Uumbaji wa maada muda baada ya muda
Wanasayansi wamefanya tafiti nyingi ili kuelewa mpangilio wa matukio tangu wakati wa kuumbwa kwa ulimwengu na uwiano wa kanuni za kifizikia katika kila tukio. Ukweli ambao unakubalika na wanasayansi katika fani ya fizikia ni kwamba:
* Wakati 0: Wakati huu maada na muda haukuwepo, na mlipuko ulipotokea tuseme ndio saa ilipoanza na nukta sifuri, dakika = 0 (t=0) katika fizikia. Ili tuelewa na kuelezea nini kilikuwepo kabla ya muda huu, hatuna budi tujue sheria za fizikia zilizokuwepo wakati huo kwani kanuni za fizikia za wakati huu hazihusishi wakati huo. Matukio yanayoelezwa na fizikia yanaanza wakati t=10-43 sekunde, ambacho ni kiwango kidogo sana cha muda hata akili ya binadamu haiwezi kukidiriki. Kitu gani kinaweza kufanyika katika muda mfupi kiasi hiki, hili liko nje ya kipawa cha kufikiri na ufahamu wa mwanaadamu. Wanafizikia wanapata taabu sana kutoa nadharia kueleza kwa ukamilifu matukio ya wakati huo. Sababu hasa ni kuwa wamekosa takwimu za kutosha kufanya mahesabu. Ukubwa wa kanuni za mahesabu na fizikia upo katika mida ya viwango vya mwisho wa hapa. Hii ni kwa wakati kabla ya muda huu na wakati wa mwanzo wa muda huu wa mlipuko. Kila maelezo ambayo yapo katika vipimo vya juu vya uwiano yana ukweli ambao akili ya binadamu na wanafizikia wanapata taabu kuuelewa. Uumbaji huu, ambao umeanza kabla ya muda kuwapo, umefanya muda baada ya muda kuwepo kwa matokeo ya maumbile ya ulimwengu pamoja na kanuni za fizikia. Sasa tuangalie kwenye matukio yaliyotokea katika uhakika wa hali ya juu sana katika muda mfupi sana wa mlipuko. Kama ilivyoelezwa hapo juu, katika fizikia, kila kitu kinaweza kuhesabika kutoka sekunde 10-43 na kuendelea. Nguvu (energy) na muda unaweza ukatafsirika baada ya tukio hili. Wakati huu wa uumbaji, joto lilikuwa kiasi cha 1032K. Ili kulinganisha, joto la jua la 108 na ile ya nyota ambayo ni kubwa kuliko jua ni 1011. Kiwango cha juu cha joto kinachopimika ni kiwango cha bilioni ya nyuzi zinazoonesha jinsi joto lilivyokuwa kubwa sekunde 10-43. * Tunapoendelea mbele zaidi ya kipindi hiki cha 10-43 sekunde, tunafikia mahala ambapo muda ni 10-37 sekunde. Muda baina ya vipindi hivi viwili sio kitu ni kama sekunde moja au mbili. Tunaongelea kiasi cha muda mfupi sana zaidi ya chini ya mabilioni ya sekunde. Joto bado ni kubwa sana kama 1029K. Chembe ndogo kama atomu bado itakuwa haijaumbwa. * Hatua moja zaidi tupo katika sekunde ya 10-2. Hii ni moja ya mia moja ya sekunde. Mpaka sasa joto liko kwenye kiwango cha nyuzi bilioni mia moja. Sasa, wakati huu ule ulimwengu wa mwanzo ulikuwa umeanza kutengemaa. Hata hivyo bado chembe chembe kama proton na neutron yenye kuifanya neucleus electron na mwenziwe positron, kwa sababu joto ya mwendo wa ulimwengu wakati huo. Kuanzia muda huu na kuendelea, muda wa kutokea kwa chembe chembe ya sub-atomuic ni muhimu sana. Kila chembe chembe lazima itokee katika muda wake maalum ili sheria ya kifizikia iweze kuelezeka. Ni muhimu sana, ni chembe chembe ipi itokee mwanzo. Ijapo kutatokea hata tafauti ndogo sana katika mtiririko au muda itafanya umbile la ulimwengu kutowezekana. Tuachie hapo na tutafakari kidogo. Mlipuko mkubwa ambao ndiyo nadharia hii ya Big Bang inatoa uthibitisho wa kuwapo kwa Muumba (s.w.) kwa kuonesha kuwa maada inayoifanya ulimwengu haikutokana na chochote. Imeonesha zaidi kuwa matofali ya ujenzi ambayo ni Atomu vile vile yametokea pasipo na chochote chini ya sekunde moja baada ya mlipuko (mpasuko) mkubwa wa Big Bang.
