Museveni Aliwachachafya Maprofesa Mlimani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Museveni Aliwachachafya Maprofesa Mlimani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumaku, Sep 30, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  • Aliwachachafya maprofesa Mlimani
  • Alikwenda vitani Vietnam na Msumbiji
  Na Born Again Pagan

  KWA wale wenye kupenda kumjua Yoweri Kaguta Museveni, mwanafunzi wa Mlimani, someni yafuatayo:

  Yoweri Kaguta Museveni alijiunga Mlimani kutokea Uganda, kama mwanachama wa UPC Youth League. Pengine ndio sababu ya kuwa karibu sana na TYL. Alichukua BA (General) ya 3:2:2 (Historia, Sayansi ya Siasa na Uchumi) mwaka wa kwanza. Ali-“drop” Historia na kumalizia na hayo mengine mawili.

  Wanafunzi wote wa ki-Tanzania waliokuwa wanachukua Science iliwabidi wachukue pia Elimu, na wale ambao walikuwa wakichukua Elimu iliwabidi wote wamalizie na 3:3:3!

  Nilikutana na Yoweri Museveni mwaka wa kwanza katika somo la Historia, chini ya ma-Prof. Walter Rodney (Imperialism and Colonialism); Isaria N. Kimambo, Arnold Temu na John Illife (The Comparative Analysis of the Rise of Nationalism: Tanzania, Ghana, India, and China), Terence Ranger (The Rise of the Industrial State: Britain, Russia and United States), John Illife (Disintegration and Integration of African Societies: The Role of the Educated Elites) na John Sutton (Mambo ya Kale – Archaeology).

  Museveni na wembamba wake alikuwa “a recluse” (mpweke). Mtu yeyote asingeweza kuyajua yaliyokuwa akilini mwa Yoweri Kaguta Museveni! Lakini aliweza kujitoa kwenye cacoon (uzimzinga) na kuanza kutetea msimamo wake. Alikuwa mwenye machachari mbele ya ma-Profesa na waadhiri aliowaona kuwa wa upande wa mkono wa kulia au hawakujua walichokuwa wakifundisha.

  Kama profesa/mwadhiri hakujua anachosema (au ni wa mkono wa kulia sana), Museveni aliweza kutoka nje ya mdahalo na kuwaita wale ambao aliwafikiria ni “ma-komrade” wake na kusema, “And you (na kutaja majina) are still sitting there!”

  Tatizo kubwa lililojionyesha wazi ni kwamba Yoweri Kaguta Museveni alikuwa kichwa maji! Pengine ni baadhi ya wanafunzi wachache tu walioweza kumbadilisha msimamo wake katika mambo mengi maishani. Alikuwa akiyavalia njuga za “blinkers” (bila kutaka kuona upande mwingine).

  Yoweri Kaguta Museveni alikuwa na tabia ya kutukana wale ambao hakuafiki nao, “You are a bunch of reactionaries!”

  Yoweri Kaguta Museveni alitumia muda wake mwingi kujisomea mwenyewe maktabani na kuandika kazi aliyokuwa amepewa. Wakati mwingine alikuwa anakwenda kwenye ofisi ya FRELIMO na vyama vingine vya ukombozi na Ofisi ya Ugenini (exile) ya Vietnam siku nzima na kurudi jioni. Wanafunzi wengi waliamini kuwa pengine ma-Profesa wangeweza kumfelisha Museveni katika mtihani wa mwisho kutokana na kutohudhuria midahalo na semina.

  Yoweri Kaguta Museveni alipenda riadha na soka. Hakunywa pombe, kama walivyokuwa wanafunzi wengi; alipendelea kunywa soda ya Fanta.

  Kulikuwa na upande mwingine wa Museveni – Museveni ambaye wengi wetu tulimwona kuwa alikuwa “extraordinarily compassionate” kwa walalahoi. Ikumbukwe kwamba alikuwa ni mwanafunzi mgeni wa Tanzania.

  Yoweri Kaguta Museveni hakutaka kubakia mgeni wa Tanzania, kulingana na msemo, mgeni siku ya kwanza, siku ya pili jumuika na wenyeji wako katika kulinda maslahi ya jamii!

  Kwahiyo, Museveni alijumuika kikamilifu (hata kuwashinda wanafunzi wengine wa-Tanzania – pamoja na baadhi ya wana-USARF) katika kusaidia kuokota korosho hapo kampasi siku za Jumatano alasiri na kuvuna mpunga wikiendi.

