Muundo huu wa Muungano utatuumiza sisi Wazanzibar!

koti likikubana livue... ha ha haaaaa, cheza na baridi, utalivaa tu. na bado hiyo ni rasmu tu. hamna vyuo vikuu (oooh sory nilisahau mnavyo vya kiislam a.k.a madrasa) je, unajua hii,,, vyanzo vya mapato ya serikali ni vipi!!!! najua utasema karafuu, haina soko duniani nowadayz, au utalii, (ni kijisehemu tu cha secta ya huduma tena hoteli ndo kidogo mnategemea) hiyo polisi mnayo taka kuanzisha mtawalipa nini? mtakula urojo mpka mkome....isue ya umeme no msamaha tena, mtalipa kama kawaida hakuna cha dezo, yale magenerator si mlishindwa kuyarun then mnalilia muungano uvunjike....na wapemba nao nasikia tetesi wanataka nchi yao, ha ha haaaaaaa....nawapa mwaka mmoja na maalim seif wenu mtakalia jiwe la moto, mwenzenu anaweza kuwakimbia akaenda huko oman we mwenzangu na mimi vipi?utakimbilia bumbwini......kulalama kwnu na kutoa mapovu juu ya muungano tunawapa mwaka mmoja katiba ikianza kutumika mtakula mabofro mpka mkome
vyuo vikuu vipo bwana acha uongo
 
]Walio zaa watoto tanganyika wataula[/SIZE], kwani watoto hao watakuwa raia wa tanganyika na wanahaki ya kumiliki,na wazee wao wataomba ukaazi wa tanganyika, sasa katika suala la ardhi inategemea na ukaazi wa mtu ambao alio nao, hilo linategemea na shera za ukaazi wenu.

Kwa upande wetu wa zanzibar tutatoa fursa ya ukaazi tu na sio uraia ,ispokuwa kwa mtua mbae amezaliwa zanzibar ila wazee wake sio wazanzibari na mtu huyu ametimiza miaka 18 ana haki ya kuomba uraia, hiyo ndio itakuwa sheria ya zanzibar. Zanzibar ni eno dogo lazima tuweke vikwazo kwa wageni kulinda rasilimali watu na ardhi.
hakuna kitu kama hicho.....huwezi kuwa raia wa nchi hata kama nikwa kuzaliwa wakati wazazi wako kipindi unazaliwa hawakuwa raia wa nchi husika labda kama sheria ya nchi husika inasema hivyo..........labda kama Tanganyika kwa uzembe wataruhusu kitu kama hicho
 
Muundo huu wa rasimu ya unaiweka Zanzibar pabaya kidogo kwa sababu serekali ya mapinduzi ya Zanzibar imeongezwa mzigo zaidi baada ya kupungua kwa mambo ya muungano. Suala kama la elimu, watapambana nalo wenyewe. In fact, itabidi waanzishe baraza la mitihani lao, board ya mikopo yao wenyewe, sijui ZCU yao kama walikuwa hawana (japo nina uhakika itakuwa na viwango vya chini sana). Wabunge watakao ingia kwenye bunge la muungano watakuwa wamepungua kwa mfano, pale Mjini magharibi kutakuwa na wabunge wanne au sita tu kutoka wilaya za mjini na magharibi badala ya hapo walikuwa zaidi ya nane. Japo bado hili litalalamikiwa kwa sababu kwanini majimbo ya Tanganyika yawe Mikoa. Mimi sioni kuwa ni mbaya sana.
Kimsingi katika bunge la sasa hivi la jamhuri ya muungano, wabunge kutoka Zanzibar hawana cha kuchangia kwa sababu mambo mengi yanayozungumziwa pale ni mambo ya Tanganyika.
 
Muundo huu wa rasimu ya unaiweka Zanzibar pabaya kidogo kwa sababu serekali ya mapinduzi ya Zanzibar imeongezwa mzigo zaidi baada ya kupungua kwa mambo ya muungano. Suala kama la elimu, watapambana nalo wenyewe. In fact, itabidi waanzishe baraza la mitihani lao, board ya mikopo yao wenyewe, sijui ZCU yao kama walikuwa hawana (japo nina uhakika itakuwa na viwango vya chini sana).

You got it right!!!
 
Mkuu nyumbani always kutamu, wengine wako Tanganyika kwa utafutaji tu, na si haba kajipatia shamba lake hekari 100 Singida huko na yeye ana maslahi pia Zanzibar, au familia yake yote iko Zanzibar au kotekote; ana nyumba tano za kupangisha Dar, na nyingine tatu ziko unguja; pagumu. Bila shaka u shahidi wa namna tulivyoishi miaka 50 hii, majanga tu. Bila shaka mamlaka husika zitazingatia mwingiliano uliopo ila wasiwasi wangu huenda kukazuka 'hostility and retaliation issues' baina ya wakaazi tofauti wa pande mbili. Tutashuhudia familia moja kuwa na raia wa nchi mbili wengi tu. Lakini pia kwa kila masharti magumu ya ukaazi/uraia au umiliki wa ardhi ya Zanzibar yatapelekea Tanganyika nayo kufanya hivyohivyo kwa ardhi yake, Mungu atuzidishie imaan kwani si mepesi kwa kifupi katika maisha haya mafupi; ulikosewa sana huu muungano kukaa muda mrefu bila kueleweka wala kanuni zozote
Mkuu

Sio zanzibar tu ambayo inamasharti magumu ya ukaazi au ardhi ,ni nchi nyingi tu duniani hasa zile zenye eneo dogo kama visiwa, hivi tukihalalisha ardhi yetu kwa watanganyika kuna eneo litakalo baki ? wazanzibari milioni 1.5 wakati watanganyika karibia milioni 50, lazima zanzibar kuwe na masharti magumu ya ardhi, sio kwa wageni hata wazanzibari wenyewe, lazima waekewe masharti, sio kujenga jenga kiholela.
 
