Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Msaada kuhusu kipengele kinachosema" Mafao ya mtumishi yatatumika kumkopeshea nyumba".
 
Ingependeza NSSF inayohudumia sekta binafsi waruhusiwe kutoa fao la kujitoa,kwa sababu kazi nyingi za sekta binafsi sio za kudumu.Mfano mtu amefanya kazi mwaka mmoja kwa asian ikaisha,huyo mfanyakazi ambao wengi ni vibarua atasubiri mpaka 55 years ndo apewe fao lake,pili nafikiri wangempa chake badala ya Fao lakutokuwa na ajira.Kama ni 1,000,000/=akanunue cherehani aanziashe kiwanda badala ya kupokea kipenaheni kidogo dogo chakutokuwa na ajira.
Mnaposema mpaka mtu afikishe miaka15 hivi mnafikiri ni rahisi kihivo kwa serikali ni sawa.Kwa wenzangu wanaofanya kazi migodini,bandarini,viwanda vya madawa ya kuulia wadudu,viwanda vya chuma n.k ajira zao sio za kudumu lakini hata afya zao ziko mashakani siku zote za kazi.Kwao pingili za uti wa mgongo kuachia na kutenguka ni mambo ya kawaida kabisa.Kijana ana miaka20 amesotea kazi mgodini anaipata baada ya miaka miwili akiwa na miaka22 baada ya miaka mitatu tu yeye mwenyewe anajiona kiafya hawezi kuendelea tena inatosha kutokana na afya yake anavyojisikia kwa hiyo huyu sasa ana miaka 25 hivyo asubiri miaka mingine 35 ndio apate haki yake?.Mnaopitisha miswada jaribuni kuangalia mazingira ya kazi sehemu mbali mbali.Napendekeza wabunge wote wapelekwe migodini,viwandani,viwanda vya kuyeyusha vyuma wafanye mahojiano na wafanyakazi wapate mapendekezo kisha waiingizwe mpaka huko chini ardhini level ya mwisho kabisa kusiko na hewa ya kutosha ambapo vijana ndio wanapofanya kazi zao.Kisha wapande sasa juu wakae mjengoni waanze kujadili.Ni rahisi sana kupanga kitu ukiwa mezani kuliko kukifanya kiutendaji zaidi.Pendekezo langu la mwisho serikali isiruhusiwe kukopa kwenywe mifuko ya jamii maana zile sio benki.Mifuko ya jamii sio bank bali ni hela za watu zilizoweka kwa faida yao baadae.Mikopo inatolewa na mabenki sio mifuko ya jamii.Hii itasaidia kutokuingiza siasa kwenye hela za watu
 
Huu ubanaji umezidi, watumishi tutaumia sana.
 
Hawajaainisha namna ya kukokotoa mafao kama inabaki kama ilivyokuwa au watabadilisha! Wanachama wa zamani wa pspf walikuwa na formula yao yenye mafao bora zaidi kuliko wanachama wapya! Nini hatima yao baada ya mifuko kuunganishwa? Sheria imekaa kimya! Naona harufu ya maumivu kwao!
Lakini pia ni vizuri sheria itamke kama kanuni ya ukokotoaji wa mafao: 1. Utabaki kama ulivyokuwa 2. Utaongeza mafao 3. Utapunguza mafao
Yasipowekwa kwenye faida itakuja kuleta mgogoro!
 
Uwepo ushindani kati ya mifuko hii miwili! Mfanyakazi wa umma ambaye ni mwanachama wa NSSF asilazimishwe kuhama na kujiunga na na huo mfuko mpya wa PSSSF. Bila kuruhusu ushindani watumishi wa umma watanyonywa sana!
Mpaka hapo na kwa sheria iliyopendekezwa hakuna mtumishi wa umma ambaye angetaka kujiunga huko kwa hiari yake!
 
Nashindwa hata kuandika baada ya kusoma yaliyomo kwenye muswada huo. Kifupi ni maumivu, enyi TUCTA, enyi wabunge, tusaidieni hiki kinachokwenda kufanyika kwa kweli ni kutiana umasikini.

=========

Serikali imewasilisha Mus-wada wa Sheria ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma 2017 ambao ukipitish-wa, wanachama wake wanaotaka kujitoa watakabiliwa na masharti makali huku ukiruhusu mtoto mle-mavu kuendelea kulipwa kwa mai-sha yake yote.

