Mjukuu wa Sechenga
Member
- Nov 13, 2015
- 34
- 37
Rais Yoweri Museveni amezindua basi la kwanza katika eneo la Afrika mashariki linalotumia nguvu za jua. Mabasi hayo yalitengezwa nchini Uganda na kampuni ya magari ya Kiira Motors Kayoola.
Yalionyesha mara ya kwanza hadharani katika uwanja wa taifa Kampala mapema mwezi huu.
Moja ya betri zake inaweza kutiwa chaji na vibamba vyenye chaji ya miale ya jua vilivyopo katika paa la magari hayo ambavyo huongeza kasi ya gari hilo kufikia kilomita 80.
Basi hilo lenye viti 35 linatarajiwa kutumika mijini badala ya miji mikuu kutokana na masharti ya umbali wa usafiri wake. Iwapo yatatengezwa kwa wingi, kila basi linaweza kugharimu dola 58,000 ambayo bwana Musaizi anasema ni bei nzuri katika soko.Kampuni ya magari ya Kiira Motors ilikuwa kufuatia mradi wake katika chuo kikuu cha Makerere,ambacho kinamiliki hisa katika kampuni hiyo na ambacho pia kimefaidika na fedha za serikali.