Muslim University of Moro Graduates huishia wapi?

and 300

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
26,325
36,121
Chuo hiki kikuu kilichopo maeneo ya Msamvu Morogoro, kilianzishwa mara baada ya kupewa majengo yaliyokuwa Chuo cha TANESCO pamoja na kuzalisha wahitimu toka enzi hizo na kufungua matawi sehemu kadhaa za pwani ya Tanzania (ikiwemo Zanzibar - Unguja) ni vigumu sana kukutana na wahitimu hao sehemu za kazi, biashara na nyanja mbalimbali za kujenga uchumi.

Tuseme hawa wahitimu wanajiajiri tu kwenye sekta zisizoonekana kwa macho? ama wanaishia ughaibuni ambako ni ngumu kuwa-track?

** Tafadhali usichafue hali ya hewa ni katika kutaka kujua tu ili kupima ubora unaoimbwa na TCU katika vyuo vikuu Tanzania.
Je Wahadhiri wake wanaajiriwa kwa sifa zipi? Je TCU inaweza kwenda kupitia CV zao na kujiridhisha? Bila kupata figisu figisu kwa uongozi wa chuo husika?
 
Hawa jamaa sidhani kama watasalimika aisee! kile chuo namna wanavyodahili wanafunzi wao UTAFURAHI na roho yako, katika vigezo vyao wanajumuisha ni RELIGIOUS SUBJECTS ambazo wengi huibuka na GRADE ZA "A" huku masomo ya ELIMU DUNIA mtu na "F"F" F" kinachofundishwa lecture theatres nako ni utata mtupu. Waajiri wengi pia hujitenga na wahitimu toka taasisi hii PENDWA
NB: Wengi waliajiriwa kipindi ambapo walimu wengi walikuwa wanaajiriwa tu sasa unamkuta mtu SOMO LA KUFUNDISHIA: Somo la DINI tu sasa sijui huko shule anaenda kuwafundisha nani dini. INATIA HASIRA SANA.
 
Waaambie Muslim haiangalii no ya udahili kama vyuo vya ambavyo vpo kibiashara zaid watu 486 wote felia wamepelekwa sua imebiid warudishwe nyuma
 
Vyuo vikuu hivi vinavyomilikiwa na taasisi za dini ni kazi sana asee unakuta sijui shehe/ulamaa sijui padiri elimu yenyewe ya kuunga unga nae ana cheo huko chuoni sijui Faculty Dean, sijui Deputy Vice Chancellor yaani ukimcheki tu kwa jicho la haraka haraka bora mbunge wetu wa pale stendi ya kwenda nje ya dar.
 
Usiwe unaongea vitu bila kuwa na uhakika mkuu;
Una uhakika gani St Joseph ni Mali ya kanisani katoliki. Wale ni wawekezaji kama wengine wanaotumia jina la mtakatifu joseph basi....
Jifunze kuongea ukiwa na uhakika
893f516f5cd34cea1cd122680f0ed907.jpg
 
Back
Top Bottom