Muundo huu wa Muungano utatuumiza sisi Wazanzibar!

Mkuu

Sio zanzibar tu ambayo inamasharti magumu ya ukaazi au ardhi ,ni nchi nyingi tu duniani hasa zile zenye eneo dogo kama visiwa, hivi tukihalalisha ardhi yetu kwa watanganyika kuna eneo litakalo baki ? wazanzibari milioni 1.5 wakati watanganyika karibia milioni 50, lazima zanzibar kuwe na masharti magumu ya ardhi, sio kwa wageni hata wazanzibari wenyewe, lazima waekewe masharti, sio kujenga jenga kiholela.
Sipingani na hoja ya maeneo ya visiwa kuwa na sheria ngumu za umiliki wa ardhi, ni kwamba najaribu kuangalia mazingira ya baina ya Zanzibar na tanganyika, sheria ngumu za umiliki wa ardhi zanzibar zipo tokea kitambo na offcourse Tanganyika zipo lakini ziko fairly loose kwa wazanzibari kwa muda mrefu, lakini sasa hivi kutakuwa na mkazo wa sheria husika ikilenga kundi fulani (sjui unanipata hapa?) ndo kile nilichobainisha hostility relationship; Offcourse hata sasa kuna watanganyika wengi tu wanaomiliki ardhi zanzibar na hivyohivyo kwa wazanzibari lakini kuna hali ya kutojali sana japo sheria hususan ya Zanzibar iko wazi na ni ukweli kuwa idadi ya watanganyika wanaomiliki ardhi zanzibar ni 'negligible'ukilinganisha na wazanzibari wanaomiliki Tanganyika. Na hii kwa sababu mahitaji ya ardhi tanganyika ni muhimu sana kuliko zanzibar kutokna na matumizi yake (Higher derived demand) pamoja na kuwa Tanganyika kuna eneo kubwa. Ndo nikasema kunatakiwa busara kali mno maana huu muungano ushakufa huu kwa sisi twenye akili zetu
 
Hiyo Zanzibar itakuwa Somalia nyingine,Mungu apishilie mbali.Watu wabinafsi sana.Huo ubaguzi utawatafuna.Maalim ataanza kudai Jamhuri ya Pemba ili waungane na Mombasa.Nchi kubwa duniani wanaungana,ila nyie Wazanzibari mnajitenga.
 
Nasikia na dodoma kuna uwanja unaitwa Jamhuri Dodoma, na pia kuna shule inaitwa Jamhuri Dodoma. Nao watakuwa wanataka kuanzisha jamhuri ya Dodoma?

Huo ni uwanja wa Jamuhuri Dodoma, wala siyo Jamuhuri ya Dodoma, tafautisha hizo sentensi. Jamaa kasema timu inaitwa Jamuhuri ya Pemba, siyo Jamuhuri Pemba.
 
Then tuandike katiba yetu watanganyika na suala la ardhi liondolewe kwenye mambo ya muungano ardhi ndio rasilimali yetu adimu mtu foreigner mliberali aiachie tu
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Shida Maalim alijua mambo bwerere!
Sasa ardhi yetu aliyochukua kusini tuna mnyang'anya

Mlipe bili za umeme fully na muache kuiua Tanesco.

Elimu ya juu mtasoma kama Foreignerz hamtaki bakini kwenu

Ajira mkajibaze kwenu Bara mtuachie tupumue maana gap ya un employment inakuwa kwasababu ya uznz

Mtuachie tufanye biashara na kodi mtulipe!

Hamna tena budget financing toka bara then mnatuachia mzigo wa madeni.

Huwezi kula keki na bado ukabaki nayo mkononi.
Akuvushaye mto usimuume mgongoni.sasa tafakarini vizuri Matumbo ya Viongozi ama matumbo yenu kipi kwanza?
 
Then tuandike katiba yetu watanganyika na suala la ardhi liondolewe kwenye mambo ya muungano ardhi ndio rasilimali yetu adimu mtu foreigner mliberali aiachie tu

Nafikiri ardhi sio swala la Muungano.so wachague moja
 
Bila Muungano au shirikisho hakuna Zanzabar! huo ni ukweli hata kama ni mchungu kumeza! na wazanzibar wakitenga (pemba na unguja) haki ya nani masultani wa kiarabu watarudi na mnaweza kuwa wakwea minazi kama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964!
Acha kuwatisha wenzako.Hata kama wataishi kwa kukwea Minazi si wapo huru kwenye nchi yao?Watanganyika tumechoka kuendelea KUNYONYWA huku TUKITUKANWA.Bora waende wakaanzishe Maisha Mapya na Waarabu wakipenda.
 
JAJI WARIOBA hakutuelewa wazanzibar tunataka mamlaka kamili ya zanzibar nani kamwambia mambo saba ya muungano hiyo akileta huku tutaipiga kibuti .sisi tunajua kusimamia ajenda yetu ya ZANZIBAR KWANZA MAMLAKA KAMILI

''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR'' kwanza mambo saba ya muungano mwisho chumbeee

Hahahahahaha kwa hiyo muungano kuvunjika utahusisha shuhuli za watu acha hizo wewe
 
Hiyo Zanzibar itakuwa Somalia nyingine,Mungu apishilie mbali.Watu wabinafsi sana.Huo ubaguzi utawatafuna.Maalim ataanza kudai Jamhuri ya Pemba ili waungane na Mombasa.Nchi kubwa duniani wanaungana,ila nyie Wazanzibari mnajitenga.