Pamoja na mapendekezo mengi yaliyomo, muswada huo umeweka masharti kwa kwa watumishi wanaostahili kulipwa kabla hawa-jatimiza umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 55 kwa hiyari au 60 kwa lazima.Atakayetaka kujitoa, muswada unamtaka awe na “cheti cha dak-tari kwamba hawezi kuendele akutekeleza majukumu yake amba-cho mwajiri wake atakiridhia au ajira yake ikisitishwa kwa maslahi ya umma au muda wake wa uteuzi utakapokamilika.”Muswada unaongeza masharti kwamba, mwanachama yeyote atastahili mafao endapo atakuwa amechangia walau miaka 15 au jum-la ya miezi 180.Mfuko unawatambua watoto na mwenza wa kila mwanachama. Kwa uzito uliopo, unapendekeza kum-lipa mtoto mlemavu wa mwana-chama atakayepoteza maisha akiwa kazini kwa maisha yake yote yali-yobaki wakati ambao ni wazima, mpaka watakapotimiza miaka 21.Wakati mtoto ikipendekezwa apewe mafao hayo, mjane naye, kul-ingana na umri na watoto alioachi-wa, amezingatiwa. Kwa aliyeachwa na watoto wenye chini ya miaka 15 naye akiwa na zaidi au chini ya miaka 45, muswada unapendekeza alipwe mafao kwa maisha yake yote au mpaka atakapoolewa tena.Endapo mwanachama hakuacha mtoto wala mke, inapendekezwa: “Wazazi wake walipewe haki zote za mtoto wao.”

Kutekeleza mabadiliko hayo, muswada unapendekeza kuvunjwa kwa mifuko ya PPF, GEPF, LAPF na PSPF kasha kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) utakaorithi mali na madeni yote ya mifuko hiyo iliyopo sasa.

Itakapopitishwa, kutakuwa na kipindi cha mpito cha miezi sita kukamilisha hatua zote za kisheria zinazohitajika kabla utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo mpya utakaokuwa na thamani ya Sh5 trilioni haujaanza.

Mabadiliko hayo yataiacha mifuko minne kutoka saba ya sasa ukiwamo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wakati PSSSF ukiwahudumia watumishi wa umma, NSSF utakuwa kwa ajili ya sekta binafsi.

Kwenye makabidhiano yatakayofanywa, michango na wanachama wa NSSF ambao ni watumishi wa umma watahamishiwa PSSF wakati wale wa sekta binafsi kutoka huko watahamishiwa NSSF. Wafanyakazi wenye sifa wa mifuko itakayovunjwa wataajiriwa PSSSF itakayochukua madeni na mali za mifuko hiyo pia.

Utafiti wa ajira na kipato wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) mwaka 2015 unaonyesha kuna watumishi milioni 2.3 nchini ambao kati yao, milioni 1.6 wanatoka sekta binafsi na 700,000 ni wa umma.

Mfuko huo utatoa mafao manane ambayo ni la kustaafu, warithi, kujitoa, uzazi na kutokuwa na ajira. Mengine ni fao la ugonjwa, kifo na mzishi.

Sharti limewekwa kwamba: “Haitaruhusiwa kwa mwanachama kupewa mafao mawili kwa wakati mmoja.”

Muswada unapendekeza wanachama kuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa nyumba kwa dhaman ya michango yao waliyonayo kwenye mfuko huu mpya. Vilevile, wanaochangia kwa hiyari kwenye mifuko minne itakayofutwa watahamishiwa PSSSF.

Muswada unashauri, mafao ya mwanachama yanaweza yakatumika kulipa deni la serikali, mkopo wa nyumba au malezi na matunzo ya mtoto au mke aliyetelekezwa baada ya kujiridhisha kwa mamlaka husika.

Kukabiliana na ucheleweshaji wa malipo ya mafao kwa wastaafu, muswada unapendekeza itakapodhihirika kuwa ucheleweshaji huo haukuchangiwa na mtumishi husika basi mfuko umlipe mafao yake pamoja na riba ya asilimia tano ya thamani ya mafao yake kwa mwaka.

Suala la makosa yanayoweza kuhumiwa kifungo gerezani, muswada unapendekeza wategemezi wake; mke na watoto walipwe stahiki za mtumishi husika ili waweze kujikimu kwa muda ambao mwanachama huyo atakuwa anatumikia kifungo chake.

Kwa mwanachama atakayehukumiwa kifungo lakini hana wategemezi, pindi hukumu yake ikiisha, mfuko unawajibika kumlipa mafao yake yote anayostahili kwa muda aliochangia.