Bendera na mawimbo ya taifa yanawasaidia wakagua magwaride... sisi Wanzibar wananchi twatake fedha mifukoni jama!
...mkuu Kasheshe vipi, leo umekula jicho la samaki nini? nashangaa ghafla umerudisha ufahamu wako wakati siku zote tnapojadili mambo ya msingi huwa unajitoa fahamu.
 
Omereyo Zanzibar ina big historia ukilinganisha na Tanganyika yenu. Tukiwa na mamlaka yetu kamili tutakua na maendeleo makubwa. lakini sijui kwa nini mnatung'ang'ania sijui mnataka nini.
 
ah ah ah, kweli hii ni ngumu kumeza, basi sisi waBARA tmeumizwa kwa kipindi chote cha miaka 49.
tulieni tu sindano itaingia labda mkimbilie omani

Hapo kwenye red, hapo. Tafadhali sana replace na Tanganyika. Tunataka nchi yetu, hakuna kitu kama tanzania bara!

Ninaposoma kwa mafano ibara ya 55, 56 61 nk ya rasimu ya katiba roho inaniuma sana. Inatamka Tanzania Bara, kitu ambacho hakipo!
Karibu Tanganyika!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Bila Muungano au shirikisho hakuna Zanzabar! huo ni ukweli hata kama ni mchungu kumeza! na wazanzibar wakitenga (pemba na unguja) haki ya nani masultani wa kiarabu watarudi na mnaweza kuwa wakwea minazi kama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964!
 
Hapo kwenye red, hapo. Tafadhali sana replace na Tanganyika. Tunataka nchi yetu, hakuna kitu kama tanzania bara!

Ninaposoma kwa mafano ibara ya 55, 56 61 nk ya rasimu ya katiba roho inaniuma sana. Inatamka Tanzania Bara, kitu ambacho hakipo!
Karibu Tanganyika!!!!!!!!!!!!!!!!
Mkuu naomba niulize, hvi Tanganyika maanake ni nini na nani aliyependekeza nchi hii iitwe Tanganyika? Kwani hatuwezi kubadili jina na kuipa nchi yetu jina lenye maana halisi inayoeleweka kwa wananchi wote!
 
Mkuu naomba niulize, hvi Tanganyika maanake ni nini na nani aliyependekeza nchi hii iitwe Tanganyika? Kwani hatuwezi kubadili jina na kuipa nchi yetu jina lenye maana halisi inayoeleweka kwa wananchi wote!

Hiyo nayo ni option nzuri, lakini kuliko kuiita Tanzania Bara bora ibaki Tanganyika yetu. Je, tanga ni Tanzania pwani?
 
Kwa nini unapingana na Ustaadhi Jussa?
Yeye kasema Wazanzibar mmefanikiwa "kuyarejesha" mambo 15 kati ya 22 mlokuwa mnapigania! Waulize wenzio yakhe wale wa 60% za Seif.

Ila Tanganyika ikirudi itabidi ninyi mlio huku "bara" mjieleze vizuri i.e. mna ujuzi gani Watanganyika wasio nao na/au uwezo gani mlio nao kiasi cha ninyi kubaki ktk ardhi ya "ukoloni" kwa mujibu wa Maalim Seif.

So get real and be very afraid.
 
Sio kwa Wanzibar tu, hata kwa serikali ya muungano ambayo itachangiwa na serkali zote mbili.

KinaWarioba wanapendekeza serikali yenye wizara zisizozidi 15. Hii haiingii akilini hata kidogo! kuna mambo gani ya muungano ya kuongozwa na wizara zote hizo? Seriakili ya mUungano wizara 15, Mapinduzi 25, Tanganyika 30. Tayari hizi ni wizara 80!! Nani atabeba mzigo huu?

Wangeenda mbali kuzianisha hizo wizara ingekuwa bora. Sio ajabu tukapata Waziri wa wizara ya safari za Rais, na waziri ofisi ya mke wa rais. Tunakazi ngumu mbele kuliko tunavyofikiri
 
Omereyo Zanzibar ina big historia ukilinganisha na Tanganyika yenu. Tukiwa na mamlaka yetu kamili tutakua na maendeleo makubwa. lakini sijui kwa nini mnatung'ang'ania sijui mnataka nini.
Hebu acha ujinga na utoto aisey, watu wanajadili vitu muhimu wee unakuja na historia, nani kakwambia historia ni "functional mobility". Haya historia kwa mfano inatambua kuwa zanzibar ni nchi ya kwanza kuwa na color televishen Afrika, sasa hii inasaidia nini katika maisha ya watu, hali ya kuwa unaona kuna nchi kama south Afrika ambazo tv zake ni all 'Africa covered'. Kwenye hoja nawe weka substantial augment sio unaleta utoto wa maskani; huoni mwenzio Ghibuu anachojadili?
 
Yaani bado watanganyika tunababaisha tu eti serikali tatu iwepo ya tanzania bara,jamani kwanini isiwe tanganyika?kwanini tulikimbie neno tanganyika??maana ya tanzania ni mchanganyiko wa maneno yaliyotolewa kwenye tanganyika na zanzibar,nina hakika hii haipiti
 
Ndo unafahamu sasa!!!mtoto akilili wembe acha umkate. Muungano unawasaidia sana wzb ila subilini mlivuokua wengi hata zanzibar yenyeww haitoshi. Mkivunja tu cha kwanza ondokei ilj mrudi na passpoti
 
Back
Top Bottom