Je! Huoni ya kwamba Mwenyezi Mungu kinamsujudia kila kilichomo mbinguni na kilichomo ardhini na jua na mwezi na nyota na milima na miti na wanyama na wengi miongoni mwa watu? Na wengi (pia) imewalazimu adhabu (ya Mwenyezi Mungu). Na ambaye Mwenyezi Mungu amemfedhehesha, basi hakuna atakayempa heshima. Kwa yakini Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
Surat-Al-Hajj: 18
Mpangilio na uwiano mkubwa katika chembe chembe hizi ni vizuri utambuliwe. Umbile la ulimwengu lina mpangilio na uwiano huu ambao tutauelezea katika maelezo yanayofuatia baadaye. Ni uwiano huu unaotufanya sisi kuishi katika maisha mazuri na tulivu. Kwa kifupi ni mpango huu uliojitokeza ukiwa na kanuni za kifizikia zisizobadilika zilizojitokeza baada ya mlipuko ambao mara nyingi ungetegemewa kuleta uharibifu na michafuko. Hii inaonesha jinsi kila wakati kufuatia kwa kuumbwa kwa ulimwengu pamoja na mlipuko wa Big Bang, ulikuwa na mpangilio mahsusi.
Sasa, tutazame maendeleo kutoka pale tulipoachia.
Tuje sasa kwenye sekunde ya mwanzo ya mpasuko au mlipuko mkubwa. Uzito (density) wa mass wakati huu ulikuwa mkubwa sana. Kutokana na mahesabu, density ya Mass iliyokuwepo ni bilioni 3.8 kilogram kwa lita. Inaweza ikawa rahisi kuielezea nambari hii kama bilioni ya kilogram za tarakimu, kuionesha kwenye karatasi.
Hata hivyo, inakuwa vigumu kuifikiria nambari hii kwa uhakika. Ingekuwa rahisi kuelezea nambari kama tungechukua mlima Kilimanjaro ukawa na density hii, ungeweza kuimeza Afrika au dunia yote na nguvu za mvutano zilizokuwamo.
Sura halisi ya wakati huo ni kuwa joto lilipungua kufikia kiwango cha chini. Wakati huo ulimwengu ulikuwa na umri wa kiasi cha sekunde 14, na joto lilikuwa kama nyuzi bilioni tatu na lilikuwa linatanuka katika kiwango cha juu kabisa. Hatua nyingine ni pale muda uliokuwa umemalizika ni sekunde 10-1. Muda huu, kiwango cha joto ilikuwa nyuzi bilioni 30. Wakati ambapo muda ulikuwa sifuri t=0. Wakati huu Neutrons na positrons, chembechembe zilizo katika Atomu zilianza kujitokeza. Neutrons na positron zina miundo maalum ambayo tutaitazama baadaye, ziliumbwa kutoka na kisicho chochote katika muda ambao ni chini ya sekunde. Hii ni hatua ambayo nucleus ya chembe chembe za Atomic, kama vile Haidrojeni na Helium, ilikuwa imeanza kujitengeneza. Zile za proton moja na neutron moja zilipata hali munasibu kwa kuwepo kwake. Chembe chembe hizi mbili ambazo zina mass katika nafasi ya ama kuwepo au kutokuwepo kwa sababu ya nguvu ya uvutano iliyokuwa inapingana na kasi ya kutanuka.
