Muswada wa Mahakama ya Kadhi kutikisa Bunge

wapewe mahakama ya kadhi lakini wajiendeshe wenyewe

wamepewa hawataki wanataka itambulike kisheria

swali ni kwanini wanataka iingie kwenye katiba ya nchi .

nilishawahi kusema haya ni malengo ya miaka miamoja ya kutekeleza plan zao za OIC za kikao kilichokaa kartum sudani mwaka 1976 kama sikosei hapo.

na malengo yao ni mawili tu.

la kwanza ni kueneza uislam duniani hata kwa kumwaga damu.

la pili ni kuhakikisha kuondoa israel katika uso wa dunia .

yanayotokea sasa hivi katika nchi za kiarabu ni baada ya mataifa ya magharibi kustukia huo mchezo sasa ndio wamepandikiza chuki za wenyewe kwa wenyewe ili wasiwe na umoja
 
Ivi hawa wakiristo kumbe hawana akili ata kidogo sasa Mahkama ya Kadhi inaenda kushughulikia matatizo ya waislamu wao kinachowauma ni nini? Kama wao katika hiyo dini yao hakuna utaratibu huo kwanini waislamu wawaekee mguu? ndo mana kuna maandiko kwenye bibliya wakiristo ni mbwa.
 
mkuu kuna kitu nashindwa kuelewa hapa. hii sheria ilikuwepo hata kabla ya uhuru na baadaye nyerere alikuja kuifuta mwaka 1964. hivi aliwashirikisha waislam wakati anafuta?
au utawala wa kikoloni uliwajali zaidi waislam kuliko hata huu utawala wa watanzania wanzao?
mbona hizo mahakama zipo nchi mbalimbali na maisha yanaendelea? hizi mahakama zipo hata kenya, s.afrika na kwengineko. tatizo hasa ni nini hapa?
Kwenye hizo nchi ulizozitaja waislamu wamejianzishia wenyewe na wanaziendesha wenyewe. Tatizo la hapa tanzania wanataka waanzishiwe na serikali na pia serikali izigharimie.
 
Ivi hawa wakiristo kumbe hawana akili ata kidogo sasa Mahkama ya Kadhi inaenda kushughulikia matatizo ya waislamu wao kinachowauma ni nini? Kama wao katika hiyo dini yao hakuna utaratibu huo kwanini waislamu wawaekee mguu? ndo mana kuna maandiko kwenye bibliya wakiristo ni mbwa.
Hili suala lifanyeni wenyewe msiingize serikali huko, litaleta sintofahamu katika jamii, imagine polisi mkristo katumwa na kadhi kuja kumkamata mtuhumiwa aliyekimbilia msikitini, atafuata taratibu zenu za kuingia msikitini? si ndo mwanzo wa ugomvi?
 
Hili suala lifanyeni wenyewe msiingize serikali huko, litaleta sintofahamu katika jamii, imagine polisi mkristo katumwa na kadhi kuja kumkamata mtuhumiwa aliyekimbilia msikitini, atafuata taratibu zenu za kuingia msikitini? si ndo mwanzo wa ugomvi?
Nahisi kanuni za Dini yao ni za kulazimisha watu kufuata matakwa ya Mungu wao.Mungu wao amewapa mamlaka ya kuwaadhibu watenda maovu.
 
Hili suala lifanyeni wenyewe msiingize serikali huko, litaleta sintofahamu katika jamii, imagine polisi mkristo katumwa na kadhi kuja kumkamata mtuhumiwa aliyekimbilia msikitini, atafuata taratibu zenu za kuingia msikitini? si ndo mwanzo wa ugomvi?
Duh ama kweli dunani kuna mambo, sasa leo hi mapolisi wanaingia misikitini kukamata watu pasipo hata amri ya Kadhi. Halafu mahakama ya kadhi ni mahakama ya madai yaani kesi za madai ya watu kutaka maamuzi ya malipo kulingana na maamrisho ya dini. Iwe mirathi ama unyumba na kadhalika haihusiani kabisa na maswala ya jinai ama kesi zinazotakiwa uende kutoa report polisi.

