Isakhamisi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 360
- 414
Msukuma uko sawa kabisa hao ni sawa na kina kabudi wameweka maslahi yao mbele kuliko taaluma zao wameokotwa majalalani wanafuata upepo unapoelekea.Mbunge wa Geita Vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema Maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.
Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.
Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?
Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.
Chanzo: Clouds Digital