BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,005
- Thread starter
- #41
Sina la kuongezea. Umewekewa statistics na uzioni! Nchi yenye kipato cha US$ 288 bado tunadai ni tajiri? Haya mimi na wenzangu kama mimi tukichukua stahili yangu ya US$ 24,000 kwa mwaka, ambao si wa kukufuru, kutabaki nini? Nani alikuambia nataka kuishi maisha ya shida au ninaishi maisha ya shida? Ninachokataa ni hii tabia ya kusimplify mambo. Tukiuza magari, wote tutapata neema? Tunamdanganya nani? Tatizo ni kubwa zaidi. Pamoja na kubanana mbavu inatubidi wote taufanye kazi ya ziada kujikomboa. Na haitatokea kesho. Na nyinyi mnaokaa nje sio panacea. Msome Kitila Mkumbo na umuelewe.
Pato linaonekana dogo kutokana na mafisadi na wizi wanaoiba mapesa chungu nzima na rasilimali zetu zinazoporwa mchana kweupe. Statistics za kutupora, wizi na ufisadi mbona hujaziweka, je unajua kama ni kubwa!? Si umesema hutaki kulipwa mshahara wa kufuru, nikakuuliza mshahara wa kufuru ndio upi? hadi sasa umeshindwa kujibu.
Ndio nyinyi mkipata uongozi mnasema Watanzania hawastahili mishahara mikubwa maana wataishia kuoa wake chungu nzima, kuwa na nyumba ndogo na ulevi. Nani kasema tuuze magari? uwe unasoma kabla hujajibu siyo kukurupuka tu! Nimesema tunaweza kupunguza gharama kubwa za uendeshaji kama watakaostahili kuwa na magari yanayohudumiwa na serikali ni watu wachache tu wengine wote wajitegemee wenyewe, kupunguza ukubwa wa sirikali na kupunguza safari za nje ya nchi na idadi ya wasafiri katika safari hizi hii itashusha kwa kiasi kikubwa gharama hizi na savings zinaweza kuhamishiwa sehemu nyingine.
Sina haja ya kumsoma yeyote, wasomi Watanzania hawasikilizwi wako tayari kabisa kuchangia maendeleo ya nchi yao lakini maoni yao miaka nenda miaka rudi yamekuwa yanatupwa kapuni matokeo yake wamegundua kwamba kuna nchi ambazo zinathamini mchango wao na elimu yao na wakati huo huo wanalipwa vizuri.
Nyie kaeni na ngonjera yenu ya tangu mwaka wa 47 kwamba "Tanzania ni nchi maskini" wakati tunaona viongozi na familia zao wanakuwa mabilionea kila kukicha.