Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Muswada mfuko mpya hifadhi ya jamii, umebeba mambo mazito

Hakuna cha formula ya zamani wala formula mpya. Wamesema watakupa kiinua mgongo 32% tu na 68% iliyobaki utapewa kila mwezi kama mshahara wa watumishi unavyochelewa kwa mizengwe na kukupa stress ili ufe mapema. Hiyo hela siyo yao! kwanini waiwekee masheria kibao? Na wakiona ufi kwao inakuwa hasara. Lakini wajue sheria ni msumeno. Acha waendelee kuweka sheria kandamizi wasifikiri nao hawatafika umri wa kustaafu. Wacha waendelee kuweka sheria kandamizi bila kujua nao wana ndugu, watoto, waume, wake, ambao ni wafanyakazi ambao itawaumiza pia. Mungu linusuru hili taifa hatujui tunakoelekea!!
Yah kwa sheria ya sasa itawabeba waajiriwa wapya maana kanuni hii ya ukokotozi itawaongezea 13% ktk malipo yao ya mkupuo. Tofauti na awali ukokotozi ulikuwa 25% na 75%. Ila itawaumiza wa 2004 kurudi nyuma maana wale kanuni yao walisema wanaiacha ile ile ya zamani ambayo ilikuwa 50% mkupuo, 50% monthly.
 
SSRA nayo ivunjwe kwakuwa haina power ya kusimamia sheriadna kanuni zake kutekelezwa na mifuko ya jamii. Mfano ni pale ilipo shindwa kuilazimisha PPF kulipa madai ya wastaafu ATCL wakijua wazi mwajiri ndiyo alishindwa kuwasilisha michango ili hali wastaafu walikatwa mishahara yao kuchangia
 
Hakuna social security fund inayotoa 100% ya michango yako yote kama malipo ya mkupuo halafu tena ulipwe mafao ya kila mwezi mpaka atakapofariki. Duniani kote ni lazima uache percent itakayotumika kukulipa monthly. Bila hivyo hivyo hiyo itakuwa pyramid scheme
 
Kuna tatizo kubwa LA gender!? Inaonekana yanaelezewa matunzo kwa watoto pindi baba akifa! Ila watambue kifo hakibagui wasiwe biased
Nimesoma hayo maelezo nikachoka kabisa.

Gender...kwamba baba ndio mwajiriwa na ndiye atakaekufa.
Ulemavu....mtoto tu ndiye anaweza kuwa mlemavu, what about mama, baba, wakipata ajali au kuugua na kuwa walemavu? Macho, miguu, mikono n.k.

Walioandika huo muswada ni vilaza au walikuwa wanapewa maelekezo bila kuyatafakari.
 
Wanaongelea watumishi wa umma, wachangie 15yrs ndio wanaweza kuwa eligible khlipwa. What about private sector....swala la kudhibitishiwa na daktari au mwajiri kwamba sipo fit tena kuendelea na kazi ni ujinga mwingine huo. Wanawaaminisha watu kwamba maisha ni ajira tu tena za umma.
Kama nipo private sector, mkataba umeisha, inakuaje...kama anaamua kufungua kiwanda cha kutengeneza matikiti a.k.a shamba la matikiti, fedha zangu wanazirakia nini?
 
Yaani ukiangalia vizuri mfanyakazi muhusika hanufaiki na mafao yake, Maelezo yote utakuta mfanyakazi akifa mafao watapata watoto au mke au mlemavu ndiyo atafaidi, ishiii hivi vigezo vya ulemavu mbona wanavipenda sana, ukienda bodi ya Mikopo hivyo hivyo, aliyefiwa na wazazi au mlemavu ndiyo atapewa mkopo
Ni unyanyapaa....kwamba walemavu ni dhaifu na wanawake ni dhaifu na hawafanyi kazi/hawajaajiriwa.
Unaweza kuona ajna ya viongozi tulionao.
 
Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.

Nimeitoa sehemu, je ni kweli?
Mkuu samahani lakini unaweza kufanya citation kwa vipengele vya kwenye bill mfano hii bullet one unyoongelea asilimia ya malipo 38% unalipwa full then 62% monthly.. Samahani lakini wengine sio watu wa sheria bill nnayo ila kuitafuta sasa hizo vipengele
 
Ngoja wasomi waje watudadavulie maana mimi hata siwaelewi...yaani mtu kulipwa mpaka awe amechangia miaka 15?????kama hajatimiza iyo miaka 15 inakuaje sasa au ndo hela yake inakua ametoa sadaka tu?????
Endapo usipofikisha hiyo miaka 15 kuna kitu kinaitwa malipo ya mkupuo ambapo huangaliwa kiasi ulichochangia then huzidishwa kwa miaka uliyochangia na inaongezwa na faida ambayo itakokotolewa na mfuko. Halafu hayo mafao utalipwa mara moja (kwa pamoja) na hutokuwa na haki ya kupata malipo ya mwezi. Nadhani nimeeleweka
 
Naona akifa mama baba kama alikuwa baba wa nyumbani/ marioo watoto watateseka.
Watumishi wa kike hili ni lakuzingatia ukichagua mwenza. Kama ni masikini kabisa ukifa gafla watoto ni ombaonba hao, sasa chukua mtumishi au anayejiweza kiuchumi
 