Leo hii ukiwa na kesi yoyote ya mada, Polisi watakwambia sio kazi yao, nenda mahakama ya madai (inatambuliwa kisheria)ambako utasimamisha madai yako. Ukiona mtu kakutumia Polisi ktk kesi ya madai basi jua kuna hofu ya uvunjaji amani baina ya mshitaka na mshitakiwa.
 
images
images
images


  • Suala la kuanzisha Mahakama ya Kadhi limo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo na unalenga kufanya mabadiliko katika Sheria ya Tamko ya Sheria za Kiislamu Sura ya 375 ili suala hilo litambuliwe kisheria.
  • Jukwaa la Wakristo linaloundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT) wapinga mswada huo.

Wakati mjadala mkali ukitarajiwa kuibuka katika Mkutano wa 18 wa Bunge unaoanza leo kuhusu uanzishaji Mahakama ya Kadhi, Jukwaa la Wakristo Tanzania limeitaka Serikali kuachana na muswada huo ili kuepusha kuvunja misingi ya Taifa inayopinga ubaguzi na kutofungamana na dini yoyote.

Suala la kuanzisha Mahakama ya Kadhi limo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wiki ijayo na unalenga kufanya mabadiliko katika Sheria ya Tamko ya Sheria za Kiislamu Sura ya 375 ili suala hilo litambuliwe kisheria.

Endapo muswada huo ambao tayari umechambuliwa na wadau utapitishwa, katika sheria hiyo kutafanyika marekebisho kwenye kifungu cha tatu baada ya maneno ‘all courts' (Mahakama zote) wataongeza maneno ‘including Kadhi Courts' (Ikijumuishwa na Mahakama ya Kadhi).

Hata hivyo, Jukwaa la Wakristo linaloundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT) limesema mapendekezo hayo "yanaibua mambo mazito ya kikatiba ambayo hayawezi kuamuliwa na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na sheria hiyo itawaathiri hata wenye imani tofauti."

Tamko la Jukwaa hilo lililokutana Januari 20 kujadili uanzishwaji wa mahakama hiyo ni mtihani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye Septemba 29, mwaka jana katika mkutano wa Bunge la Katiba aliahidi kuliwasilisha suala hilo katika mkutano wa Bunge unaoanza leo ili kuanza mchakato wa uanzishwaji wa chombo hicho.

Pinda alitoa ahadi hiyo kuwapoza wajumbe wa Bunge hilo kutokana na baadhi yao kuhamasishana kuipigia kura ya kukataa Rasimu ya Katiba, iwapo chombo hicho kisingeingizwa katika Katiba.

Pinda aliahidi ifikapo Januari 2015, Sheria ya Mahakimu, sura ya 11 na Sheria ya Kiislamu sura ya 375 zitafanyiwa marekebisho ili kutambua Mahakama ya Kadhi kwa lengo la kuhakikisha umoja na mshikamano vinadumu kwa Watanzania.

Wapingwa katika Kamati
Uanzishwaji wa mahakama hiyo pia uliibua mvutano mkali katika vikao vya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wiki iliyopita na wajumbe walisema uwezekano wa kuanzishwa kwake ni mgumu.

Katika vikao hivyo, ilielezwa kuwa kati ya wadau 15 kutoka taasisi za dini, wanaharakati, wanasiasa, wanasheria na wasomi waliofika mbele ya kamati hiyo, ni mdau mmoja tu aliyekubali kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Miongoni mwa wadau hao ni; Islamic Propagation Centre (IPC), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, CCT, TEC, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania.

Wengine ni Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (BMKT), Mwakilishi wa Kanisa la Wasabato (SDA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Profesa Abdallah Safari na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Tamko la Jukwaa
Katika tamko lake, Jukwaa wa Wakristo limetoa hoja nane likieleza kuwa ni mapendekezo makubwa yatakayokuwa na athari kubwa na nzito kwa kuwa yanahoji msingi wa dola ya Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini.

