Muonekano wa barabara ya Ubungo baada ya marekebisho

Muonekano wa barabara ya Ubungo baada ya marekebisho

Hapo ni kuhamishia foleni sehemu ingine...waje na suluhisho la kudumu..
 
ndoto hii ni sawa na ndoto ya membe kwenda ikulu haitakuja kutokea leo
 
Duh utasubiri sana ndugu yangu.
Masuala ya maendeleo yanataka mikakati endelevu na inayotekelezeka siyo siasa na sanaa.
Tumeshindwa kurudishia mifuniko ya chemba za barabarani iliyoibiwa na wajasiriamali wa vyuma chakavu ndiyo tutajenga barabara za juu ? Barabara za lami zinaharibika kabla ya kukabidhiwa na mkandarasi , hii ndiyo TZ bhana
 
Watanzania mnapenda pepo ya kufikirika... Picha tu yawachanganya...
 
Mitaro tu pembeni ya barabara inatushinda kujenga...sembuse hizo barabara za juu...

Tutasubiri sana...
 
Huyu magufuli uishetu utawala huu aondoke, wanangangania kujenga barabara zisizo na maana kilomita 100 zinazopitisha magari manne kwa siku wakati dar watu wanalala barabarani kwa foleni, kwanini wasingerekebisha miundombinu ya dar?
 
Dr. Magufuli alisema Bungeni wakati wa hotuba yake kuwa pale Ubungo mataa kutakua na barabara za juu tatu kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Kama hili likitekelezeka na ile ya Chalinze ambayo itakua na barabara za juu tano nadhani tutakua tumejitahidi kiasi flani kupunguza foleni.

Hongera Magufuli naombea ndio uwe Rais wetu ili haya yatimie.

View attachment 255467

Story za vijiweni kuombea kura,
Usiwaamini sana wanasiasa
 
hapo ndio utajua jinsi gani nchi hii huwa na mipango ya miaka 5 tuu.. sasa hizo fly over na mitambo ya gesi ile itakuwaje...hivi kiuhalisia ile nafasi pale inatosha kweli?
 
Watanzania baada ya kujua kubonyeza laptop zao Na kutumia design software imekuwa inshu nzito, Mtu anachorachora anatupia mtandaoni..!

Barabara hiyo unajua itahitaji square metre Ngapi?au mnachora tu.. Kwa Haraka nikiangalia UPANDE mmoja tu say ubungo -Kimara naona barabara 18. Kila moja Kama Ina 4m hapo tunapata Mita 72, Ukiangalia kuna maeneo nyasi ukubwa wake Ni Sawa Na barabara. Hapo kuna 72'm this is 144m heka 2 au uwanja wa mpira Na Nusu. Wapi eneo Hilo Ubungo?
 
Nadhani hizo ni siasa tu, si walisema wanataka kutengeneza barabara kutoka dara hadi Zenji kupitia baharini wakati ya tandale uzuri yenyewe imewashinda!
 
Hii ndoto labda wataweza weka flyover ya njia mbili zikutane msalaba hivi yaani barabara moja juu ingine chini (+)lakini kuwepo hizo lane 2juu na chini iwepo lane nyingine kibongobongo haitakua!maana hizo barabara zitakazozidi zitaelekea wapi?hiyo intercection ni barabara kwenda Mwenge,buguruni,Posta na Kimara kwisha
 
Back
Top Bottom