Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

Kweli ccm mwaka huu hawana pa kutokea....huku Bara moto,visiwani moto. BIg up wazanzibari kwa kuuchanachana huo muswada wa ccm.
 
Safi sana kwa kuuchana huo muswada big up zenj watakanyika uchomeni moto mbele za media tena bbc na cnn dunia ifahamu fast moto umewaka bongo.
 
Thanx jabulani, ni ndefu lakini nimeisoma.
Summary yangu ni kuwa zanzibar imefanya marekebisho kwenye katiba yake na kupokonya yale yaliyokuwa chini ya Serikali ya Jamh. ya muungano Tz, ilhali viongozi wa SJMT wanajua na wasiseme.
Kwamba Zanzibar inatambulika kama nchi kamili yenye mipaka na jeshi na mahakama.
So?
Kumbe Muungano ushavunjika siku nyingi tu!
 
haya anna makinda sema!huku bara unasema wanasiasa wanawachochea wanafunzi jee huko zenj sheikh kachochewa na nani?
 
Najua maandishi haya ni mengi na huenda yakawachosha kusoma, lakini mwenye muda asome. Hapo ndipo mtakapojua kwamba CHADEMA ina wabunge makini sana. Tundu Lissu aliwahi kuongea bungeni na kwenye mihadhara mbalimbali ikiwamo pale Nkrumah, lakini alipoongea bungeni nakumbuka wabunge wa CCM walibeza na kusema kwamba "MUUNGANO NI IMARA !" Anne Kilango alikuwa mmojawapo akiijibu hoja ya Lissu kwa mifano ya maridhiano ya CUF na CCM. Huenda wabunge wa CCM hawajui maridhiano ya vyama ni kitu tofauti na Muungano wa nchi. Hii hapa chini ni makala ya mbunge mahiri Tundu Lissu:

 
Mkuu! muungano unafaida kwa CCM tu. Faida yao ya kwanza ni wakati wa uchaguzi mkuu....maana wanapata kura nyingi sana za mgombea wao wa urais (kumbuka wazanzibar wanaruhusiwa kumpigia kura mgombea urais kutoka bara,ila sisi wabara haturuhusiwi kumpigia kura mgombea urais wa visiwani) so kwa mtaji huu CCM huwa wanavuna kura nyingi sana kutika Zanzibar. Faida yao ya pili ni pale wahisani wanapotoa misaada kwa ajiri ya watanzania wote,yaani ikiwemo zanzibar (Kumbuka wahisani wanazisaidia hizi nchi za Africa kulingana na idadi ya wananchi) So chama cha mafisadi(CCM) kimejitengenezea mrija mwingine wa kula fedha za wananchi kwa mgongo wa wazanzibar na wabara kwa kujumlisha wingi wetu pale wanapoomba misaada toka nje ya nchi. Kwa ufupi hakuna mtu mwenye faida ya huu muungano isipokuwa ni miCCM yenyewe tu!.....wanafaidika kwa kupata kura za mgombea wao wa urais na kupatia misaada kutoka nje ya nchi.
 
Nadhani ukweli utagundulika muda si mrefu...ukombozi wa Taifa hili umekaribia,mapambano bado yanaendelea na hakuna wa kuyazuhia hata iweje....si JK,EL,wala RA....hukumu kwa waovu yaja na watakinywea kikombe cha hasira ya watanzania....
 
Jamani Ndugu zangu watanganyika ni wakati sasa wa kuvunja huu muungano, nawakilisha hoja.
 

mtu mwenye akili huwa anajituma wala hategemei cha bure. angalia uganda baada ya kuwatimua wahindi wakidhani wanawakomoa na kuchukua mali zao kiko wapi leo. baada ya kuuvunja muungano na kuwatimua wazanzibar nahisi itabidi ushauri tuwatimue wahaya na wachaga warudi moshi ili ufaidi mali zao. itungwe sheria kama mchaga au mnyamwezi marufuku kumiliki ardhi nje ya mikoa yao. nahisi kama tutatumia akili zako finyu huku ndio tutafikia.
KABLA HUJATOA MAONI YAKO SHIRIKISHA UBONGO WAKO.
 
Najua maandishi haya ni mengi na huenda yakawachosha kusoma, lakini mwenye muda asome. Hapo ndipo mtakapojua kwamba CHADEMA ina wabunge makini sana. Tundu Lissu aliwahi kuongea bungeni na kwenye mihadhara mbalimbali ikiwamo pale Nkrumah, lakini alipoongea bungeni nakumbuka wabunge wa CCM walibeza na kusema kwamba "MUUNGANO NI IMARA !" Anne Kilango alikuwa mmojawapo akiijibu hoja ya Lissu kwa mifano ya maridhiano ya CUF na CCM. Huenda wabunge wa CCM hawajui maridhiano ya vyama ni kitu tofauti na Muungano wa nchi. Hii hapa chini ni makala ya mbunge mahiri Tundu Lissu:

 

Mmmh....kumbe hata kwenye siasa maama humo?.... nilifikiri wewe ni ant kikombe tu basi! Anyway nimefarijika kuona tupo pamoja ktk kuikomboa nchi yetu Tanganyika hadi kieleweke....Big up dada
 
....Kwa kuwa wazanzibari wamesema kuwa tumewanyonya kwa muda mrefu..na kwakuwa wazanzibari hawatusaidii chochote,na kwakuwa Tanganyika yetu imefunikwa na hili li-Muungano...Mh muanzisha thread naunga mkono hoja kwa asilimia 100...Ahsante
 
Muungano ni mzigo usiobebeka, hakuna mtu anayefaidika nao zaidi ya viongozi wanafiki, umefika sasa wakati wa kuuvunja, kila mtu aende kwa amani
 
Jamani Ndugu zangu watanganyika wakati sasa wa kuvunja huu muungano, nawakilisha hoja.

WaTanganyika ndio taifa gani? Mimi nilizaliwa Tanganyika, lakini hiyo nchi ilikufa na hakuna mahali ilipo. Rais wake nani? Bunge lake lipi? Bendera yake ipi? Mbona tunakuwa wanafik, hatutaki kusema kuwa nyerere aliiuwa Tanganyika?

Hakuna wa Tanganyika. Tuanze kwa kudai uhuru toka Tanzania, hususan Zanzibar kwani wao ndi wenye nchi. Sisi tuanze kutafuta jina la kuipa nchi tutakayoidai.
 
Naililia nchi yangu Tanganyika, nani wamekupoteza Tanganyika yetu? Bila Tanganyika hakuna muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…