasa (siyo SMZ) inalipa wabunge zaidi ya 80 wa Zanzibar (yenye wapigakura pungufu ya laki 4 na 50 na ukubwa sawa na wilaya ya Sengerema). Kila mbunge akilipwa milioni 11 kwa mwezi (11x80) sawasawa na milioni mia 8 na 80. Muundo wa serikali 3 tutakuwa na wabunge 30 au 40 (15 au 20 toka kila upande kufanya kazi za muungano wakigharamiwa na pande zote 2) na wabunge Serikali ya Tanganyika wapatao 150. Huu ni mzigo mwepesi kwa walipa kodi wote. SERIKALI MBILI NI MZIGO!!!!!
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja.
   
 3. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mi sijaelewa vizuri serikali tatu ni mzigo kivipi..
  Naomba anae pinga serikali tatu anieleweshe
   
 4. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  we ni mjinga tanganyika tuko mil zaidi ya 40 zanzibar wapo zaiidi ya mil 3 sasa ukisema tugawane 50/50 ni sawa......
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,220
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Kwenye thread inzoulizamaswali kuhusu serikali 3 au mkataba mnakimbia.
  Kuna nini cha ziada hapa zaidi ya kile kilichopo katika thread nyingine?

  Labda nikuulize Tayadi maana sitachoka, Hivi hiyo ya muungano(tatu) itashughulikia nini?
   
 6. F

  Falconer JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  At long last munaanza kuona mwangaza. Na wazanzibari walikuwa na kilio hiki kwa muda wa miaka 48. Lakiini kulingana na wakati tulio nao, serikali tatu ni gharama kubwa sana. Bora tugawane mbao. Kila mmoja aendeshe jahazi lake ki vyake.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  NA JE, Kutengana na kuwa Nchi Mbili tofauti Gharama zake si ndio zitakuwa pungufu mara dufu?

  Kwanini tuwe na Serikali tatu wakati Mmoja wetu hata hataki kutuona HAI? Wanaona VIONGOZI wetu kama WALAFI

  SIJUI NYERERE alibeba nini toka ZANZIBAR chenye UMARUMARU... Sidhani aliibia Zanzibar zaidi ya Alhaj Mohammedraza

  [h=1][/h]
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  WanaJF,
  Mimi nafikiri kuwa Mwalimu Nyerere alitusaidia dawa ya matatizo ya (usanii)Muungano wa Tanzania kupitia hotuba yake bungeni na kupitia hiki kitabu chake.

  Vyenginevyo ni kutafuta kuvurugana tu na kulikoroga zaidi.

  Mwalimu alisema mengi na haya yakiwa baadhi yake.

  Basi na tutafute mfumo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikalli mbili zenye uzito unaolingana.

  Labda ni vizuri kukumbusha kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa nikuunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katikati ya mazungurnzo ya kutafuta uwezekano, wa kuungana. Kama jambo hilo, lingetokea, nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungelikuwa ni Shirikisho.

  Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.

  Uk 11-12 link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

   
  Je tumeshapata sababu ya kuimeza Zanzibar?

  Je tumeshapata sababu ya kuanzisha ubeberu (ukoloni) mpya?

  Je Shirikisho la Afrika la Mashariki la kisiasa( kuunganisha nchi za Afrika Mashariki) liko njiani kuja/ kuundwa?

  Nani kati yetu anapinga kuwa Mwalimu Nyerere alishatuonesha njia kufikia kule tunapotaka, Shirikisho la nchi moja kubwa yenye wanachama wengi?

  Nani atamfunga paka kengele?

  Ni wakati muafaka kwa CCM kuona upepo unakoelekea na kufanya maamuzi magumu.Hapa nimesema CCM kwa sababu ndio wanaoongoza serikali/ nchi.

  Au nini maana ya kauli hizo za Mwalimu?
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Serikali mbili zinatosha ila muundo ubadilishwe kidogo! Tuwe na rais wa jamhuri wa muungano wa tanzania akisaidiana na mawaziri wakuu kutoka Tanganyika na Zanzibar ambao ndiyo watendaji wakuu wa kila upande na wenye mamlaka ya kuwa na mabaraza yao mawaziri. Mambo mengine uliyosema hapo juu yanabaki kama yalivyo.
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Muungano huo ulioasisiwa na vyama vilivyozaa Hichi Chama cha mabwepande uvunjwe
   
 11. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,163
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Selikali moja ndiyo suluhisho.
   
 12. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hayo ndiyo maneno, nakuunga mkono 100%
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono. Muungano ulioshinikizwa na Nyerere na Karume usio na faida kwa pande zote, sioni sababu ya kuwepo.
   
 14. t

  tenende JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,220
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
   
 16. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Ni wazo zuri la kuwa na Serikali tatu(3). Vile vile, Mihimili iwe 4: Bunge,Serikali, Mahakama na Wananchi!
   
 17. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali tatu ndo nzuri bana maana kwa sasa Muungano huu unagharamiwa pakubwa na Tanganyia. TAYADI nakuunga mkono.
   
 18. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  50% kwa 50% ktk muungano wa Serikali tatu ndo sahihi kwa7bu itatupunguzia gharama bara na itaongeza Uhuru wa Znz kujiendesha na kujiamulia mambo yake yenyewe hivyo kupunguza hasira za makundi kama uamsho.
   
 19. mito

  mito JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,612
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Tuendelee tu na serikali hizi mbili zilizopo au tuunde serikali moja tu, tuachane na interest za wanasiasa
   
 20. S

  Sipendi Ubepari JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanganyika ipi?. Ile iliyokufa 1964?. Bila kuirejesha Serikali ya Tanganyika bado wazo lako halijatimia mkuu. Serikali3 haziepukiki kabisa.
   
Loading...