Ikitokea mfanyakazi wa umma amebadili mwajiri na kwenda sekta binafsi, uanachama wake utahamishiwa NSSF lakini michango yake itaendelea kubaki PSSSF na muda wa kustaafu utakapofika au sababu nyingine ya kulipwa mafao yake, ukokotozi wa pamoja utafanywa kati ya mifuko hiyo miwili.

Jambo jingine muhimu kwenye muswada huo ni madai yaliyotelekezwa. Inapendekezwa, mwanachama ambaye warithi wake hawatajitokeza kwa miaka mitatu mfululizo kufuatilia michango yake kutokana na kifo au sababunyingine yoyote, kiasi kilichopo kitahamishiwa kwenye akaunti maalumu ya serikali.

Na hali ikiendelea kuwa hivyo kwa miaka 10, akaunti ya mwanachama itafutwa na fedha zake kuhamishiwa serikalini.

Muswada unatambua watumishi wa mifuko inayotarajia kuunganishwa, mali za taasisi hizo, madeni pamoja na miradi mbalimbali. Muswada unapendekeza kwamba, mikataba yote iliyopo ambayo inaendele akutekelezwa kuhamishiwa PSSSF.

Uhamisho huo pia utahusisha mali na madeni yaliyopo bila kusahau miradi. Haya yote yanatakiw ayafanywe ndani ya miezi sita ambayo ni kipindi cha mpito kwa ajili ya makabidhiano.

Ndani ya miezi sita baada ya kukamilika kwa mwaka wa fedha, bodi ya wakurugenzi ya PSSSF italazimika kuandaa hesabu za fedha na ripoti yake kuiwasilisha kwa waziri mwenye dhamana ambaye atawajibika kupeleka nakala na kuisoma bungeni.

Bodi itatakiwa kutoa ripoti hizi kila mwaka ambazo zitajumuisha taarifa za mali na madeni, operesheni za mfuko, matumizi ya fedha za mfuko na taarifa nyingine yoyote ambayo waziri au mamlaka za juu zaidi zitahitaji.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Jamii (SSRA), Irene Isaka anasema mapendekezo haya yamefanywa baada ya tathmini ya kina iliyozingatia mambo mengi yaliyoshauriwa na vyama vya wafanyakazi.

Kukamilisha mchakato huo, Isaka anasema tahadhari inachukuliwa kuhakikisha watumishi waliopo hawapotezi kazi zao. Kwa waliopo ngazi za ukurugenzi, alisema wanaweza kupangiwa majukumu mengine endapo itaonekana nafasi zao zimejaa kwenye mfumo huu mpya.

“Hii sekta bado inahitaji wafanyakazi wengi kukidhi mahitaji yaliyopo na yanayoongezeka kila siku. Hatma ya wafanyakazi waliopo kwenye mifuko inayounganishwa itafahamika baada ya muda mfupi,” anasema.

Kuhakikisha mambo yanaenda sawa, anasema Wizara ya Utumishi inashughulikia suala hilo hasa kwa kutambua kwamba baadhi ya mifuko ilikuwa na wafanyakazi wengi kuliko mahitaji ilhali mingine ilikuwa nao wachache hivyo, kama watakuwapo watakaopoteza nafasi zao, hawatokuwa wengi.

Licha ya mustakabali wa watumishi waliopo, anasema wizara hiyo pia inaandaa mfumo sahihi utakaowahudumia waajiriwa waliopo sekta binafsi pamoja na wale wa sekta ya umma.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya HakiPension, Christian Gaya anasema muungano huo utakuwa mzuri endapo wananchi wengi zaidi watakuwa na nafasi ya kujiunga na huduma za hifadhi ya jamii na mmafao kutolewa kwa wakati. “Kwa sasa mafao ya wafanyakazi yanacheleweshwa ilhali kuna mifuko mingi yenye ushindani. Sijui itakuwa kutakapokuwa na mifuko miwili pekee,” anatia shaka Gaya.

Chanzo: Mwananchi
Baada ya kusoma hiki kipande cha gazeti ya mwananchi nimegundua yafuatayo:

Mfuko huo utatoa mafao manane ambayo ni la kustaafu, warithi, kujitoa, uzazi na kutokuwa na ajira. Mengine ni fao la ugonjwa, kifo na mzishi.

Muswada unapendekeza wanachama kuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa nyumba kwa dhaman ya michango yao waliyonayo kwenye mfuko huu mpya.