Kwa kuusoma muswada huu, utagundua kuwa kuna harufu ya dhuluma kubwa mbele yetu. TUCTA, kumbukeni kila mwezi mnachukua asilimia mbili toka kwenye mishahara yetu. Waheshimiwa wabunge, chondechonde--msiupitishe muswada huu kwa sababu hauna sehemu unasema kuhusu watu waliopoteza ajira kwa kufukuzwa ama wanaopoteza ajira kwa redundancy. TUCTA msipopigania hili maana yake mmesaliti wafanyakazi, na hakutakuwa na maana ya wafanyakazi kuendelea kuwa wanachama wakati mnashindwa kuwatetea. Walisema kutakuwa na FAO LA KUKOSA AJIRA, ila haioneshi kama lipo. Enyi mliotunga haya, hivi mna roho gani nyie, mna dini kweli?
Fao la kukosa ajira lipo
 
Naona akifa mama baba kama alikuwa baba wa nyumbani/ marioo watoto watateseka.
Watumishi wa kike hili ni lakuzingatia ukichagua mwenza. Kama ni masikini kabisa ukifa gafla watoto ni ombaonba hao, sasa chukua mtumishi au anayejiweza kiuchumi
Kama baba alikuwa marioo sheria inamtaka athibitishe tu kuwa alikuwa akimtegemea mkewe na Atapata mafao kama ilivoonyeshwa kwa mwanamke (naye akioa tu mke mwingine na mafao yataishia hapo)
 
Wanaongelea watumishi wa umma, wachangie 15yrs ndio wanaweza kuwa eligible khlipwa. What about private sector....swala la kudhibitishiwa na daktari au mwajiri kwamba sipo fit tena kuendelea na kazi ni ujinga mwingine huo. Wanawaaminisha watu kwamba maisha ni ajira tu tena za umma.
Kama nipo private sector, mkataba umeisha, inakuaje...kama anaamua kufungua kiwanda cha kutengeneza matikiti a.k.a shamba la matikiti, fedha zangu wanazirakia nini?
Naomba yote wajadili Ila private sector ni watu ambao ni risk taker ni bora mtu sheria ihakikishe kila aliye kwenye ajira ni mwanachama Ila kama ajira ikisitishwa apewe malimbikizo yake!! Kwani unaweza kuwa mtaji wake WA kuanzisha shughuli nyingine
 
Kama baba alikuwa marioo sheria inamtaka athibitishe tu kuwa alikuwa akimtegemea mkewe na Atapata mafao kama ilivoonyeshwa kwa mwanamke (naye akioa tu mke mwingine na mafao yataishia hapo)
Sasa sisi ambao wote tunafanya kazi inakuwaje?
 
Hutopata mafao(either male ir female) kwa sababu unauwezo wa kuendesha maisha (according to them)
 
Bora wangeweka na option ya mtu kuamua kuchangia au lah? Ili kuondoa utata, mtu km ukiamua kuchangia basi ujue kbs kilichopo mbele yako ni nini?
Halafu haya mambo ya kutuamulia matumizi ya hela zetu sijui yanatoka wapi?
 
Wanaongelea watumishi wa umma, wachangie 15yrs ndio wanaweza kuwa eligible khlipwa. What about private sector....swala la kudhibitishiwa na daktari au mwajiri kwamba sipo fit tena kuendelea na kazi ni ujinga mwingine huo. Wanawaaminisha watu kwamba maisha ni ajira tu tena za umma.
Kama nipo private sector, mkataba umeisha, inakuaje...kama anaamua kufungua kiwanda cha kutengeneza matikiti a.k.a shamba la matikiti, fedha zangu wanazirakia nini?
Huo ndio ujinga sasa, hv contract ikiisha na hauna kazi na huko labda una milion kadhaa basi sijui ndio unakaa tu hadi ufikishe huo umri.
Mi nachukia kweli kujifanya wanatupangia hadi matumizi ya hela zetu, km vipi iwe ni uamuzi wa mwanachama kuchangia au lah.
 
Wanaongelea watumishi wa umma, wachangie 15yrs ndio wanaweza kuwa eligible khlipwa. What about private sector....swala la kudhibitishiwa na daktari au mwajiri kwamba sipo fit tena kuendelea na kazi ni ujinga mwingine huo. Wanawaaminisha watu kwamba maisha ni ajira tu tena za umma.
Kama nipo private sector, mkataba umeisha, inakuaje...kama anaamua kufungua kiwanda cha kutengeneza matikiti a.k.a shamba la matikiti, fedha zangu wanazirakia nini?
Kama mkataba umeisha kuna mambo mawili, kama utapata ajira sehemu nyingine maana yake uanachama wako hautakoma michango yako itaendelea kwenda ktk mfuko wako.

Ila kama utakuwa hujaajiriwa tena bado kuna fao la kujitoa uanachama kwa wale ambao hawajatimiza 15 yrs ya uchangiaji ambapo atalipwa kwa mkupuo michango yake yote.
 
Kama baadae wataondoa FAO la kujitoa maana yake hata kama umefanya kazi miaka 3 na ukaiacha hiyo kazi ukiwa na miaka 30 itakupasa usubir mpaka 55. Ila kwasasa FAO la kujitoa bado lipo.
 
Back
Top Bottom