  Yoweri Kaguta Museveni alikuwa jasiri! Wakati wa mapambano huko Vietnam, Ofisi ya u-Balozi wa Serikali Ugenini (exile) ya Vietnam mjini Dar es Salaam iliwakaribisha wanaharakati viongozi wa wanafunzi (USARF/TYL) kwenda nchini Vietnam kuona makali ya moto wa vita vya mapambano baina ya Marekani na Vietnam.

  Wakati wa likizo, Yoweri Musevenii (USARF), Henry Mapolu na Andrew Shija (USARF/TYL) walikwenda na kurudi salama, na kutuhakikishia: Amerika itapigwa tu! Hapo baadaye ujasiri wa namna hiyo uliwapeleka tena (natumaini waliongozana na kijana mwingine Salim Msoma) kwenye mapambano ya FRELIMO dhidi ya Wareno huko Msumbiji Walienda na kurudi salama! Ujumbe wao ulikuwa sawa na ule wa kutoka Vietnam: Wareno watachapwa tu!

  Kwa kulilia walalahoi na ujasiri wake kulivuta baadhi ya wanafunzi wengi kumpenda Yoweri Kaguta Museveni. Wanafunzi wengine, Hirji, Salim Msoma, Henry Mapolu (wa-Tanzania) walikuwa wana-USARF wakereketwa na Museveni, licha ya kuwa wana-TYL.

  Vijana wa msimamao mkali walipohitimu machi, 1970, walitawanyika Tanzania, Uganda, Kenya na hata Guinea. Yoweri Kguta Museveni alikwenda kufanyakazi Ikulu ya Uganda chini ya rais Milton Obote. Na wakati Idi Amin anampindua Rais Obote, Museveni alirudi Tanzania kufundisha hapo Chuo cha Ushirika Moshi na hapo badaye kuanzisha chama chake cha ukombozi wa Uganda, Front for National Salvation (FRONASA) na wenzake waliokuwa nao hapo Mlimani.

  Salim Msoma alikwenda kufundisha Elimu ya Siasa hapo Business College. Hirji alipelekwa kufanya kazi ya Afisa wa Wilaya, Sumbawanga. Henry Mapolu (nafikiri) alikwenda kufanya kazi Kiwanda cha Urafiki. Ali Mchumo alikwenda kuwa mwana-sheria wa Jeshi la Kujenga Taifa. Charles Kileo alijiunga na TANU hadi kuwa Mkuu wa Mkoa Mtwara.


  Emily Ndonde (nadhani) alijiunga na Ikulu. Inaendelea Jumanne ijayo.
  Romuinja@yahoo.com
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hongera Yoweri Mseveni
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hawa wasomi wa miaka ya 60 na 70 wengi walikuwa Wazalendo na walifundishwa uzalendo lakini cha kushangaza wengi wao walipoingia kwenye system wakageuka kuwa mzigo kwa nchi zao.

  Museveni amesahau yote aliyokuwa anayatetea miaka hiyo na sasa hana tofauti na viongozi wengine wengi wa Afrika ambao wamejaa ubinafsi na kushindwa ku deliver ahadi zao kwa wananchi ambao wanazidi kuwa maskini.
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sawa tunaangalia kwa nn museveni amekuwa king'ang'anizi uganda ?
  au ndio anaamini ni yeye tu anaweza kuongoza uganda ?
   
 5. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  hawa wenzetu akina lowasa , kikwete, walifanyia nini taifa kwa elimu nzuri na mwamko pale udsm wakati wa Nyerere? ikumbukwe kuwa tulikuja pale baadaye tuliundiwa matatizo lukuki kama ukosefu wa chakula, maji, ada, allowance, tukajikita katika haya tukasahau mustakabali wa bara letu na Taifa letu
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Historia....ni nzuri sana kuijua na vizazi vijavyo lazima waijue wasidhanie haya mambo ya sasa yameiota ota tu kama uyoga...maana rika la sasa wanapenda short cut methods....sio kwa kila kitu........
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Mkuu Mtanzania.......

  Nimewahi "bahatika" kuwa karibu na Mkuu huyo (Wilayani Mbarara)...........trust me hiyo tabia hapo juu........mpaka leo hii iko pale pale.......what he fights for what he believes......kitu ambacho may or may not bear good results............

  notwithstanding that.......he has so many positive things for Uganda
   
Loading...