SI KWELI Muombeeni Samia hali yake ya afya ni mbaya sana

SI KWELI Muombeeni Samia hali yake ya afya ni mbaya sana

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
MAKONDA.jpeg
 
Tunachokijua
Tunachokijua

Paul Christian Makonda
anahudumu kama Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania na pia ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini.

Madai

Kumekuwepo na nukuu inayosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, ikidaiwa kutolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ikieleza kuwa hali ya afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, si nzuri.

Chapisho hilo linamnukuu Makonda akisema: “Ndugu zangu Watanzania, tumuombee Rais Dkt. Samia, kwa sasa hali yake mbaya sana”

Uhalisia

Hata hivyo, ufuatiliaji wa taarifa hiyo kwa kutumia maneno muhimu haujabaini ushahidi wa kuaminika unaothibitisha kuwa Waziri Makonda alitoa kauli hiyo kama inavyodaiwa kwenye chapisho hilo.

Aidha, katika taarifa zilizopatikana kupitia vyanzo rasmi vya serikali, ikiwemo tovuti ya Idara ya Habari-MAELEZO na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, hakuna uthibitisho uliopatikana unaohusisha nukuu hiyo na Waziri Makonda.
Back
Top Bottom