Ni wazi kuwa hali hii inahitaji maendeleo yenye udhibiti wa uhakika na uangalifu mkubwa. Mpasuko mkubwa unatoa nafasi kwa uwiano na mpangilio madhubuti. Protons na Neutrons zimeanza kuja pamoja kufanya tunachokiita Atomu, ambayo ni matofali ya kuundia Maada(matter). Ni kweli kwa ujumla wake haiwezekani kwa chembe chembe hizi kuwa na nguvu ya kufikirika kuweka uwiano sahihi wa kuwepo kwa Maada. Jumla ya dakika 34 na sekunde 40 kupita kuanzia mwanzo, Ulimwengu wetu sasa una umri wa nusu saa. Joto limeshuka katika kiwango kikielezeka kwa bilioni hadi nyuzi milioni 300. Electrons na positrons ziliendelea kutoa nguvu baada ya migongano. Kwa sasa hivi idadi ya chembe chembe ambayo ilihitajika kuumbika kwa ulimwengu ilikuwa tayari imetosha kwa kutokea kwa ulimwengu na vilivyomo. Muda baada ya matukio haya, joto la ulimwengu lilishuka na kuwa nyuzi bilioni moja hivi. Joto hili ni mara 60 ya joto la katikati ya jua. Baada ya kupita kwa dakika 3 na sekunde 2 baina ya wakati huu na sekunde. Kwa sasa, sub-atomic (chembe chembe) kama vile photos, protons, anti-protons, neutrinos zilikuwa zimekwishajaa ulimwenguni. Uwingi wa chembe chembe hizi zilizotajwa na maingiliano yao ni kitu ambacho ni muhimu sana sana. Kiasi ambacho ikitafautiana kidogo tu kwa kiwango cha chembe chembe hizi basi nguvu iliyo baina yao itadhurika na kuzuia mabadiliko ya nishati (energy) kuwa Maada (Matter).
Tuchukulie mfano wa electrons na positrons: Chembe mbili hizi zinapojumuishwa pamoja, nishati (energy) hutokea. Kwa hivyo, idadi ya chembe chembe hizi ni muhimu sana. Tuseme idadi 10 ya eletrons na 8 ya positrons zimekutana. Kwa hali hii idadi 8 ya 10 ya electrons inaingiliana na 8 ya positrons na kutoa nishati (energy). Na matokeo yake idadi ya 2 ya electron inatolewa. Kwa sababu electron ni moja ya chembe chembe inayofanya Atomu ambayo ni sawa na matofali ya ujenzi wa ulimwengu, inatakiwa ipatikane katika kiwango kinachotakiwa ili ulimwengu uwepo. Kwa mfano huo hapo juu, kama idadi ya positrons itakuwa zaidi ya electrons, basi kutakuwa na mabaki ya positrons badala ya electron kwa sababu ya kutolewa kwa nguvu (energy released), na ulimwengu wenye vitu usingeweza kutokea. Kama idadi ya pasitrons na electrons zingekuwa sawa, basi nguvu (energy) ingekuwepo na kusiwe na chochote kilichobakia kuufanya ulimwengu wa material.
Pamoja na yote, idadi hii ya ziada ya electrons imepangika katika namna ambayo inakubaliana sawa sawa na idadi ya protons zilizopo ulimwenguni kwa ajili ya muda unaofuatia. Katika Atomu itakayojitokeza baada ya hapa, idadi ya electrons na protons zitakuwa sawa.
Idadi ya chembe chembe hizi zinazojitokeza baada ya mlipuko huu mkubwa wa Big Bang, zimeweza kuhesabiwa kwa uhakika saana, na baadaye kufanya matokeo ya ulimwengu wenye vitu ndani yake.
Profesa Steven Weinberg alipoelezea migongano kati ya chembe chembe hizi alisema:
Kama ulimwengu katika muda mfupi ulikuwa na idadi sawa ya chembe chembe - (particles na antiparticles), zingeungana wakati joto lilipokuwa linateremka chini ya nyuzi 1000 na isingebakia chochote ila mionzi. Kuna ushahidi mzuri saana dhidi ya uwezekano huu.
Lazima kumekuwepo na electrons za ziada kulinganisha na positrons, vile vile protons kulinganisha na anti-protons, hivyo hivyo neutrons ukilinganisha na antineutrons, ili kuwepo mabaki ambayo yatakinga yaani particles na anti-particles ili kuwezesha kuwepo kwa Maada (Matter) katika ulimwengu huu.
Iwapo kasi ya mlipuko ingepungua, chembe chembe hii ambayo ina mass ndogo sana sana ingeanza migongano. Atomu ya kwanza ya Haidrojeni ingejitokeza kwa kutulizana kwa electron katika njia ya mzunguko wa Proton.
Kufanyika huku kunafanya kuwepo kwa msukumo wa msingi (fundamental force) ambao ni wa kawaida kukumbana nao katika ulimwengu.Bila shaka yoyote, haiwezekani chembe chembe hizi, zenye mpangilio wa ajabu na nyeti sana katika uwiano unaounda maumbile uwe umetokea pasipo aliyeuunda.
Ukamilifu huu umewafanya watafiti wengi wa somo hili kuwa na hitimisho:
Ni uumbaji ambao hauna kifani na haulinganishiki na mtu yeyote aliyekuwa mkaguzi wa kazi hii hatua baada ya hatua.
