Muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi

Muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi

Muuza viatu

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2020
Posts
3,839
Reaction score
7,924
Rejea kichwa cha habari hapo juu mara kibao tumewasikia wadau mbalimbal kutoka kada tofauti wakilalamika kuhusu utendaj kazi wa tume ya uchaguzi wengine wamefika mbali zaidi kwa kukosoa upatikanaji wa watendaji waandamizi wa tume ya uchaguzi.

Lakini wote hao sijawahi ona sehemu yoyote wakitoa mtazamo mbadala kuwa kipi kifanyike ili kupata namna ya kuweza kupata watendaji kuanzia waandamizi makao makuu ya tume mpaka wanaosimamia chaguzi za serikal za mitaa.

Kupitia bandiko hili napendekeza wanajamvi tujadiliane kistaarabu kama mara zote tunavyoamin katika demokrasia na uhuru wa kujieleza ukizingatia humu jamvini tuna wasomi wa kada tofauti naamin tutaongezeana maarifa.
 
Never ever sabufa hawez kukubali nfano polisi hawa sekta huru lkn ni waajiriwa serikal ba serikal ndio inawalipa na kuwaajir we unafikir wale wateule wa rais hata wakichapa watu bakora hadharan wanaweza kuwakamata
 
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mkuu awe jaji msitafu ateuliwe na wawakilishi wa vyema vya siasa kwa kupiga kura na alipwe na vyama vya siasa vyenye ruzuku kwa mkataba wa miezi 6 maana yangu mwenyekiti wa uchaguzi mkuu awe ni wa muda
 
Kuhusu mshahara labda watendaj wote waandamiz walipwe na vyama vyenye ruzuku, changamoto yake ni hata hivyo vyama vyenye ruzuku vinalalamikia ukata wa pesa ya kuendeshea vyama vyao.
 
We do not have to reinvent the wheel, it is a matter of copy and paste kutoka democratic countries practising independent electoral committees with some necessary modification to cater for our exceptional need if at all are there
 
Labda tulizane hivi ule mjadala wa Katiba Mpya ulishiaga wapi?

Je, ni nini hasa kilicho kwamisha suala hili?
 
Mkuu wewe ndio mvivu kusoma yalisasemwa mengi Sana na mifano mingi ikalewa. Soma huku jukwani utaona namna walivyofananisha na tume ya uchaguzi ya Kenya na muundo wake.

Ukishindwa kuipata nijulishe nikuoneshe ulivyo mvivu.

Ukishindwa kabisa pitia pendekezo la katiba ya Warioba.
 
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mkuu awe jaji msitafu ateuliwe na wawakilishi wa vyema vya siasa kwa kupiga kura na alipwe na vyama vya siasa vyenye ruzuku kwa mkataba wa miezi 6 maana yangu mwenyekiti wa uchaguzi mkuu awe ni wa muda
Kwa sasa mwenyekiti wa nec ni jaji Kaijage (jaji mstaafu wa mahakama ya rufani)
Kuhusu kulipwa na vyama vyenye ruzuku,
Je vyama visivyo na ruzuku vitatendewa haki?
Hebu tupe rejea mfumo ulioupendekeza unatumika wapi duniani!!??
 
Mkuu wewe ndio mvivu kusoma yalisasemwa mengi Sana na mifano mingi ikalewa. Soma huku jukwani utaona namna walivyofananisha na tume ya uchaguzi ya Kenya na muundo wake.

Ukishindwa kuipata nijulishe nikuoneshe ulivyo mvivu.

Ukishindwa kabisa pitia pendekezo la katiba ya Warioba.
Huko Kenya pia mbona kuna malalamiko ya uchaguzi kutokuwa huru na haki
 
Kuna suala la muundo na Kuna suala la kisheria na suala la utendaji. By default tume ni huru, Ila watendaji wanaweza kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa kuingiliwa au incompetence vyote vinaweza kufanya uchaguzi usiwe huru.

Mfano walichokifanya DED 2020, sio matakwa ya time yetu (pamoja na mapungufu yake) ule ulikua utashi binafsi, kulinda cheo na hata kuingiliwa na mamlaka zingine. Hivyo uchaguzi inakosa Ile sifa tarajiwa
 
Rejea kichwa cha habari hapo juu mara kibao tumewasikia wadau mbalimbal kutoka kada tofauti wakilalamika kuhusu utendaj kazi wa tume ya uchaguzi wengine wamefika mbali zaidi kwa kukosoa upatikanaji wa watendaji waandamizi wa tume ya uchaguzi.

Lakini wote hao sijawahi ona sehemu yoyote wakitoa mtazamo mbadala kuwa kipi kifanyike ili kupata namna ya kuweza kupata watendaji kuanzia waandamizi makao makuu ya tume mpaka wanaosimamia chaguzi za serikal za mitaa.

Kupitia bandiko hili napendekeza wanajamvi tujadiliane kistaarabu kama mara zote tunavyoamin katika demokrasia na uhuru wa kujieleza ukizingatia humu jamvini tuna wasomi wa kada tofauti naamin tutaongezeana maarifa.
Unaweza kuunda Tume huru ya Uchaguzi Tanzania iwapo tu wajumbe wake watakuwa ni malaika wa Mwenyezi Mungu, kinyume cha hapo sahau kuhusu kupata Tume ya aiana hiyo, Tanzania na hata kwingineko.

Kenya walijaribu, lakini angalia kilichowakuta. Ndani ya Tume hiyo kulikuwa na wafuasi wa chama tawala na wale wa Chama kikuu cha upinzani cha Raila Odinga, kiasi cha kuwafanya wajumbe wa Tume kutumikia na kulinda maslahi ya Tume na ya Vyama pendwa vyao sawia, hadi ikafikia wakati, mmoja wa wajumbe akiamua kurejea Marekani kuendelea na kibarua chake, baada ya kusaliti Tume na kupigania maslahi ya chama chake,
 
Back
Top Bottom