Muungano ukivunjika


Nilikua nasubiri uniambie wazanzibar wangapi watapoteza kazi pia?
 
Hivi John Okello alikuwa na chuki sana na Waarabu?!
 
Je John Okello ni Che guavara wa Afrika ya Mashariki,kila nikimsoma huyu jamaa huwa nafikiria sana,aliwezaje kuuangusha Usultani wa miaka dahari?! Imaaminika Okello aliuwawa na Iddi Amini.
 
Familia ya hayati Okello huenda inateseka na maisha huko Uganda,wakati sisi kila mwaka tunashaherekea siku kuu ya muungano.
 
Unajua sisi Waafrika ni watu wa ajabu sana badala ya kujadili siasa zetu za Muungano tunahamia kutukana dini zetu ile habari ya low IQ huenda ikawa ya ukweli

Desemba 1993

MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:

Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.

Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.

Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.

Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.

Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:

Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.

Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.

Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.

Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!

Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
 
Muanze kuondoa jeshi lenu pamoja na watu wasiojulikana mliowajaza kila uchochoro zanzibar
Tuwaondoe kwa kumuogopa nani, Maalim Seif!!!? Mtaondoka nyinyi kurudi kwenu arabuni...kwa babu zenu....[emoji35]
 
Bila mihemko huu uzi ungekuwa wa kujenga sana,kuna haja ya kuanzisha uzi mwingine ambao inatakiwa tujadili bila kuingiza kashfa zozote.
 

Sasa hao wabunge wananufaisha nini wazanzibari?
 

Hivi hizo ni akili zako au ndio chuki tu?
 
Ni gharama rahisi zaidi kuuboreshe kuliko kuuvunja swala la FIFA na kero nyingine ni kitu cha kukaa mezani na kulitatua kupitia CCM visiwani.

CCM visiwani haiwezi kutatua tatizo la aina yoyote. Tatizo la CCM visiwani ni watu ambao hawana kauli wala hawawezi kudai haki yao ya aina yoyote mbele ya CCM bara, kufadhiliwa kitu kibaya sana. Wamekua wakiwaweka madarakani toka 95, unafiki wanaweza kuinua mdomo wakawambia kitu? wanaishia kutii amri tu.
 
Je kuna haja ya kuwa na Ferry kubwa kama hii il watu waweze kwenda na magari yao Znz/Tanganyika ili kuboresha undugu na Muungano?!! Kwa mfano basi linatoka Arusha hadi Stone Town.
 
Je kuna uwezekano Wazanzibari wote kujiunga na CCM ili iwe rahisi kuondoa kero mbalimbali za muungano kwa urahisi?!!
 
Kuna tetesi kuwa Visiwa vya Komoro navyo vinataka kujiunga na muungano wetu wa Tanzania.
 
Mbona Karume jr alikuwa na maamuzi, kwanini swala la FIFA halikuwekwa mezani

Angeendelea mwaka tu mungelimuua.

Tatizo ni nia safi, Bila yakuwa na nia safi hakuwezi kutatuka kwa kero yoyote.
SMT haipo tayari zanzibar wawe na nguvu ya aina yoyote, Hawataki zanibar wawe ni wanachama wa FIFA, kwaiyo hata kukaamezani hapawezekani kupatikana suluhu. Wawape nchi CUF halafu wache walete iyo meza. Lakini kwa wale vibaraka wao tusahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…