Kila chembe chembe inayoumbwa baada ya mlipuko ilifanyika katika muda wake maalum, katika nyuzi joto na mwendo maalum.
Inaonekana kama mfumo huu ulikuwa kama saa iliyopangwa katika namna makini zaidi ya akili ya binadamu. Hii ina maana mlipuko wa Bing Bang na umakini wa ulimwengu uliotokea baada yake, ulikuwa umepangwa kabla ya mlipuko na baada yake.
Nani aliyejua, aliyepanga na aliyedhibiti kabla na baada ya ulimwengu kuwepo, si mwingine ila Muumba wa kila kitu.
Mpango huu huonekana sio tu katika Atomu bali na katika vitu mbalimbali katika ulimwengu, vikubwa na vidogo. Chembe chembe hizi ambazo zimekuwa zikikimbiana katika mwendo wa mwanga sio tu zimesababisha kutengenezwa kwa Haidrojeni atomu lakini pia zimesababisha mifumo mingi iliyopo kwenye ulimwengu wa leo, pamoja na atomu, moleckyuli, sayari ikiwa pamoja na jua na mifumo yake, makundi ya nyota, mawimbi, mwanga na radio mbalimbali, na kadhalika.
Ni ujinga uliopindukia kuzungumzia kwamba haya yote yametokea tu kwa bahati nasibu. Mwenyezi Mungu (s.w.) anahusika katika mpango huu madhubuti na usio na mashaka mashaka.
Atomu za aina nyingine zilizojitokeza baada ya ile ya Haidrojeni, ambayo ni maajabu kweli kweli. Mtu anaweza kujiuliza maswali kama vile Jinsi gani atomu zilivyotokea? Kwanini protons na neutrons zote zitengeneze Haidrojeni atomu pekee? Kwa namna gani chembe chembe hizi ziamue ni atomus gani zitokee na kwa idadi ipi? Majibu ya maswali haya yanatuongoza katika hitimisho lile lile - muhusika ni Mwenyezi Mungu (s.w.).
Kanuni za fizikia ambazo zimetokea baada ya Big Bang hazijabadilika kwa takriban miaka bilioni 17 iliyopita. Zaidi ya hayo sheria hizi zinatokana na mahesabu ya uhakika sana ambayo yangekuwa yamekosewa kidogo tu hali ya ulimwengu wa sasa isingekuwepo.
Maneno ya mwanafizikia maarufu Profesa Stephen Hawking kuelezea swali hili kuwa ni mahesabu makini zaidi ya tunavyoweza kufikiria yanasema:
Kama kiwango cha mtanuko baada ya mlipuko mkubwa - Big Bang kingekuwa kidogo kwa angalau moja kwa mia moja elfu milioni milioni, ulimwengu huu ambao ulikuwa na kupasuka, ungeangamia kabla haujafikia kiwango chake cha sasa.
Kuelezea haya Mwenyezi Mungu (s.w.) anasema:
Na amekutiishieni usiku na mchana na jua na mwezi. (Vyote vimeumbwa kwa ajili ya maslaha yenu). Na pia nyota zimetiishwa kwa amri yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wenye akili.
Surat Nahl:12
Nadharia ya Big Bang ambayo imeegemea mahesabu makali sana inaonesha muda (time), nafasi (space), na maada (matter) hazikujitokeza zenyewe tu, bali zimeumbwa na Muumba (s.w.). Ni kweli kuwa haiwezekani kwa matukio yaliyokwishaelezewa kuwa ni ya kubahatisha.
Ndio maana, wanasayansi wengi kwenye somo hili wanakubali msukumo(force) mkubwa usio na kiwango umekuwepo katika maumbile ya ulimwengu. Mnajimu anayejulikana sana High Ross anamuelezea muumbaji wa ulimwengu kama asiye na mfano:
Kwa maelezo, muda unatumika kuelezea matukio ya mambo mbalimbali. Hakuna muda, hakuna chanzo wala hakuna kinachotokea. Kama chanzo cha muda ni sambamba na mwanzo wa ulimwengu, kama muda-wa nafasi, nadhariya inasema, chanzo cha ulimwengu lazima iwe ni kitu kinachoendelea katika muda ambao hausiani kabisa na kuwepo kwa kiwango cha muda cha Cosmos... na inatueleza Mwenyezi Mungu (s.w.) hayupo katika ulimwengu huu.