Muswada unashauri, mafao ya mwanachama yanaweza yakatumika kulipa deni la serikali, mkopo wa nyumba.

Maswali yangu:
1. Fao la kufukuzwa kazi mbona silioni?
2. Riba ukichukua mkopo wa nyumba ni kiasi gani isije ikwa ni "wizi mtupu"
3. Kama mtumishi ana deni la Higher Education Loan Board, hilo nakubaliana nalo maana kuanza kazi na mshahara kiduchu alafu uanze kukatwa 15% utabakiwa na nini? Bora wakati kwenye mfuko wa ifadhi ya jamii
4. Kama kiinua mgongo ni 32%, basi wafanyakazi wengi kuweni macho kabla ya kufikisha miezi 180 ambayo ni miaka 15 nenda wakupigie mahesabu hiyo 32% ni kiasi gani? Linganisha na kiasi kilichopo ukiamua kuacha kazi kwasababu naona kuna fao la kujitoa. Ukiona ukijitoa unalipwa hela nyingi kuliko kusubili kustaafu ukalipwa 32%, then wengi bora uachekazi upewe chako kuliko kusubiri umezeeka alafu wanakupora 62% ya jasho lako
 
Mnaposema mpaka mtu afikishe miaka15 hivi mnafikiri ni rahisi kihivo kwa serikali ni sawa.Kwa wenzangu wanaofanya kazi migodini,bandarini,viwanda vya madawa ya kuulia wadudu,viwanda vya chuma n.k ajira zao sio za kudumu lakini hata afya zao ziko mashakani siku zote za kazi.Kwao pingili za uti wa mgongo kuachia na kutenguka ni mambo ya kawaida kabisa.Kijana ana miaka20 amesotea kazi mgodini anaipata baada ya miaka miwili akiwa na miaka22 baada ya miaka mitatu tu yeye mwenyewe anajiona kiafya hawezi kuendelea tena inatosha kutokana na afya yake anavyojisikia kwa hiyo huyu sasa ana miaka 25 hivyo asubiri miaka mingine 35 ndio apate haki yake?.Mnaopitisha miswada jaribuni kuangalia mazingira ya kazi sehemu mbali mbali.Napendekeza wabunge wote wapelekwe migodini,viwandani,viwanda vya kuyeyusha vyuma wafanye mahojiano na wafanyakazi wapate mapendekezo kisha waiingizwe mpaka huko chini ardhini level ya mwisho kabisa kusiko na hewa ya kutosha ambapo vijana ndio wanapofanya kazi zao.Kisha wapande sasa juu wakae mjengoni waanze kujadili.Ni rahisi sana kupanga kitu ukiwa mezani kuliko kukifanya kiutendaji zaidi.Pendekezo langu la mwisho serikali isiruhusiwe kukopa kwenywe mifuko ya jamii maana zile sio benki.Mifuko ya jamii sio bank bali ni hela za watu zilizoweka kwa faida yao baadae.Mikopo inatolewa na mabenki sio mifuko ya jamii.Najua serikali yetu kuendeleza mambo yake inaweza kukopa sawa ila isikope moja kwa moja kupitia mifuko ya jamii bali bank inayotaka kuikopa serikali ikope kwanza kwenye hii mifuko kwa sababu kwa kawaida mabenki yana bima kubwa kubwa ila serikali hatuwezi sema ina bima.Basi mifuko ya jamii itakuwa inazidai hizo bank moja kwa moja.Tuwekane sawa tena hapa narudia mifuko ya jamii sio taasisi za kibenki bali ni mifuko ya kuhifadhi hela za watu kwa ajili ya maisha yao ya baade.Hii itasaidia kutokuingiza siasa kwenye hela za watu.Mimi binafsi napinga dhana watu wanaposema serikali imeamua kufanya hivi ajili ya deni la taifa.Hakuna nchi isiyodaiwa na toka enzi ya baba wa taifa tulikuwa na madeni kudaiwa ni kitu cha kawaida
 
