Mkuu Nguvuri3
Nakusoma vyema tu lakini inaonekana umeshindwa kutegua kitendawili cha mwalimu.
Naomba uzipitie hizi.
1.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-moja-nchi-moja-taifa-moja-5.html#post4415616
2.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...cha-zanzibar-un-kirudishwe-4.html#post4439091
3.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...cha-zanzibar-un-kirudishwe-4.html#post4439205
Sasa nikuulize. Wewe unataka Muungano uvunjike? Tuuvunje? Uvunjwe?
Kama jibu ni ndio...Kabla ya muungano kulikuwa na serikali ngapi ? Zipi?
Mwalimu anasema ziwepo serikali ngapi? Zipi?
Maana yake nini?
Au wewe unafahamu serikali moja au tatu hapo?
Bado hutaki kuipigia debe, Tanzania yenye serikali mbili? Ya Tanganyika na ya Zanzibar?
Au unataka tung'ang'anie mazingaombwe?
Mkutano, mashirikiano itakuwa EA federation kama unavyosema ndio itakavyokuwa. Suluhisho rahisi limetolewa na mwenyewe muunda muungano lakini tumekuwa wazito kuelewa.
Nonda, sijui niweke maswali yangu vipi ili nieleweke, hata hivyo nadhani hii ni fursa nzuri sana ya kuwaeleza Watanganyika kwanini tuvunje muungano.
Ni fursa nzuri kwasababu Wazanzibar wameng'ang'ania mkataba au serikali 3. Wasichoweza kueleza ni kuwa hizo serikali 3 zishughulikie nini ikiwa kila jambo tumeshatengana na hata yale tunayodhani yanatuunganisha kama mambo ya nje hutayataki tena.
Hatari kubwa ni kuwa Zanzibar itaendelea kudai hata kile isichostahiki. Kwa mfano, wamedai kuwa tume ya katiba iwe na wajumbe sawa kutoka kila upande. Hilo ni sawa, kinachotatiza ni kuwa ZNZ hiyo hiyo haidai mchango sawa wa kuendesha serikali ya muungano, mambo kama ya ulinzi ameachiwa Tanganyika.
Kwa uchache ni kuwa ZNZ inautaka muungano kuliko Tanganyika vinginevyo wasingebaki kutaka serikali 3 au mkataba.
Kwanini wanataka muungano kama wanavyodai
1. Soko kubwa kwa shughuli zao za kijamii lipo Tanganyika
2. Ustawi wa uchumi wa ZNZ unategemea sana Tanganyika.
3, Soko la ajira za WZNZ linategemea Tanganyika
4. Gharama za ulinzi na usalama zinategemea Tanganyika
5. Gharama za kuendesha serikali ya mapinduzi zinategemea Tanganyika
6. Ufinyu wa ardhi ni tishio kwa mustakabali wa ZNZ,ni Tanganyika wala si Kenya au Uganda wanakoweza kupata uhondo walio nao sasa
Katika orodha hiyo hakuna hata kimoja Tanganyika inategemea ZNZ. Kuvunjika kwa muungano ni mateso kwa WZNZ.
Njia gani wanatumia?
1. Kudai mkataba ili yale mambo yatakayowasaidia kama Ardhi, udogo wa bajeti, na nishati kama umeme viendelee kupatikana bure.
2. Serikali 3, ile ya tatu ni ya mambo yanayohusu matatizo ya ZNZ.
Wasichokijua; Kurejea kwa Tanganyika ni kuondoa kila jambo na kila upande uwe sawa kwa kila kitu. Tanganyika haitakubali kuwaajiri zanzibar kama ilivyo sasa wakati Mtanganyika hatapata ajira visiwani kama ilivyo sasa.
MZNZ itabidi aje Tanganyika kama mwekezaji, masikini wasioweza kulipia hata nauli huo ndio mwisho wao.
Kuhusu Nyerere, yeye aliwahi kusema kama ZNZ watasema hawataki muungano hawezi kuwapiga mabomu. Kauli zake zililenga nyakati hizo na hakika wakati umebadilika. WZN hawataki muungano na hakuna haja ya kuwapiga mabomu. Tatizo ni kuwa wamegawanyika, washirazi wakitaka utawala wa sultani na wanyamwezi wakiyataka mapinduzi.
Nonda, ni kitu cha ajabu sana leo tukitumia mawazo ya Nyerere kuhusu muungano. Huyu Nyerere kule ZNZ ni Laanatullah sasa iweje hata uthubutu kuweka mawazo yake? Nyerere ni muasisi wa muungano lakini wapo wenye nchi wanaoamua hatima ya nchi zao, hao ni mimi na wewe kutokana na mazingira tuliyo nayo.
Mazingira tuliyo nayo yanasema kuwa muungano hauna faida kwa pande zote, moja ikionewa na nyingine ikibeba mzigo wa gharama na lawama. lIlilo jema ni kuachana tukiwa na mapenzi kwasababu haitatokea hata siku moja Tanganyika ikaihitaji ZNZ, lakini ZNZ inaihitaji Tanganyika hata leo hii na hilo ndilo chimbuko la serikali 3 au mkataba.
Serikali 3 ni jawabu baya kwa WZNZ na mkataba lazima Tanganyika ielezwe itafaidika na nini?
Nimekusaidia kujibu maswali na nadhani utatumia fikra na siyo link kufikiri.