Kuwe na kamati maalum ya uteuzi, ihusishe jaji mkuu, mwenyekiti wa tume ya haki za binaadamu, tume ya utawala bora(iundwe sio sasahivi ambapo zimeunganishwa pamoja na tume ya haki za binaadamu).
Asasi za kiraia na vyama vya siasa ziruhusiwe kupeleka majina ya wanaoona wanafaa kwenye kamati ya uteuzi, na yoyote anaetaka kuwa mjumbe wa tume apeleke application kwenye kamati ya uteuzi. Baada ya hapo kamati inayapitia majina na kuwasilisha bungeni. Bungeni kuna kuwa na kamati inayohusisha wabunge toka pande zote. Upande wa serikali na upinzani. Hiyo kamati itayapitia tena hayo majina na kuwahoji. Baada ya hapo itawasilisha tena majina ya watu inayoona wanafaa kisha wanapitishwa kwa kupigiwa kura na bunge zima ili kuwa wajumbe wa tume. Rais yeye anakuja kuwaapisha tu.
Wajumbe wa tume ndo watachaguana wenyewe kati yao ili kumpata mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume.
Ili kumpata mtendaji mkuu wa tume ambae ndo mkurugenzi wa uchaguzi. Watu watawasilisha maombi yao kwa tume ya uchaguzi, kisha tume itayapitia na kupeleka majina kwenye ile kamati ya bunge, nao watayapitia na kuwahoji kisha kuwasilisha jina moja litakalo pigiwa kura na bunge zima na kupitishwa. Baada ya hapo rais anakuja kumuapisha tu.
Tume iruhusiwe kuajiri watumishi wake. Ambao ndo hao hao watasimamia uchaguzi.
Mkurugenzi wa uchaguzi na watumishi wote watawajibika kwa tume na si mwingine. Mtu yoyote asiruhusiwe kuwapa maelekezo.
Wajumbe, mkurugenzi wa uchaguzi na watumishi wa tume wasiwe watu ambao waliwahi kuwa makada au viongozi wa chama chochote na pia kuwahi kuwa watumishi serikalini.
Tume pia iwe na uhuru wa kifedha. Ina wasilisha bajeti bungeni na fedha kuidhinishwa bila mjadala au kufanyiwa editing. Itakuwa ni kinyume cha sheria kwa hazina kushikilia au kuipa tume fedha pungufu kuliko ile iliyoidhinishwa na bunge.
Kumuondoa mjumbe wa tume ni mpaka jopo la kijaji liundwe, na huyo mjumbe apate nafasi ya kujitetea. Jopo la kijaji likifanya uchunguzi na kuthibitisha kuwa anafaa kuondolewa ndo huyo mjumbe aondolewe.
Mwisho kabisa watu waruhusiwe kuomba "admnisitrative review" kuhusu maamuzi ya tume. Kama mtu hajaridhishwa na maamuzi ya tume au mtumishi wake, aruhusiwe kuiomba tume ipitie tena maamuzi hayo. Na kama hajaridhika bado, aruhusiwe kufungua shauri mahakamani. Ambapo tume itabidi ifuate maamuzi ya mahakama.
Yote hayo yakifanyika. Tutakuwa na tume ambayo iko huru na ya haki.