Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Chama cha National Resistance Movement (NRM) cha Uganda, kimesema Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni atachukua fomu za kutetea nafasi yake kwa muhula mwingine wa miaka mitano katika uchaguzi unaotarajiwa mapema mwaka ujao 2026.
Kama atachaguliwa, Museveni ataongeza utawala wake wa takriban miongo minne, kulingana na afisa mkuu kutoka chama tawala.
Ingawa alitarajiwa kugombea tena wadhifa huo, ni uthibitisho wa kwanza kutoka kwa chama chake cha
Uganda itafanya uchaguzi wake mkuu Januari 2026 ambapo wapiga kura pia watawachagua wabunge.
Museveni, 80, amekuwa madarakani tangu 1986 na ni kiongozi wa nne barani Afrika aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi. Chama tawala kimebadilisha katiba mara mbili huko nyuma ili kumruhusu kuongeza muda wa utawala wake.
Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa chama cha NRM, imesema Museveni atachukua fomu katika ofisi za Tume ya uchaguzi za chama hicho Jumamosi Juni 28, 2025 ili kutetea uenyekiti wa chama hicho na kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya NRM, Tanga Odoi akizunguza na waandishi wa habari leo Juni 24 jijini Kampala.
BBC