Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Bunny Wailer

Member
Oct 29, 2017
11
11
Nashindwa hata kuandika baada ya kusoma yaliyomo kwenye muswada huo. Kifupi ni maumivu, enyi TUCTA, enyi wabunge, tusaidieni hiki kinachokwenda kufanyika kwa kweli ni kutiana umasikini.


=========

Serikali imewasilisha Mus-wada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma 2017 ambao ukipitish-wa, wanachama wake wanaotaka kujitoa watakabiliwa na masharti makali huku ukiruhusu mtoto mle-mavu kuendelea kulipwa kwa mai-sha yake yote.


Pamoja na mapendekezo mengi yaliyomo, muswada huo umeweka masharti kwa kwa watumishi wanaostahili kulipwa kabla hawa-jatimiza umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 55 kwa hiyari au 60 kwa lazima.Atakayetaka kujitoa, muswada unamtaka awe na “cheti cha dak-tari kwamba hawezi kuendele akutekeleza majukumu yake amba-cho mwajiri wake atakiridhia au ajira yake ikisitishwa kwa maslahi ya umma au muda wake wa uteuzi utakapokamilika.”Muswada unaongeza masharti kwamba, mwanachama yeyote atastahili mafao endapo atakuwa amechangia walau miaka 15 au jum-la ya miezi 180.Mfuko unawatambua watoto na mwenza wa kila mwanachama. Kwa uzito uliopo, unapendekeza kum-lipa mtoto mlemavu wa mwana-chama atakayepoteza maisha akiwa kazini kwa maisha yake yote yali-yobaki wakati ambao ni wazima, mpaka watakapotimiza miaka 21.Wakati mtoto ikipendekezwa apewe mafao hayo, mjane naye, kul-ingana na umri na watoto alioachi-wa, amezingatiwa. Kwa aliyeachwa na watoto wenye chini ya miaka 15 naye akiwa na zaidi au chini ya miaka 45, muswada unapendekeza alipwe mafao kwa maisha yake yote au mpaka atakapoolewa tena.Endapo mwanachama hakuacha mtoto wala mke, inapendekezwa: “Wazazi wake walipewe haki zote za mtoto wao.”

Kutekeleza mabadiliko hayo, muswada unapendekeza kuvunjwa kwa mifuko ya PPF, GEPF, LAPF na PSPF kasha kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) utakaorithi mali na madeni yote ya mifuko hiyo iliyopo sasa.

Itakapopitishwa, kutakuwa na kipindi cha mpito cha miezi sita kukamilisha hatua zote za kisheria zinazohitajika kabla utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo mpya utakaokuwa na thamani ya Sh5 trilioni haujaanza.

Mabadiliko hayo yataiacha mifuko minne kutoka saba ya sasa ukiwamo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wakati PSSSF ukiwahudumia watumishi wa umma, NSSF utakuwa kwa ajili ya sekta binafsi.

Kwenye makabidhiano yatakayofanywa, michango na wanachama wa NSSF ambao ni watumishi wa umma watahamishiwa PSSF wakati wale wa sekta binafsi kutoka huko watahamishiwa NSSF. Wafanyakazi wenye sifa wa mifuko itakayovunjwa wataajiriwa PSSSF itakayochukua madeni na mali za mifuko hiyo pia.

Utafiti wa ajira na kipato wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) mwaka 2015 unaonyesha kuna watumishi milioni 2.3 nchini ambao kati yao, milioni 1.6 wanatoka sekta binafsi na 700,000 ni wa umma.

Mfuko huo utatoa mafao manane ambayo ni la kustaafu, warithi, kujitoa, uzazi na kutokuwa na ajira. Mengine ni fao la ugonjwa, kifo na mzishi.

Sharti limewekwa kwamba: “Haitaruhusiwa kwa mwanachama kupewa mafao mawili kwa wakati mmoja.”

Muswada unapendekeza wanachama kuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa nyumba kwa dhaman ya michango yao waliyonayo kwenye mfuko huu mpya. Vilevile, wanaochangia kwa hiyari kwenye mifuko minne itakayofutwa watahamishiwa PSSSF.

Muswada unashauri, mafao ya mwanachama yanaweza yakatumika kulipa deni la serikali, mkopo wa nyumba au malezi na matunzo ya mtoto au mke aliyetelekezwa baada ya kujiridhisha kwa mamlaka husika.