Mimi nakuunga mkono 100%. Serikali kwa kitendo chake kukopa hela kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kulipa imepelekea mifuko kuwa na madeni kushindwa kulipa viinua mgongo vya wasitaafu na wanachama wengine. Kwanini serikali ikope hela bila kurudisha hela za wavuja jasho walizozitaabikia? kila kukicha serikali inakuja na miswada yenye lengo la kuwapora wafanyakazi haki zake. Mara harmonization scheme, mara hakuna fao la kujitoa, mara mfuko huwe mmoja kwa watumishi wa serikali na wa sector binafsi??? Ukiangalia kiini cha haya yote ni kusudi kuwapora haki wafanyakazi. Ebu jiulize umetumikia serikali unataka kustaafu alafu eti unapewa 32%??? Inaingia akilini kweli? yaani kusudi serikali ikupore 68% iliyobaki ikijua kwa umri wa kustaafu 68% huwezi kuitumia sana sana utakufa tu ndani ya miaka 5. Huu ni uonevu mkubwa. Naashangaa wanasheria wetu wako wapi? nashangaa asasi za kiraia za kutetea haki za binadamu mko wapi? nashangaa vyama vya wafanyakazi ambavyo hukata 2% ya mishahara ya wafanyakazi kama kweli wanatetea wafanyakazi au nao ni wanyonyaji? Kwahili naomba tuamke? Watoto wetu watakuja kuwa ombaomba wakati tumelitumikia taifa miaka 55 hadi 60!!!
 
Hawajaainisha namna ya kukokotoa mafao kama inabaki kama ilivyokuwa au watabadilisha! Wanachama wa zamani wa pspf walikuwa na formula yao yenye mafao bora zaidi kuliko wanachama wapya! Nini hatima yao baada ya mifuko kuunganishwa? Sheria imekaa kimya! Naona harufu ya maumivu kwao!
Lakini pia ni vizuri sheria itamke kama kanuni ya ukokotoaji wa mafao: 1. Utabaki kama ulivyokuwa 2. Utaongeza mafao 3. Utapunguza mafao
Yasipowekwa kwenye faida itakuja kuleta mgogoro!
Hakuna cha formula ya zamani wala formula mpya. Wamesema watakupa kiinua mgongo 32% tu na 68% iliyobaki utapewa kila mwezi kama mshahara wa watumishi unavyochelewa kwa mizengwe na kukupa stress ili ufe mapema. Hiyo hela siyo yao! kwanini waiwekee masheria kibao? Na wakiona ufi kwao inakuwa hasara. Lakini wajue sheria ni msumeno. Acha waendelee kuweka sheria kandamizi wasifikiri nao hawatafika umri wa kustaafu. Wacha waendelee kuweka sheria kandamizi bila kujua nao wana ndugu, watoto, waume, wake, ambao ni wafanyakazi ambao itawaumiza pia. Mungu linusuru hili taifa hatujui tunakoelekea!!
 
Mnaposema mpaka mtu afikishe miaka15 hivi mnafikiri ni rahisi kihivo kwa serikali ni sawa.Kwa wenzangu wanaofanya kazi migodini,bandarini,viwanda vya madawa ya kuulia wadudu,viwanda vya chuma n.k ajira zao sio za kudumu lakini hata afya zao ziko mashakani siku zote za kazi.Kwao pingili za uti wa mgongo kuachia na kutenguka ni mambo ya kawaida kabisa.Kijana ana miaka20 amesotea kazi mgodini anaipata baada ya miaka miwili akiwa na miaka22 baada ya miaka mitatu tu yeye mwenyewe anajiona kiafya hawezi kuendelea tena inatosha kutokana na afya yake anavyojisikia kwa hiyo huyu sasa ana miaka 25 hivyo asubiri miaka mingine 35 ndio apate haki yake?.Mnaopitisha miswada jaribuni kuangalia mazingira ya kazi sehemu mbali mbali.Napendekeza wabunge wote wapelekwe migodini,viwandani,viwanda vya kuyeyusha vyuma wafanye mahojiano na wafanyakazi wapate mapendekezo kisha waiingizwe mpaka huko chini ardhini level ya mwisho kabisa kusiko na hewa ya kutosha ambapo vijana ndio wanapofanya kazi zao.Kisha wapande sasa juu wakae mjengoni waanze kujadili.Ni rahisi sana kupanga kitu ukiwa mezani kuliko kukifanya kiutendaji zaidi.Pendekezo langu la mwisho serikali isiruhusiwe kukopa kwenywe mifuko ya jamii maana zile sio benki.Mifuko ya jamii sio bank bali ni hela za watu zilizoweka kwa faida yao baadae.Mikopo inatolewa na mabenki sio mifuko ya jamii.Hii itasaidia kutokuingiza siasa kwenye hela za watu
Umenena vyema,ikiwezekana wabunge ambao awajafikisha miaka 55 wakistaafu wasirusiwe kupata mafao yao mpaka wafikishe miaka 55 au wapewe fao la kutokuwa na ajira.
 
