kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,705
- 17,188
Linaonekana kama swali la kipumbavu kwa wasomaji lakini mimi linanifikirisha sana usiku na mchana na sipati majibu.
Mafanikio ya maisha niliyonayo mimi ni makubwa na hayalingani kabisa na nguvu, muda na mali ninayompatia Mungu wangu mimi. Mimi huwa ninamwamini sana (100%) kuwa anayaweza yote na atanifanyia yote na kumshuru kwa kila jambo linanonikuta basi, sifanyi kitu kingine chochote zaidi ya hapo.
Lakini, Wako watu ambao maisha yao yote, nguvu zao zote, muda wao wote na rasilimali zao nyingi wanazitumia kwa Mungu wao. Wanakesha kwenye nyumba za ibada wakiomba, kusali na kuswali, wanafunga, wanatoa sadaka na zaka, wanaimba, wanahudhuria mahubiri mengi tu, wanaombewa, wanakanyaga mafuta, wanachangia ujenzi wa nyumba za ibada, wanantunza wakuu wa dini, nk; lakini mafanikio yao kwenye maisha ya kawaida hayanizidi, ni kama yangu, ninawazidi kwa mbali au maisha yao ni mabaya zaidi.
Mimi sina ugomvi na majirani zangu, tunasaidiana, silali na njaa, watoto wanakwenda shule na kutibiwa, wazazi wanafurahia uwepo wangu, mke wangu hana tabu na mimi, pakulala tunapo, usafiri upo, nk. namshukuru Mungu wangu kila siku.
Kwani kuna miungu wengi?
Kila mtu ana Mungu wake?
Mungu wako anakutaka umfanyie nini?
Mungu wako ana sifa zipi?
Au kuna vitu zaidi ya MwenyeziMungu kwenye maisha?