Nakubalia na wewe Mia kwa Mia ! Leaved there too, nataka owe kesho ili mbatata zetu, nyama, maharagwe etc etc tuwauzie kwa dola sasa!!. Na Hao wa Inge na Waziri waliopo bars sijui watawapa post gani huko!. Infact Kama wao wakipata mafuta obviously hata sisi tutakuwa nayo. Mungu Ibariki Tanganyikawildernesscamps .
Nimekaa Zanzibar kwa miaka saba sasa, nakuhakikishia inawezekana kukatokea machafuko Zanzibar baada ya muungano. Wazanzibari ni watu ambao ni rahisi kudanganywa na wanasiasa. Na kwa sababu ya wazanzibari wengi kukosa kazi, wana muda mwingi wa kusikiliza uwongo bila kufanya utafiti wa maana.
Tuanze na OIC. Kati ya waisilamu wenye matatizo makubwa ya kimaisha hapa ulimwengini ni Wapalestina. Lakini OIC haiwasaidii Wapalestina badala yake Wapalestina wanaishi kwa msaada kutoka EU. Sasa niwaulize, kulikoni OIC (Jumuia ya nchi za Kiisilamu) zishindwe kuwasaidia waislamu wenzao wa Palesintina ila wawasaidie wazanzibari? Pili nchi gani ulimwenguni humu imeendelea kwa misaada?
Uchimbaji wa mafuta. Huenda ni kweli kuna mafuta Zanzibar. lakini nawashauri Wazanibari walichukulie suala la mafuta kwa makini sana. Kuna nchi zilikuwa na amani sana hapa Afrika, lakini siku tu mafuta yalipoanza kuchimbwa ndio siku walipigana na maelufu wakafa kwa sababu ya mafuta.
Uvuvi. Uvuvi haujawahi kutajirisha nchi hata moja. Norway ambayo ni tajiri sana, huenda tajiri kuliko nchi zote ulimwenguni hawakutajirika kwa uvuvi pekee. Kwanza utajiri wa Norway umekuwa mkubwa pale walipogundua mafuta na kuanza kuyachimba tena wakakataa kujiunga na OPEC kwa hiyo wanachimba bila mashariti ya OPEC.
Utalii. Utalii wa Zanzibar unaendeshwa kiholela na in fact, hakuna cha kuwavutia watalii Zanzibar. watalii wanaokwenda Zanzibar ni wale masikini, wanawaita vishuka. Alafu, hawana skills za kuendeleza utalii. Mahoteli yaliopo yanaendeshwa na Wakenya na Watanzania bara.
Kuna tatizo kubwa la ufisadi ninaloliona Zanzibar japo watu wengi hawalioni. Viongozi ni matajiri sana ukilinganisha na vipato vyao, yaani mshahara. Miaka ya 2006 niliambiwa na mchumi mmoja kuwa kipato cha ZRB kipindi kile kilikuwa 3 Bil kwa mwezi lakini matumizi halali ya serekali yanayolipwa na mapato kutoka ZRB yalikuwa 1.8 Bil. Kwa hiyo kila mwezi 1.2 Bil ambayo ni sawa na 40% ilikuwa inapotea.
Tatizo jingine ni siasa za uhasama. Siasa za Zanzibar ni za uhasama. In fact, alichokisema Nyerere kuwa wazanzibari wanajiita wazanzibari ndani ya muungano ni kweli. Kuna kipindi watu walikuwa hawasali hata msikiti mmoja, kisa yule ni mpemba na huyu ni muunguja. Mbaya zaidi ni kuwa wanafahamiana na itikadi za kichama zinarithishwa kwa watoto. Sio kama Tanzania bara unamkuta Vicent Nyerere ni CHADEMA lakini Makongoro Nyerere ni CCM na wote wanagombea ubunge. Niliona kipindi Vicent Nyerere akifanya kampeni kule Musoma, Madaraka nyerere, japo ni CCM yule, lakini alikuwa anampa support.
Last, nadhani zaidi ya theluthi ya Wazanzibari wanaishi bara. Na mbaya zaidi ni kuwa wale wenye uwezo kielimu na kifedha in terms of mitaji, ndio wako bara. Nimeenda pemba na kuilinganisha na matajiri wa kipemba walioko daa, kwa kweli havifanani.
Muungani japo si upendi kabisa kwa sababu naamini Zanzibar inapendelewa sana, kwa mfano wabunge wanaotoka Zanzibar ambao ni zaidi ya 60 katika bunge la jamhuri ya muungano wakati in terms of resource contribution Zanzibar inachangia kidogo zaidi chini ya mkoa wangu wa Kilimanjaro, naona kama si halali. Wangetakiwa walete wabunge chini ya 10 kama mkoa wangu wa Kilimanjaro.