Hakuna cha formula ya zamani wala formula mpya. Wamesema watakupa kiinua mgongo 32% tu na 68% iliyobaki utapewa kila mwezi kama mshahara wa watumishi unavyochelewa kwa mizengwe na kukupa stress ili ufe mapema. Hiyo hela siyo yao! kwanini waiwekee masheria kibao? Na wakiona ufi kwao inakuwa hasara. Lakini wajue sheria ni msumeno. Acha waendelee kuweka sheria kandamizi wasifikiri nao hawatafika umri wa kustaafu. Wacha waendelee kuweka sheria kandamizi bila kujua nao wana ndugu, watoto, waume, wake, ambao ni wafanyakazi ambao itawaumiza pia. Mungu linusuru hili taifa hatujui tunakoelekea!!
Bado nafatilia hiyo section ya 32% sijaiona, unaweza kunitajia ni section gani mkuu?
 
Ngoja wasomi waje watudadavulie maana mimi hata siwaelewi...yaani mtu kulipwa mpaka awe amechangia miaka 15?????kama hajatimiza iyo miaka 15 inakuaje sasa au ndo hela yake inakua ametoa sadaka tu?????
Hii hata kwa sheria ya sasa hivi IPO hivyo yani katika 100% ya michango yako katika ukokotozi yule mtumishi anayeachishwa au kuacha kazi baada yaa kuchangia kwa miaka 15 atalipwa malipo ya mkupuo ambayo ni 25% ya michango yake. Halafu 75% itakokotolewa na kulipwa monthly kwa kipindi chote cha maisha yake hii itakoma pale mwanachama atakapofariki.

Ila kwa mtumishi atakayepoteza kazi kabla ya kuchangia ktk mfuko kwa miaka 15 huyu atalipwa 100% ya michango yake yote yani malipo ya mkupuo tu. Hataacha ile 75% kwa ajili ya malipo endelevu. Kwahyo huyu anamalizana na mfuko moja kwa moja anapewa chake chote anasepa.
 
Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.

Nimeitoa sehemu, je ni kweli?

Kwa sheria ya watumishi walioajiriwa baada ya July 2004 mpaka sasa kanuni ya ukokotozi wa mafao ilibadilika na kuwa 25% malipo ya mkupuo na 75% inabaki ktk mfuko kwa ajili ya malipo ya kila mwezi mpaka mwanachama atakapofariki. Hivyo kama mil 100 utapewa mil 25 then mil 75 inabak.

Ila kwa walioajiriwa 2004 July kurudi nyuma kule wao kanuni yao ilibaki vile vile ya 50% malipo ya mkupuo 50% malipo ya mwezi. Hivyo kwa utaratibu huu kama zile percent zitawekwa kwa mwanachama wrote bila kujali uliajiriwa lini basi itawaumiza sana wale was 2004 kurudi nyuma. Ila mwajiriwa was baada ya July 2004 itambeba kwasabab atakuwa na nyongeza ya 13% kwenye malipo ya mkupuo.
 
Hii hata kwa sheria ya sasa hivi IPO hivyo yani katika 100% ya michango yako katika ukokotozi yule mtumishi anayeachishwa au kuacha kazi baada yaa kuchangia kwa miaka 15 atalipwa malipo ya mkupuo ambayo ni 25% ya michango yake. Halafu 75% itakokotolewa na kulipwa monthly kwa kipindi chote cha maisha yake hii itakoma pale mwanachama atakapofariki.

Ila kwa mtumishi atakayepoteza kazi kabla ya kuchangia ktk mfuko kwa miaka 15 huyu atalipwa 100% ya michango yake yote yani malipo ya mkupuo tu. Hataacha ile 75% kwa ajili ya malipo endelevu. Kwahyo huyu anamalizana na mfuko moja kwa moja anapewa chake chote anasepa.

Mkuu hebu nami nisaidie kidogo hapo. hiyo pesa inayobaki (75%) inalipwa kwa rate gani kila mwezi kama sio flat rate kwa wastaafu wote?
 
Mkuu hebu nami nisaidie kidogo hapo. hiyo pesa inayobaki (75%) inalipwa kwa rate gani kila mwezi kama sio flat rate kwa wastaafu wote?
Hii 75% inayobaki hailipwi kwa usawa kwa kila mwanachama. Inategemea ulikuwa unachangia kiasi gani ktk mfuko na hii inatokana na kiwango cha mshahara ulichokuwa unalipwa kipindi cha utumishi wako.
 
Back
Top Bottom