SABABU NANE

  1. Lcha ya sababu na madhumuni ya muswada huo kuwa ni kutambua Mahakama ya Kadhi, kwa utaratibu wa sasa wa kisheria, Mahakama za Kadhi hazipo. "Kwa maana hiyo, hoja ya kutambua uwepo wa mahakama hizo si sahihi. Kama inavyofahamika, Mahakama za Kadhi, pamoja na Mahakama za Wenyeji (Native Courts), zilizokuwapo wakati wa ukoloni, zilifutwa na Sheria ya Mahakama za Mahakimu ya mwaka 1963. Tangu wakati huo, mahakama hizi hazipo na hazitambuliwi na sheria yoyote na mapendekezo ya muswada huu yakipitishwa ndiyo yatazianzisha."
  2. Kwa mapendekezo hayo, ni wazi kuwa Serikali inachukua jukumu la kuanzisha yenyewe taasisi za kidini kinyume na utaratibu wa kikatiba na Serikali imekuwa haijishughulishi na uanzishwaji na uendeshaji wa taasisi za kidini. "Sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu (Inayorekebishwa) haikuanzisha mahakama au taasisi nyingine yoyote ya kusimamia sheria hiyo bali iliweka utaratibu wa mahakama za kawaida kuitambua na kuisimamia sheria hiyo."
  3. Mapendekezo hayo yanampa Waziri Mkuu mamlaka ya kutunga kanuni za utekelezaji wa uamuzi, hukumu na amri za Mahakama za Kadhi. "Kwa maana hiyo dola ya Tanzania, siyo tu inakusudia kuanzisha mahakama ya kidini, bali pia kuweka utaratibu wa kutekeleza uamuzi, hukumu na amri za mahakama hizo."
  4. Mapendekezo hayo yanafuta utaratibu ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka hamsini, ambao unatambua matumizi ya sheria za dini zisizokuwa za Kikristo katika masuala ya hadhi ya mtu, mirathi, ndoa na talaka kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, Mirathi na Talaka.
  5. Kwa mapendekezo ya muswada huo, hakuna uhakika kama mamlaka za mahakama za sasa za kusikiliza na kuamua masuala ya hadhi ya mtu, mirathi na ndoa kwa mujibu wa Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu itaendelea kuwapo. "Aidha mapendekezo ya muswada huu yako kimya juu ya uhusiano wa Mahakama za Kadhi na mahakama za kawaida. Kwa mfano, haieleweki kama kutakuwa na utaratibu wa rufaa, marejeo na mapitio ya uamuzi wa mahakama hizo…"
  6. Mapendekezo hayo yako kimya juu ya kesi zinazohusu Waislamu na watu wa imani nyingine, kwamba hata kwa wadaiwa ambao ni Waislamu, ikiwa upande mmoja (mdai) unakwenda kwa hiari ila upande mwingine (mdaiwa) unataka shauri lisikilizwe na mahakama ya kawaida, muswada hautoi jibu nini kifanyike.
  7. Baadhi ya madhehebu na taasisi za Kiislamu hazikubaliani na mamlaka ya Mufti kwenye masuala yao, hivyo kumpa Mufti mamlaka ya kutunga kanuni zitakazotumika katika Mahakama za Kadhi na kuwateua makadhi, kunaweza kusababisha migongano na migogoro ndani ya jamii za Waislamu.
  8. Haturidhiki na hoja kwamba mahakama hizo hazitatumia fedha za umma. "Mfano, Waziri atakapokuwa anatunga kanuni atatumia fedha na rasilimali mbalimbali za umma. Vilevile, utekelezaji wa amri na hukumu za mahakama hizi utahitaji polisi na madalali wa mahakama ambao wanalipwa kwa fedha za umma."

