Nauchunguza huu mchoro, naona ulikuwa na nia ya kuwakoga Wabunge ili waipitishe bajeti ya Magufuli bila vikwazo - wakiwa wamepatwa na mchecheto wa picha! Poor strategy bwana Magufuli.
Pia naona kama mchoro uko feki sana. Kwanza, hizo barabara zilizotengeneza kama U kulia na kushoto, ni kwa ajili ya nini? Na kwa nini zina kona? Iweje mtu anae -drive kutoka kulia kwenda kushoto apige kona kali kama hivyo? Kwa nini kwenye interchange umwekee kona mtu ambaye anakwenda moja kwa moja?
Pili, sioni mtu ambaye anatoka juu kaskazini atakavyoingia kwenye barabara kwenda kulia au kushoto. Na pia wale wanaotoka kulia au kushoto, wanaingiaje kwenye freeway inayokwenda juu na chini kulia na kaskazini? Nikiangalia pembeni mwa kulia na kushoto naona service roads, lakini sioni jinsi gani barabara za kuia na kushoto zimeunganishwa na ile ya kwenda juu na chini, kaskazini na kusini.
Nadhani kuna mtu kafanya ku copy na ku paste wakampa Magufuli, na kwa kuwa Magufuri ni nguini akaona inapendeza aiweke kama cover picture kwenye bajeti yake!
Labda kuna details zimejificha, lakini sidhani. Magufuli, nadhani watu wako wamekuingiza mjini!