Musukuma na Bashe ndio wabunge wa CCM ambao wamethubutu, hongereni

MAGACHA

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,076
2,000
Nimekuwa nikifuatilia siasa za chama cha mapinduzi kwa ukaribu sana na kwa miaka mingi nimegundua yafuatayo.
1,Wanafiki,wanasiasa wengi waliomo ndani ya chama hiki ni wanafiki sana,wanajua kuyaongelea ya wengine na kuyaacha yaliyomo ndani ya chama chao,mfano,kwa miaka mingi kulikuwapo na watuhumiwa wa ufisadi katka nchi hii lakini hakuna hata mmoja amewahi kusimama hadharani na kuwataja fulani na fulani mnatuharibia nchi,mfano Chenge,Thibaijuka,Rostam Azizi,Lowasa,na wengine kibao na hadi juzi waliotajwa kwenye ripoti ya makenikia tofauti na musukuma,wabunge wa ccm wengine wamejitoa akili kana kwamba hawawajui waliotajwa,badala yake wanakomaa na wapinzani kana kwamba wapinzani ndo wametajwa na kamati ya osoro,

2,Hawataki kuwa wazi,wanasiasa wengi wa chama hiki,na wengine waliomo ni madokta na maprofesa lakn kwenye ukweli hawataki kusema ukweli,hujitoa akili kwamba linalofanyika hawalijui hivyo hadi kuruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa,mfano,bajeti kwa asilimia kubwa huwa hazitekelezeki,badala yake profesa anasimama bungeni anapongeza bajeti kwa kutotekelezeka ,kwel wabunge wa ccm badala ya kuisimamia serikali,muonyeshe ukali kwa kutotekelezeka kwa bajeti hadi serikali ilete majibu yanayoeleweka,badala yake naunga hoja asilimia mia,siyo siri hii nchi haijitambui

Pongezi ziende kwa waheshimiwa hawa wawili,
Musukuma, amethubutu kusema sisi ccm ndo tunafuga wezi,amejitambua hadi na kuwataja,MTU kama Ulega hajitambui anachokifanya anakijua mwenyewe
Pongezi pia zimwendee Bashe,mhe anachangia kwa fact,anaikosoa serikali,hajatumwa kuipambia serikali,anataka serikali ifanye kazi,huwa namkubali sana mh kwenye michango yake,
Ushauri ,Wabunge wa ccm acheni kuipambia serikali,ibane serikali ifanye kazi,huku mtaani hali ni mbaya haijawahi kutokea,wanafunzi kujiunga na elimu ya juu ni shida,watanzania wanashindia uji,nyie pigeni meza lakini siku zenu zinakuja,halafu hawa wabunge wasichokijua ni kuwa,wakiibana serikali,wananchi hawatakuwa omba omba kwa wabunge,maisha yao yatakuwa mazuri,pia mjue serikali haina shukurani hata siku moja,serikali inakutambua wakati ukiifanyia kazi au kama uko hai kwa mbali kidogo,kufa uone,mazishi watafanya halafu wakiondoka,wala hawatajua kwamba familia yako ikoje,kwa hiyo unapoisimamia serikali kwa umahiri na serikali ikafanya kazi,maisha kwa familia yako yatakuwa mazuri,kwa familia ,jamii inayo kuzunguka na Taifa,
Ccm acheni kuliangamiza Taifa
 
  • Thanks
Reactions: MTK

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,152
2,000
Hivi hakuna wa kumkumbusha Bashe kuwa kuna nafasi yake UKAWA inamsubiri kwa hamu!!!???
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,521
2,000
angalau msukuma pamoja na elimu yake ya darasa la saba amekuwa jasiri. miprofessa mingi iliyoko ccm si jasiri zaidi ya unafiki wa kulilia vyeo. hongereni geita kwa kumpata mbunge jasiri.
 

MAGACHA

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,076
2,000
Hawa ndo wale waliomo ccm, ambao wanashtumiwa kuwa ni wezi halafu wanashindwa kuwajadili bungeni,Acheni musukuma hana unafiki huo,anasema,"kila kashfa chenge,kila kashfa chenge,hivi ccm halioni hili"big up musukuma
 

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,096
2,000
Pamoja na yote, mimi nina mashaka na Msukuma. Akili yake haijakaa sawa. Nakumbuka haya:
-Huyu alikuwa swahiba wa Edward mpaka kushinda jikoni kwake na hata kuchunga ng'ombe kwake. Ghafla alibadilika na kutoweka kabisa akiihama kambi hiyo.

-Aliwahi kufukuzwa kwenye council yao kwa kuwa na msimamo wa kudhibiti mapato na matumizi ya council hiyo. Baadaye alirudi na kuanza kuunga mkono matumizi mabaya kuliko ya awali.

-Juzi juzi alikamatwa na polisi Dodoma kwa kujiunga na kundi lililokuwa linakataa udikteta na ubabe ndani ya CCM. Hivi sasa amegeuka jumla jumla kana kwamba si yule aliyelala central Dodoma akihema na kulaani CCM na Mwenyekiti wake. Hadi polisi waliomuhoji wanashangaa wenyewe.

-Alipotoka Dodoma akaenda Geita na kuitisha vikao vya siri akiwashawishi wana CCM waitishe kikao na kumfukuza uanachama JPM ili iwe skendo ndano ya CCM. Hivi sasa aliowaita wanashindwa hata kumuangalia usoni.

Kwa upande wa Bashe, nakubaliana na observation ya mleta mada. Namwona kama mbunge mwana CCM anayejua nini maana ya kuwa mbunge. Hajishughulishi na umbeya - yeye ni facts tu. Yeye Bashe, Zitto, Tundu, Zungu, Sauda Mkuya, na kiasi fulani Mdee, ni wabunge hazina.
 

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
2,358
2,000
Njaa mbaya,ukiishi kea hisani na ujanjaujanja hauwezi kuwa mkweli na mtetea hali!!!
 

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,951
2,000
Mimi napenda michango ya Ms Kiteto Zawadi Koshuma (Viti Maalumu - CCM) kwa michango yake ya mawazo anajikita katika kutetea akina mama na watoto. Ushauri wa bure, apunguze ushabiki wa kichama uliopitiliza abaki kwenye facts, principals, sheria na kanuni.
 

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,731
2,000
IMG_20170601_142426.jpg
 

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,469
2,000
Hivi hakuna wa kumkumbusha Bashe kuwa kuna nafasi yake UKAWA inamsubiri kwa hamu!!!???

You don't need to be in the opposition in order to challenge the government and its policies.
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,812
2,000
You don't need to be in the opposition in order to challenge the government and its policies.
Kama si hivyo basi Je ni kwanini waliwatupa ndani kule Dodoma? Je nikweli mtu anaweza kuwapinga CCM akiwa mwenzao na wakamuacha salama? Ikiwa hivyo ndivyo basi nitawapongeza ikiwa watamuomba Sophia Simba na wenzake msamaha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom