MUONGOZO JAMANI au KUHUSU UTARATIBU

MUONGOZO JAMANI au KUHUSU UTARATIBU

Mimi ni mpya humu chit chat, nauliza kuhusu utaratibu....nini hasa kinafanyika huku, isije kuwa watu wana cheza disco humu mimi nikaanza maombi! Nawasilisha

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Karibu sana DONNYANGAKA , huku ni stress freezone, tunachangamana, tunawasiliana na kufurahi mwanzo mwisho. Tunaheshimiana na kupendana sana. Hatuulizani dini, kabila, itikadi ya kisiasa wala timu ya mpira unayoshabikia, jinsia utaulizwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na shughuli nyingine za kibailojia, Otherwise CHIT CHAT MUCH FUN MUCH LOVE..!!
 
Last edited by a moderator:
Shem, mzima weye??? hivi ni lini utaacha kudunda dunda kwa hiyo keyboard???

Hadi akili imkae sawa ndo ataacha, siku akitulia na mume mmoja ndo utamuona kaacha kudundadunda, vinginevyo sahau..!!!
 
Hadi akili imkae sawa ndo ataacha, siku akitulia na mume mmoja ndo utamuona kaacha kudundadunda, vinginevyo sahau..!!!

Unanitaka?
Unanitaka?
Nakuuliza unanitaka Baba V?
 
Last edited by a moderator:
Shem, mzima weye??? hivi ni lini utaacha kudunda dunda kwa hiyo keyboard???

Me Mzima Shem wangu handsome watu8.
Nitaacha kudunda dunda siku nikipata Mwanaume wa Ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Karibu sana DONNYANGAKA , huku ni stress freezone, tunachangamana, tunawasiliana na kufurahi mwanzo mwisho. Tunaheshimiana na kupendana sana. Hatuulizani dini, kabila, itikadi ya kisiasa wala timu ya mpira unayoshabikia, jinsia utaulizwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na shughuli nyingine za kibailojia, Otherwise CHIT CHAT MUCH FUN MUCH LOVE..!!

Thanx broo! Tuko pamoja!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ada ya usajili ni 300,000 caution money 100,000 chit chat ID 300,000 fedha hizi ziwasilishwe kwangu haraka kwani nafasi ni chache.Naku pm for bank details

Duhh! Hapo pagumu!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kama ni ME,
Mwambieni aje kwangu akaguliwe na Mwanadada, Mdafada, Mwanamke Rijali Madame B.

Ila kama ni KE,
Babu Asprin anamuhusu.

Madame B, nitakutafuta kwa ukaguzi, nipe tu maelekezo !

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kama ni ME,
Mwambieni aje kwangu akaguliwe na Mwanadada, Mdafada, Mwanamke Rijali Madame B.

Ila kama ni KE,
Babu Asprin anamuhusu.
Ewaaaaaaaa!! Waambie kabisa tulishakaguana na kupeana setifiketi ya ukaguzi baada ya kufanyiana ukaguzi wenyewe na kujipasisha kuwa tunafaa kuwakagua wa kukaguliwa.
 
Karibu! Ila sehemu ya utambulisho rasmi nenda jukwaa la siasa kule ndio wageni wanapokelewa.

Kule kuna stress za kutosha anaweza kujikuta bado mgeni akalamba ban! Chezeiya mods wewe
 
Back
Top Bottom