Chanzo:
Mwananchi Publication


Imekuwa kawaida kwa Kanisa kufanya kila juhudi kuhujumu lolote
lile lenye manufaa na Uislam na Waislam kwa kupitia mawakala
wake walio ndani ya serikali ya Tanzania.

Mifano iko mingi na hapa JF mimi binafsi nimeshaitoa JF katika
mijadala kadhaa.

Kanisa limepinga EAMWS kujenga Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
mwaka 1968.

Hii ilipelekea hadi kuvunjwa kwa taasisi yenyewe EAMWS iliyokuwa
inataka kuwaletea Waislam maendeleo.

Katika miaka ya 1980 OIC ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania
Kanisa tena likitumia mawakala ndani ya serikali wakahujumu na
chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda.

Katika miaka hiyo hiyo Darul Imaan ya Saudi Arabia ikataka kujenga
Chuo Cha Ufundi Kibaha Kanisa likahujumu Aboud Jumbe akaiomba
Darul Imaan wahamishie mradi huo Zanzibar na Chuo Kikuu Cha
Tunguu kikajengwa.

Zanzibar ikajiunga na OIC mwaka wa 1993 na mawakala wa Kanisa
ndani ya Serikali ya Tanzania wakaja juu na sakata lake ni maarufu.

Nitaweka hapa kiungo atakae asome ajue ukweli:
Zanzibar Membership to Organisation of Islamic Conference (OIC) and Islam in Africa Organisation (IAO) - Mohamed Said

Haya ni baadhi tu ya madhila ya ubaguzi yanayotukuta Waislam
wa Tanzania.

Leo tunaposikia ati tukiwa na Mahakama ya Kadhi ''itavunja umoja
wakitaifa,'' huu unakuwa mzaha mbaya kwetu Waislam.

Viongozi wetu wachunguze watajua ukweli ikiwa kweli hawajui.

Kinachopiganiwa na Kanisa si umoja wa kweli bali muondelezo wa
Mfumokristo uliodumu toka tulipopata uhuru.

Mfumo ambao umeweza kulipa Kanisa Katoliki 76% ya viti katika
Bunge na hiyo 24% iliyobaki ikiwa chini ya madhehebu mengine
ya Kiprotestanti wakigawana na Waislam na Waislam hao mgao
wetu ni 6%.

Atakae kujua ukweli huu na akasome kitabu maarufu cha Dk.
John Sivalon.

Yako mengi lakini haya yanaweza kuwafanya watu wakafikiri.
Ikiwa ipo haja In Sha Allah nitaeleza mengine.

Sasa kwa kumalizia.
Hili la Mahakama ya Kadhi Waislam tunasubiri.
 
Mahakama ya kadhi si majengo waislamu wanaitaje kutambulika kwa mahakama ya kazi. Mahakama ambayo haito muhusu asiyekua muislam. Hakuna umwagaji damu utakao jitokeza kwa kutambulika kwa mahakama hii. Ila ni propaganda zinazoenezwa na wakristo kupinga mahakama hii bila sababu za msingi
 
mkuu kuna kitu nashindwa kuelewa hapa. hii sheria ilikuwepo hata kabla ya uhuru na baadaye nyerere alikuja kuifuta mwaka 1964. hivi aliwashirikisha waislam wakati anafuta?
au utawala wa kikoloni uliwajali zaidi waislam kuliko hata huu utawala wa watanzania wanzao?
mbona hizo mahakama zipo nchi mbalimbali na maisha yanaendelea? hizi mahakama zipo hata kenya, s.afrika na kwengineko. tatizo hasa ni nini hapa?

Yawezekana ilikuwa vigumu sana ku-practise equality na secularism ukizingatia kwa waingereza divide and rule ilikuwa ndio mbinu iliyokuwa inalipa kiutawala. Halafu kuwa na mahakama ya kadhi, ita-fall wapi kwenye judiciary ambayo ni moja ya branches za state.

Mi nilifikiri Islamic Banking ingewatosha ingawaje ni kinyume na cha sheria za nchi ambayo ilisimamiwa na Prof. Assad.