Mnaonaje watanganyika mkaacha na hao wabinafsi mkaungana na kenya,burundi,uganda,msumbiji ambao c wabinafsi?
 
Shangilieni kutaka Zanzibar yenu, Mpemba Maalim anawatia mkenge, muungano ukivunjika ataanza kudai Pemba yake, hapo ndio mtakuwa mmekwisha kiuchumi maana karafuu na mafuta yote yatabaki Pemba. Halafu mtajitia kutaka nchi ya Kiislamu, hakuna hata mtalii atakaekuja Zanzibar. Wajinga ndio mliwao au mnafikiri mtapata msaada toka IOC mpaka lini? Kwa manufaa gani hakuna misaada bila sababu...yaani wenzenu wachume nyie mle. MUUNGANO UKIFA MMEKWISHA...!
 
Waende zao hatuna hajanao tupunguze na matumizi yasiyo ya lazima, kama galama za umeme, vyuo vikuu, matibabu nk.
Watuchie nafasi zetu kariakoo, namanga, buguruni kwa mnyamani, magomeni mapipa na kwingine kulipokaliwa na wapemba kibao.

Aisee.....wapo wengi knm!!!cjui walikuja na mbio z mwenge!!
 
Hiyo Zanzibar itakuwa Somalia nyingine,Mungu apishilie mbali.Watu wabinafsi sana.Huo ubaguzi utawatafuna.Maalim ataanza kudai Jamhuri ya Pemba ili waungane na Mombasa.Nchi kubwa duniani wanaungana,ila nyie Wazanzibari mnajitenga.

Haiwezi kuwa somali ila fikra zetu sisi wabara wengi hatuwajui wazanzibar tunapandishwa chuki sana na hasa wanaoishi mikoani hawawajui wazanzibar,kwani wewe aliekwambia zanzibar haitaki kuungana nani??au ndio nyie mliokuja dar ukubwani na kuwakuta wazawa tumetulia na kujua kila kinachoendelea,wanachodai wazanzibar wananyonywa sana maana serikali zipo mbili lkn ndani yake kuna utatu umejificha,ikija misaada mingi hubaki bara wakidai kuwa hii haipo ktk muungano lkn je inakuja kwa jina gani km si tanzania??au hujui kuwa jina la TANZANIA ni mchanganyiko wa zanzibar na tanganyika
 
Suali sio serekali ngapi,ni mamlaka kamili.zanzibar kwanza.
Mamlaka kamili ipi tena mnayotaka?, mlitaka serikali tatu...hizo mmepewa, serikali yenu mnayo, na sisi wabara tuliowabeba ninyi miaka 49 bila mamlaka yetu kamili tumepata yetu ambayo ni nyinyi mliipigania, sasa mnataka nini tena?. Let the reality take it's course.
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Jitoeni - kwani mumelazimishwa kuwemo katika muungano. kila kukicha kelele, jitoeni.
 
Mamlaka kamili ipi tena mnayotaka?, mlitaka serikali tatu...hizo mmepewa, serikali yenu mnayo, na sisi wabara tuliowabeba ninyi miaka 49 bila mamlaka yetu kamili tumepata yetu ambayo ni nyinyi mliipigania, sasa mnataka nini tena?. Let the reality take it's course.

Kila mara huwa nasema suala la muungano wa kujadili ni watu wa dar wazawa sio wa mikoani km wewe maana huna ujualo ht moja khs muungano km upo dar naamini umekuja kwa kazi au kuona magorofa,ukisikia mamlaka kamili wanayoyataka wenzetu wa zenji ni kuamua kila kitu serikali yao na sio kupangiwa na sisi wabara,smz kwa sasa haina mamlaka ya mikataba wala kujiunga na sehemu yyte bila ruhusa ya bara,rais wa zanzibar hasaini mikataba na hana ruhusa,pia misaada yyte lazima itambuliwe na bara,juzi membe amekataa misaada ya kwenda zenji,pia nadhani pia huna ujualo usichangie,hizo serikali tatu unazosema km umesikia moja wapo ni serikali ya tanzania bara,wapi kuna neno la tanzania bila ya zanzibar?hv hujui kuwa tanzania ni mchanganyiko wa herufi sawa kutoka tanganyika na zanzibar??au umeikuta tu bila kujua chanzo??ndio maana wanasema km bara kuwe na tanganyika na sio tanzania bara,ukisema tanzania ndani yake kuna zanzibar,na ndio maana nikawa mara nyingi nasema msichangie msiyoyajua maana naamini kuna watu hd leo mwanaamini nyerere ni rais hd leo,tuwachieni sisi wazawa wa dar tujadili maana hapo awali nchi zinaunganishwa tunajua sisi wazawa wa dar na wazanzibar na wa mikoani mlikuja kusikia tu baadae wengine miaka kuwa nchi imebadilishwa jina na kuitwa tanzania na sio tanganyika.
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,

Ulitaka muundo upi kaka?
 
Imani yangu Katiba hii hatimae miaka ijayo itatupeleka kwenye muunganowa serikali moja

Maana tutakuwatumeona mapunguu ya serikali mbili na tatu. kwani mdadhaiko wa kutotimia matarajio ya kupata maziwa na asali utaturudisha na utatuweka pamoja
 
Back
Top Bottom