Rais Mwinyi aweka Jiwe la Msingi katika Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) - Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Bodi na Menejimenti ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa kuona umuhimu wa ujenzi wa Ofisi na maabara kwa lengo la kuimarisha huduma za Nguvu za Atomu Zanzibar.

Aidha, Dk. Mwinyi amesema Uwekezaji huu utaimarisha udhibiti wa matumizi salama ya mionzi pamoja na kuimarisha utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi katika Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) - Zanzibar. Leo tarehe 16 Februari, 2023. Dunga Zuze, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
IMG-20230216-WA0038.jpg
 
Back
Top Bottom