Hawa jamaa mwisho wa siku watadai katiba iseme kigezo cha kuwa raia wa Tanzania ni kuwa muislamu kama kila wanachoomba wanapewa!!
 
MNATAKA KUTEKELEZA HAYA? JIENDESHENI WENYEWE...................







MKUTANO WA UISLAMU BARANI AFRIKA:
TAMKO.

LIMETOLEWA KWA PAMOJA NA BARAZA LA KIISLAMU, LONDON, SHIRIKA LA UMOJA WA KIISLAMU (OIC) NA CHOMBO KILICHOUNDWA PUNDE, YAANI SHIRIKA LA UISLAMU BARANI AFRIKA (ORGANISATION - IAO).

Sisi wajumbe (wote) tuliojumuika hapa jijini ABUJA leo tarehe 1 Jumata AL Awawal 1410 (28/11/1989) tukiongozwa na dhamira kuu ya kuunda CHOMBO CHA KIISLAMU chenye mizizi dhabiti ndani ya Uislam chenye lengo la kuendeleza matumaini ya joja au matakwa ya Uislamu barani Afrika, na kuratibu kazi za Kiislamu zinazoendelea kutekelezwa na jamii na mashirika mbalimbali ya Kiislamu kuanzia miradi inayoweza kusaidia kuboresha maisha ya Uislamu Barani Afrika na katika ulimwengu wa Waislamu kwa jumla, TUNAAMUA KAMA IFUATAVYO:

Tunatoa wito kwa Waislamu kote Barani Afrika waungane wakiwa kiungo muhimu cha umma wa Kiislamu uliobarikiwa kupewa muongozo na huruma vilivyoletwa na mjumbe wa Allah yaani Muhammad (amani iwe juu yako).

Tunahimiza Waislamu waliotenganishwa na vigingi na tofauti za mipaka isiyo na uhalisia ya kijografia na kisiasa iliyalazishwa na watu juu yao ambayo imewekwa na mabeberu kwa maslahi yao ya kikoloni na isiyozingatia maslahi ya Waislamu, ilikwamba waislamu barani Afrika waache kujali mipaka hiyo bandia na badala yake waweze kushirikiana na ndugu zao wote katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa minajiri ya kuusimika upya umma imara na ulio ungana wa kiislamu wenye kudhamiria kutekereza amiri za Allah muweza wa yote.

Tunatoa wito kwa ulamaa (wanazuoni wa dini ya kiislamu) wa ushirikiano utakao rahisisha kupatikana kwa umoja miongoni mwa jamii nzima ya kiislamu hususani vijana.

Tunatoa wito kwa waislamu wote kuyafanyia mipitio mitaala inayotumika kufundisha katika taasisi mbalimbali za elimu kwa lengo la kuifanya iendane na maadili, malengo na misingi ya kiislamu na kutumikia mahitaji ya jamii.

Tunahimiza waislamu wote wawe makini zaidi kuhusu elimu kwa wanawake katika ngazi zote.
Tunahamaisha ufundishaji wa Lugha ya Kiarabu ambayo ndiyo lugha ya Kuran sanjari na lugha kuu za asili barani Afrika na kufanya kila jitihada ili utaratibu wa matumizi ya maandishi (script) ya Kiarabu katika kuandika lugha kuu za Kiafrika urejeshwe.

Mkutano unatambua na kupongeza sana juhudi zinazofanywa na vijana wa kiislam katika kuutumikia uislam na unaahidi kuwaunga mkono katika kazi yao hiyo adhimu.

Tunawahimiza waislam waanzishe mahusiano imara ya kiuchumi kati ya nchi za Kiislam za Bara la Afrika na pande nyingine za ulimwengu wa Kiislam ili kurahisisha usaidizi na ushirikiano katika nyanja za biashara, viwanda na fedha katika pande hizo, kwa lengo la kujenga mfumo imara wa kiuchumi wenye misingi yake katika Uislam.