Kukabiliana na ucheleweshaji wa malipo ya mafao kwa wastaafu, muswada unapendekeza itakapodhihirika kuwa ucheleweshaji huo haukuchangiwa na mtumishi husika basi mfuko umlipe mafao yake pamoja na riba ya asilimia tano ya thamani ya mafao yake kwa mwaka.

Suala la makosa yanayoweza kuhumiwa kifungo gerezani, muswada unapendekeza wategemezi wake; mke na watoto walipwe stahiki za mtumishi husika ili waweze kujikimu kwa muda ambao mwanachama huyo atakuwa anatumikia kifungo chake.

Kwa mwanachama atakayehukumiwa kifungo lakini hana wategemezi, pindi hukumu yake ikiisha, mfuko unawajibika kumlipa mafao yake yote anayostahili kwa muda aliochangia.

Ikitokea mfanyakazi wa umma amebadili mwajiri na kwenda sekta binafsi, uanachama wake utahamishiwa NSSF lakini michango yake itaendelea kubaki PSSSF na muda wa kustaafu utakapofika au sababu nyingine ya kulipwa mafao yake, ukokotozi wa pamoja utafanywa kati ya mifuko hiyo miwili.

Jambo jingine muhimu kwenye muswada huo ni madai yaliyotelekezwa. Inapendekezwa, mwanachama ambaye warithi wake hawatajitokeza kwa miaka mitatu mfululizo kufuatilia michango yake kutokana na kifo au sababunyingine yoyote, kiasi kilichopo kitahamishiwa kwenye akaunti maalumu ya serikali.

Na hali ikiendelea kuwa hivyo kwa miaka 10, akaunti ya mwanachama itafutwa na fedha zake kuhamishiwa serikalini.

Muswada unatambua watumishi wa mifuko inayotarajia kuunganishwa, mali za taasisi hizo, madeni pamoja na miradi mbalimbali. Muswada unapendekeza kwamba, mikataba yote iliyopo ambayo inaendele akutekelezwa kuhamishiwa PSSSF.

Uhamisho huo pia utahusisha mali na madeni yaliyopo bila kusahau miradi. Haya yote yanatakiw ayafanywe ndani ya miezi sita ambayo ni kipindi cha mpito kwa ajili ya makabidhiano.

Ndani ya miezi sita baada ya kukamilika kwa mwaka wa fedha, bodi ya wakurugenzi ya PSSSF italazimika kuandaa hesabu za fedha na ripoti yake kuiwasilisha kwa waziri mwenye dhamana ambaye atawajibika kupeleka nakala na kuisoma bungeni.

Bodi itatakiwa kutoa ripoti hizi kila mwaka ambazo zitajumuisha taarifa za mali na madeni, operesheni za mfuko, matumizi ya fedha za mfuko na taarifa nyingine yoyote ambayo waziri au mamlaka za juu zaidi zitahitaji.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA), Irene Isaka anasema mapendekezo haya yamefanywa baada ya tathmini ya kina iliyozingatia mambo mengi yaliyoshauriwa na vyama vya wafanyakazi.

Kukamilisha mchakato huo, Isaka anasema tahadhari inachukuliwa kuhakikisha watumishi waliopo hawapotezi kazi zao. Kwa waliopo ngazi za ukurugenzi, alisema wanaweza kupangiwa majukumu mengine endapo itaonekana nafasi zao zimejaa kwenye mfumo huu mpya.

“Hii sekta bado inahitaji wafanyakazi wengi kukidhi mahitaji yaliyopo na yanayoongezeka kila siku. Hatma ya wafanyakazi waliopo kwenye mifuko inayounganishwa itafahamika baada ya muda mfupi,” anasema.

Kuhakikisha mambo yanaenda sawa, anasema Wizara ya Utumishi inashughulikia suala hilo hasa kwa kutambua kwamba baadhi ya mifuko ilikuwa na wafanyakazi wengi kuliko mahitaji ilhali mingine ilikuwa nao wachache hivyo, kama watakuwapo watakaopoteza nafasi zao, hawatokuwa wengi.

Licha ya mustakabali wa watumishi waliopo, anasema wizara hiyo pia inaandaa mfumo sahihi utakaowahudumia waajiriwa waliopo sekta binafsi pamoja na wale wa sekta ya umma.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya HakiPension, Christian Gaya anasema muungano huo utakuwa mzuri endapo wananchi wengi zaidi watakuwa na nafasi ya kujiunga na huduma za hifadhi ya jamii na mmafao kutolewa kwa wakati. “Kwa sasa mafao ya wafanyakazi yanacheleweshwa ilhali kuna mifuko mingi yenye ushindani. Sijui itakuwa kutakapokuwa na mifuko miwili pekee,” anatia shaka Gaya.

