Inastaajabisha! Siasa majitaka na uchawa zinadidimiza Taifa hili

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
Tusipozinduka sasa, tutakuja kuamka na kukuta majirani wako dunia nyingine, Pamoja na hali ya siasa za ndani Uganda kuwa ni za kidikteta, Lakini taifa hilo linazidi kupiga hatua kubwa, Kupitia kiwanda chake cha Magari cha Kiira Motors LTD, Mwaka 2018 ilianza rasmi kuzalisha mabasi yanayotumia umeme jua. Mradi huu sasa umekuwa mkubwa na kama unavyoona katika picha mabasi ya kiraia sasa yanazalishwa katika kiwanda hicho kwa wingi sana.

Ikumbukwe kwamba Tanganyika ilikuwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha magari kabla ya uhuru pale Keko Chang'ombe kiwanda hicho kilikuwa maalumu kuzalisha magari aina ya Land Rover, na baada ya Uhuru sera za ujamaa zilikiondoa kiwands hicho na waingereza wakarudi nacho kwao, Baada ya Ujamaa kukolea Tanzania tulijengewa kiwanda kingine kule Kibaha kinachoitwa Nyumbu, (Lokomotiv), kwakutumia teknolojia ya Moscow tukafua vyuma na kuunda magari, lakini sera zetu za undumilakuwili yaani leo unakula soseji Moscow, kesho unakula siagi Washington, zilisababisha kiwanda kufa. Japo juzi kimerudi kianiaina.

Niliwahi kueleza katika Kitabu cha Ujasusi kwamba kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii linatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya makataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na uwezo wa kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badi ingekusanya gawio toka kwa chombo kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake. Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha iliutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa.

Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi kusitisha, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5, hii ni Bandari inayotajwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania la kutaka kujenga vinu vya kuchenjulia madini sasa imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Unaweza kufikiria, juzi tu kampuni kubwa dunia ya Microsoft imefungua kituo chake Nairobi Kenya kwa Afrika, Hiki ni kituo muhimu ambacho tungekipata kingesaidia sana ulinzi wa nchi kimtandao, kingetoa ajira kubwa kwa watu wetu, na kingelipa kodi kubwa na kusaidia uchumi wetu. Elon Munsk anataka kuleta huduma ya Satellite ya Starlink ili kupata internet ya bei ya nchini na ya haraka zaidi duniani, Serikali imekuja na hoja dhaifu sana kwamba ati Elon ajenge ofisi hapa Tanzania na Seva zake aziweke hapa Tanzania ili iwe rahisi kwa Kamilius Wambura na Kingai kwenda kuzichokonoa chokonoa Seva hizo wakiwa wanawatafuta akina Yericko na Chadema.

Wasichojua ni kuwa katika dunia mpya ya leo data haziwekwi kwenye Seva tu zikatulia kama maji ya mtungi, bali zinawekwa pia kwenye iCloud ambako ni angani huko dunia. Masikini Tanzania yangu, tuko na watu wanaofikiria madaraka zaidi nk. Angalau kidooogo walewale walioua kiwanda cha umma cha Nyumbu kule kibaha wameanza kuzalisha Magari tena. Jambo jema.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Nimejitahidi kueleza Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwamba, Ujasusi wa Kiuchumi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana. Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo kwa Tanzania basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za Ujasusi wa Kiuchumi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Urusi chini ya Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kijasusi na kununua sensitive Navy informations za USA na kuweza kutengeneza balance ya Navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Jasusi Johny Walker Junior. Leo Dunia ya kijeshi ya Nyuklia iko mikoani mwa Urusi, kwa miezi 13 sasa Mataifa 67 ya Ulaya na Marekani yameshindwa kuiangusha Urusi kupitia Ukraine.

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa kifikra na Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa ya sasa ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado "unaiserve CCM kwanza" kisha ndio Taifa linatafsiriwa liko salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm. Kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Ujasusi wa kidola wa kulinda serikali na chama tawala limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, hii haikubaliki.

Tunahitaji mabadiliko makubwa ya lazima na ya haraka sana, mfumo wa Idara ya Usalama wa Taifa na Mfumo mzima wa Ulinzi na Usalama, Dunia haijasimama inasonga mbele, taifahaliwezi kushinda na majirani zetu ikiwa mfumo wa Usalama wa taifa bado uko kwenye usingizi wa Ujamaa, Mfumo ambao roho yake iko kwenye siasa za vyama hauwezi kulisaidia Taifa hili kiuchumi
 
Back
Top Bottom