Mkutano umebaini vilio na milalamo ya waislam wote barani Afrika ambao wamenyimwa haki yao ya kutawaliwa kwa mujibu wa sheria za Kiislam(sharia) na unawahimiza wazidishe nguvu zao katika mapambano ya kusimika upya matumizi ya sheria za Kiislam (sharia).

Mkutano umebaini ya kwamba taratibu za kuanzisha chama cha Kiislam cha waandishi na wenye vyombo vya habari Barani Afrika (African Muslim Media Practitioners Association) nchini Nigeria, zimeanza kutekelezwa. Mkutano umefurahishwa na hatua hiyo muhimu sana na unawahimiza waislam wote wanaofanya kazi katika mashirika ya habari kupitia chama hicho uungwaji mkono wa dhati kinachouhitaji ili kiweze kufanikisha malengo yake.

Kuunda/ kuanzisha chombo cha kudumu kitakachoitwa Islam in Africa Organization (IAO) yaani shirika la Uislam Barani Afrika, chini ya udhamini wa wawakilishi watakaochangiwa miongoni mwa nchi washiriki wa Mkutano huu: kutekeleza, miongoni mwa majukumu yao mengine , kazi ya dola na kuwezesha upatikanaji wa malengo na makusudio kama yalivyowekwa na (neno lisilosomeka) ndani ya tamko hili.

Mkutano kwa pamoja unatoa shukrani zake za kuelezea kufurahishwa kwake kwa Serikali ya watu wa Nigeria kwa umakini ulioonyeshwa juu ya mkutano huu, na kwa namna ya pekee mkutano unatoa shukrani zake kwa Rais, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Nigeria Jenerali Ibrahim Badamasi Badangida, kwa hotuba yake nzuri na ya kusisimua ya uzinduzi wa mkutano ambayo ilisomwa na Jenerali Sani Abacha ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nigeria; kwa baraza kuu la masuala ya kiislam, la Nigeria na kwa Baraza la Kiislam,London na shirika la umoja wa Kiislam,OIC kwa kuufadhili na kuuendeleza; kwa wanazuoni na watu wengine muhimu waliowasilisha mada na kuongeza vikao wakati wa Mkutano huu na kwa wale wote ambao ama wamesimika nguo au wamesaidia vinginevyo na kuufanya Mkutano huo kuwa wa mafanikio makubwa.

Wakisukumwa na umoja wa Allah, Muumba na Mola wa Ulimwengu mzima wakipata hamasa katika maneno ya kur'an "Hakika mwaka huu Umma (wa kiislam) ni wamoja" na wakidhamiria kuzingatia maagizo ya Allah ndani ya aya za kur'an, shikilieni kamba ya Allah bila kutetereka na msigawanyike katika makundi. WASHIRIKI wa mkutano wa shirika la Uislam Barani Afrika (IAO), mnamo tarehe ya kwanza, jumata Al wwwal, 1420 A.H (28/11/1989) wameazimia kuasisi(kuanzisha) ISLAM IN AFRICA ORGANIZATION – IAO yaani shirika la uislam barani afrika, nikiwa na malengo yafuatayo:-

1. Kuanzisha programu ngangari za maendeleo ya nguvu – kazi

2. Kutumika kama kisemeo kwa uzingatifu wa mambo yenye maslahi kwa waislam na kuokoa/kurejesha kazi za sanaa na kumbukumbu muhimu zinazoambatana navyo.

3. Kuteuwa wataalam na kuwapa kazi ya kuiandika upya Historia ya Uislam kwa Waislam wa Afrika pamoja na mtazamo halisi wa Kiislam na kuokoa/kurejesha kazi za sanaa na kumbukumbu muhimu zinazoambatana navyo.