Chanzo: Mwananchi
 
Ngoja wasomi waje watudadavulie maana mimi hata siwaelewi...yaani mtu kulipwa mpaka awe amechangia miaka 15?????kama hajatimiza iyo miaka 15 inakuaje sasa au ndo hela yake inakua ametoa sadaka tu?????
 
Kwa kuusoma muswada huu, utagundua kuwa kuna harufu ya dhuluma kubwa mbele yetu. TUCTA, kumbukeni kila mwezi mnachukua asilimia mbili toka kwenye mishahara yetu. Waheshimiwa wabunge, chondechonde--msiupitishe muswada huu kwa sababu hauna sehemu unasema kuhusu watu waliopoteza ajira kwa kufukuzwa ama wanaopoteza ajira kwa redundancy. TUCTA msipopigania hili maana yake mmesaliti wafanyakazi, na hakutakuwa na maana ya wafanyakazi kuendelea kuwa wanachama wakati mnashindwa kuwatetea. Walisema kutakuwa na FAO LA KUKOSA AJIRA, ila haioneshi kama lipo. Enyi mliotunga haya, hivi mna roho gani nyie, mna dini kweli?
 
Kiukweli hivyo Vyama vya Wafanyakazi hata sijui Msaada wao kwa hao Wafanyakazi ni upi
Haswa haswa kwa hii awamu, hivyo vyama vya wafanyakazi havina sauti tena. Wafanyakazi wamebakia kuwa watoto yatima, pamekuwa kimya utafikiri hakuna matatizo!!!!
 
Ingependeza NSSF inayohudumia sekta binafsi waruhusiwe kutoa fao la kujitoa,kwa sababu kazi nyingi za sekta binafsi sio za kudumu.Mfano mtu amefanya kazi mwaka mmoja kwa asian ikaisha,huyo mfanyakazi ambao wengi ni vibarua atasubiri mpaka 55 years ndo apewe fao lake,pili nafikiri wangempa chake badala ya Fao lakutokuwa na ajira.Kama ni 1,000,000/=akanunue cherehani aanziashe kiwanda badala ya kupokea kipenaheni kidogo dogo chakutokuwa na ajira.
 
Kumekucha.
Hiyo issue ya gender hapo vipi? Akifa mama je? Au akifungwa mwanamke then mwanamme akaachwa na watoto inakuwaje?
Mambo ya kutunza mke ni soooo old school labda watoto tu basi!
 
Kuna tatizo kubwa LA gender!? Inaonekana yanaelezewa matunzo kwa watoto pindi baba akifa! Ila watambue kifo hakibagui wasiwe biased
Yaani ukiangalia vizuri mfanyakazi muhusika hanufaiki na mafao yake, Maelezo yote utakuta mfanyakazi akifa mafao watapata watoto au mke au mlemavu ndiyo atafaidi, ishiii hivi vigezo vya ulemavu mbona wanavipenda sana, ukienda bodi ya Mikopo hivyo hivyo, aliyefiwa na wazazi au mlemavu ndiyo atapewa mkopo
 
Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.

Nimeitoa sehemu, je ni kweli?
 
Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.

Nimeitoa sehemu, je ni kweli?

Sina hakika. Ila kabla ya kusubiri wabunge, TUCTA watuambie kwa nini wameshiriki haya maana naamini walihusishwa kama wadau na wawakilishi wa wafanyakazi. Asilimia mbili ya kutoka mishahara yetu ni kubwa, kwa hiyo watueleze walifikiria nini kushiriki haya.
 
Sina hakika. Ila kabla ya kusubiri wabunge, TUCTA watuambie kwa nini wameshiriki haya maana naamini walihusishwa kama wadau na wawakilishi wa wafanyakazi. Asilimia mbili ya kutoka mishahara yetu ni kubwa, kwa hiyo watueleze walifikiria nini kushiriki haya.
TUCTA hawawezi kutuambia hilo, wale wanakula pesa tu hawana shida, nadhani mwenye huo Muswada sio mbaya akautupia hapa.
 
Kwa uzoefu wangu wa kingumbaro najua msaada ukishaandikwa una Nia na malengo yake, wah Wabunge watapewa Semina nyingi kuhusu hili na kama kawaida watapitisha. Watumishi Wataumia. Ningeshauri suala hili Kuachwa tu km ilivyo sasa.
Walemavu wametajwa sijaelewa why, kwa vile Ni wachache??
 
Back
Top Bottom