Muungano ukivunjika

Hivi likija swala la Referendum watachagua serikali ya mkataba au serikali tatu au kujitoa kabisa?!!
Asilimia 80 watakataa Muungano hio bila ya kujali kabisa.
 
inawezekana watu wa Kagera na Kigoma wakawa jamuhuri kabla ya zanzibar.kwa niliyo yaona kwenye binge LA Katiba, sidhani kama Zanzibar wana ubavu wa kujiondoa kwenye muungano
 
inawezekana watu wa Kagera na Kigoma wakawa jamuhuri kabla ya zanzibar.kwa niliyo yaona kwenye binge LA Katiba, sidhani kama Zanzibar wana ubavu wa kujiondoa kwenye muungano
Kuna watu walishawahi kusema mpemba hawezi kuwa raisi pia walisema mtu mweusi hawezi kutawala USA kwa hiyo mungu ndie ajuaye.
 
Wenzetu wanaungana kwa manufaa. Muungano Tanganyika na Znz hauna manufaa yoyote kwa wananchi isipokuwa kwa maslahi ya viongozi!.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
 
Muungano ufe hata leo usiku kwani mwenye kupata hasara ni Zanzibar, kumbuka Tanzania bara ( Tanganyika) ndiyo anaifuga, kuilea kuilisha Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuilinda kwa gharama kubwa.
 
Muungano ufe hata leo usiku kwani mwenye kupata hasara ni Zanzibar, kumbuka Tanzania bara ( Tanganyika) ndiyo anaifuga, kuilea kuilisha Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuilinda kwa gharama kubwa.
Inawezekana wenzetu FIFA ikawa na umuhimu zaidi.
 
Wenzetu wanaungana kwa manufaa. Muungano Tanganyika na Znz hauna manufaa yoyote kwa wananchi isipokuwa kwa maslahi ya viongozi!.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu
Zanzibar ndiyo hufaidi Muungano kwani Zanzibar imerundika utitiri wa wabunge kwenye kaeneo kadogo huku ikiwa na serikali yake, bendera yake, wimbo wake wa Taifa kwa gharama ya pesa toka Hazina Tanganyika, yaani gharama ya kuvitunza kuvinyonyosha visiwa viwili ni kubwa, na siku Muungano ukifa hakika Tanganyika itakuwa Nchi tajiri kuliko South Africa, pesa ya kuilinda kuitunza kugharamia Zanzibar ikisalia Tanganyika kwa kweli Tanganyika itakuwa Nchi ya Neema.
 
Na Tanganyika kutagawika nchi nyingi, kigoma,mtwara, arusha,kilwa,hawa ukivunjika watadai nchi zao.
 
Ni gharama rahisi zaidi kuuboreshe kuliko kuuvunja swala la FIFA na kero nyingine ni kitu cha kukaa mezani na kulitatua kupitia CCM visiwani.
 
Ukiacha hao wabunge na waliogaiwa uwaziri hao ndio wanaoutaka muungano, sasa kama hesabu zako zitakuwa sawa sijui ni wapi wengi kati ya wanaoutaka na walokua hawautaki.
 
Muungano ufe hata leo usiku kwani mwenye kupata hasara ni Zanzibar, kumbuka Tanzania bara ( Tanganyika) ndiyo anaifuga, kuilea kuilisha Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuilinda kwa gharama kubwa.

Inalindwa Zanzibar kwani imetoka kwenye vita?
 
Na Tanganyika kutagawika nchi nyingi, kigoma,mtwara, arusha,kilwa,hawa ukivunjika watadai nchi zao.
Hizo hazipo na hawajawah kudai. Nyie jaribun kujitenga muone moto wake. Kwa sbb mna serikali yenu sijui hata mlichoshindwa kufanya ni nn. Au mnadhan mkiwa nje ya muungano ndo mtapata misaada zaid. Mawazo yenu ni misaada tu.
 
Kama hujawahi kuwasikia watu wa kigoma jaribu jufika. Tanganyika inalilia misaada na inakomba yote inayokuja kwa Zanzibar pia.
 
Jumuiya ya kimataifa inajua fika kuwa jamhuri ya muungano wa Tanzania ni muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar.
 
Unajifany hujui au unajisahaulisha kuwa Zanzibar pia ipo TRA ambayo inakushanya kodi na kuzipeleka uko bara na ndio hulipwa hao wabunge na sio kwamba iyo mishahara na posho za wabunge wa Zanzibar zinatoka uko Tanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…