4. Kuanzisha (neno lisilosomeka ) la Kiislam na vitu vya ufundi kusudiwa kufundisha wafanyakazi wenye jukumu la kueneza dini ya kiislam na kuwapatia ujuzi utakao wawezesha kuajiri na kuwa na tija;

5. Kuhakikisha muendelezo wa kazi iliyo bora kabisa, iliyoanzishwa kwenye mkutano huu;

6. Kushirikiana na mashirika mengine ya Kitaifa na kimataifa kufanikisha upatikanaji wa malengo yao yaliyo kusudiwa.

7. Kuimarisha umoja wa hali na mali miongoni mwa waislam kote ulimwenguni, hususani barani Afrika.

8. Kuimarisha amani, utengamano na maendeleo ya watu wote na kuongeza jitihada za kuondoa aina zote za ubaguzi.

9. Kuunga mkono, kuongeza nguvu na kuratibu kazi ya uenezi wa Dini ya Kiislam kote barani Afrika na kufundisha limu juu ya uislam kila mahali barani Afrika.

10. Kuhamasisha kazi za utafiti juu ya masuala ya kiislam na kusambaza matokeo ya kazi hizo;

11. Kuchukua jukumu, na kuhamasisha kufanyika kwa tafsiri za kazi za kiislam katika lugha mbalimbali za kienyeji barani Afrika, uchapishaji na usambazaji wake;

12. Kuunga mkono uanzishwaji na matumaini ya sheria za kiislam(sharia) kwa waislam wote.

13. Kuhamasisha ushirikishwaji ngangari wa vijana wa kiislam katika nyanja na maeneo yote ya shughuli na kuona wanawake wanapatiwa haki na nafasi ya kutekeleza majukumu yao katika jamii kwa mujibu wa sheria za kiislam(sharia)

14. Kuhakikisha kwamba ni waislam pekee ndio wanaoteuliwa kushika nafasi zote za kutawala na kisiasa katika mataifa wanachama.

15. Kukomesha dini zote zisizokuwa Uilslam katika mataifa yote wanachama Dini zote zisizokuwa Uislam katika mataifa yote wanachama: Dini hizo ni pamoja na Ukristo, Ahmadiyya na namna nyingine za ibada za kienyeji zisizokubalika kwa waislam katiak aina za matawi yote;

16. Kuhakikisha kuwa ni waislam pekee ndio wanaochaguliwa kushika nafasi zote za kiutawala na kisiasa katika mataifa wanachama.

17. Kuhakikisha kutawazwa kwa taifa la Nigeria mwanachama namba 24 Barani Afrika na namba 46 Duniani wa OIC kuwa shirikisho la kiislam la kisultani katika tarehe na muda mujarab/muafaka kuanzia tarehe 28 Machi 1990 na kumsimika Sultani wa Sokoto kuwa Sultani Mkuu mwenye mamlaka ya dola nchini Nigeria.

18. Kuhakikisha kuwa hatimaye sheria za Kiislam(sharia) zinachukuwa nafasi ya aina zote za sheria na mifumo ya mahakama za nchi za magharibi katika mataifa yote wanachama kabla ya mkutano ujao wa shirika la Uislam Barani Afrika(OIC)

19. Kuandaa mara kwa mara mikutano ya shirika la Uislam Barani Afrika (OIC) sanjari na semina, makongamano, warsha na mikusanyiko mingineyo ya aina hiyo:

Kwa hiyo kwa lengo la kufanikisha maamuzi haya, Kamatiya utekelezaji ikiwa na wajumbe kutoka nchi zifuatazo ( ambazo tayari ni wanachama wa IAO) na pia kutoka katika Baraza la Kiislam, London na Kutoka katika shirika la Umoja wa Kiislam OIC limeundwa ikiwa na mataifa wajumbe kama ifuatavyo:

1. Nigeria 2. Nigeria 3. Gambia 4. Maulitania 5. Senegal 6. Libya 7. Tanzania 8. Sudan 9. Tunisia.
Makao makuu ya kudumu ya shirika la Uislam Barani Afrika IAO, yatakuwa jijini Abuja-Nigeria.

