Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Mkuu samahani lakini unaweza kufanya citation kwa vipengele vya kwenye bill mfano hii bullet one unyoongelea asilimia ya malipo 38% unalipwa full then 62% monthly.. Samahani lakini wengine sio watu wa sheria bill nnayo ila kuitafuta sasa hizo vipengele
Me mwenyewe natafuta uhakika, naomba uweke hiyo bill hapa tuisome
 
Kwa sheria ya watumishi walioajiriwa baada ya July 2004 mpaka sasa kanuni ya ukokotozi wa mafao ilibadilika na kuwa 25% malipo ya mkupuo na 75% inabaki ktk mfuko kwa ajili ya malipo ya kila mwezi mpaka mwanachama atakapofariki. Hivyo kama mil 100 utapewa mil 25 then mil 75 inabak.

Ila kwa walioajiriwa 2004 July kurudi nyuma kule wao kanuni yao ilibaki vile vile ya 50% malipo ya mkupuo 50% malipo ya mwezi. Hivyo kwa utaratibu huu kama zile percent zitawekwa kwa mwanachama wrote bila kujali uliajiriwa lini basi itawaumiza sana wale was 2004 kurudi nyuma. Ila mwajiriwa was baada ya July 2004 itambeba kwasabab atakuwa na nyongeza ya 13% kwenye malipo ya mkupuo.
Asante kwa ufafanuzi kiongozi, kumbe tangu mwanzo panga lilikuwepo me nilijua walikuwa wanapewa 100%.
 
Ngoja wasomi waje watudadavulie maana mimi hata siwaelewi...yaani mtu kulipwa mpaka awe amechangia miaka 15?????kama hajatimiza iyo miaka 15 inakuaje sasa au ndo hela yake inakua ametoa sadaka tu?????
Ndugu hii miaka 15 kutokana na calculation za malipo ndo maana ukifuatilia vizuri nafasi nyingi za kazi utakuta muombaji asizidi miaka 45 sababu kubwa ni hiyo hiyo calculation za mafao. Miaka 45 +15 =60. Mtumishi kafanya kazi miaka 15 tu
 
SERIKALI INAONNEKANA IMESHINDWA KULIPA MADENI WANAYODAIWA NA MIFUKO HIVYO WANATAFUTA PAKUTOKEA, NGOJA TUONE MWISHO WA PICHA

NA KIVYOVYOTE KUNA WAFANYAKAZI WANAENDA KUPOTEZA KAZI, KWA SABABU KAMA MTU UMEMWAJIRI KWA AJILI YA KUTANGAZA USHINDANI WA MFUKO DHIDI YA MIFUKEO MINGNE, UKIUNGANISHA UKASEMA HUYU AHUDUMIE PRIVATE SECTOR NA MWINGNE AHUDUMIE SERIKALINI,INA MAANA HAPO HAKUNA TENA USHINDANI NA MAJUKUMU YA HUYO MTU YANAKUFA MFN: AFISA MASOKO

MWISHO, WAKATI WA USHINDANI HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII ZILIKUWA MBOVU, JE BILA USHINDANI HALI SI ITAKUWA MBAYA ZAIDI? KWANZA HAKUTAKUWA NA UBUNIFU KWA SABABU WANAJUA WEWE UTAKE USITAKE UTAJIUNGA TU, TOFAUTI NA SASA AMBAPO KUNA USHINDAN KTK KUPATA WANACHAMA WA MFUKO
 
Mkuu hebu nami nisaidie kidogo hapo. hiyo pesa inayobaki (75%) inalipwa kwa rate gani kila mwezi kama sio flat rate kwa wastaafu wote?
Inategemea mshahara wako thou kuna kima cha chini na cha juu......kuna wanaolipwa 100,000 na wengine wanachukua hadi 4m mwisho wa mwezi kama pension.
 
Nadhani kulitakiwa kuwe na kukua kwa pato la mwanachama/na wastaafu maana pesa yao haikai bure ndani ya mifuko ya jamii bali huzalisha. hivyo sio vema mtu akaweka 100000 akavuna 100000 baada ya miaka 20 ya uanachama. Na pia thamani ya pesa yetu hubadilika kila kukicha hivyo basi wanachama wanatakiwa wathaminishiwe pesa yao kipindi wanachangia na kipindi wanachukua iwe na nguvu sawa ya manunuzi.
 
Back
Top Bottom