20. Kamati ya utekelezaji imepewa jukumu maalumu la kubuni / kutengeneza (formulate) vingine bayana vilivyoanzisha shirika la IAO nchini Nigeria, ikiwemo mifuko (structures) na katiba, ndani ya miezi sita (6). Mkutano uliweka wazi kuwa kamati ya utekelezaji lazima itengeneze mipango ya kina ya kugeuza chama cha siasa cha Kitaifa kila nchi mwanachama kuwa chama cha kiislam cha Taifa na ya kwamba chama cha National Republican Convention NRC cha Nigeria sharti lifanywe litimize lengo hili kama chama pekee cha kiislam cha Taifa nchini Nigeria. Vyama hivi vya kisiasa vitakavyopewa barabara hizo zitakuwa ndiyo pekee vitakavyotoa watendaji wandamizi (wa dola na bunge) Chama cha NRC cha toa watendaji wandamizi (wa dola na bunge). Chama cha NRC cha Nigeria na vyama vingine vya aina yake katika nchi wanachama sharti vibadilishe majina yao ili kuakisi dhamiri yao kukumbatia uislam.

Mkutano pia ulikubali na kuamua kuwa kwa sasa (1989) IAO itafanya kazi kupitia huduma za Baraza la Kiislam, London na siyo kupitia OIC (ambayo imesababisha gumzo na utata mkubwa nchini Nigeria).

Mkutano huu wa pamoja hatimaye uliridhia Nigeria kuwa mwanachama kamili wa shirika la umoja wa kiislam,OIC na ukatoa shukrani zake kwa serikali na watu wa Nigeria kwa kutoa kwa ukarimu mkubwa msaada wa dola za Kimarekani bilioni ishirini na moja(US $ 21 Bilioni) kwa mfuko wa maendeleo ya waislam ( Islamic Development Fund ambayo ni mali ya OIC na kwa moyo mkunjufu kuiomba serikali kuonyesha ulimwengu mzima kwamba Nigeria kweli ni Taifa la Kiislam.


Mkataba huu umefasiriwa
Kutoka katika Lugha ya Kiingereza
Na wakili Mark S. Lebba na
Mwinjilisti Samson R. Bullegi
Wa huduma ya
Uinjilisti ya Injili kwa wote
 
Hivi hawa ndugu zetu mbona wabaguzi sana shuleni wakadai vijuba na suruali kwa watoto wa kike wakaruhusiwa ss wamekuja na mahakama ya kadhi wajenge wenyewe na wajitegemee.
 
Kama unakubali comment ndio na kama hutaki comment hapana lakini kama utaweza kutoa sababu ya kukubali au kukataa itakuwa pia vyema
 
mkuu kuna kitu nashindwa kuelewa hapa. hii sheria ilikuwepo hata kabla ya uhuru na baadaye nyerere alikuja kuifuta mwaka 1964. hivi aliwashirikisha waislam wakati anafuta?
au utawala wa kikoloni uliwajali zaidi waislam kuliko hata huu utawala wa watanzania wanzao?
mbona hizo mahakama zipo nchi mbalimbali na maisha yanaendelea? hizi mahakama zipo hata kenya, s.afrika na kwengineko. tatizo hasa ni nini hapa?

leta hiyo document hapa tuijadili au mnamezeshwa ujinga tu na nyie mnakuja kutapika hapa jamvini weka hapa tuone hiyo document ya kadhi kwa tanganyika
 
Omba Poll vinginevyo utakuwa unacheza mdundiko..!!!

Anyway, hakuna anayekataa Mahakama ya Kadhi, ila kinachogomba ni namna ya kuiendesha,kuigharimia na hatamaye Mambo ya Rufaa.

Kitu kitu kokubwa unachopaswa kuelewa ni kwamba, huwezi kupinga masuala ya Umani ya mtu mwingine ila Kama ni kupinga utapinga endapo itakuwa Inagongana na misimamo/Maslahi yaw dini yako wewe. Hapo tu ndipo penye utata sehemu zingine zote shwari tu..

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom