Mungu na Shetan wanapopiga story!!

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,854
1,128
Wadau nafikiri wengi tinaifahamu hadithi ya kuhusu Ayubu na yanayoitwa majaribu!!

Katika hicho kitabu (Ayoub 1; 7) Mungu anamuuliza shetani "umetoka wapi?" Shetani anajibu "nimetoka duniani katika kutembea huku na huko"(bado sijajua mahali walipokutana), Hawa wawili wanaendelea kubadilishana mawazo...huku Mungu akimsifu Ayubu huku naye shetani akidai kwamba Ayubu kabarikiwa na kuzingirwa na nguvu za mungu!!

Mwisho wanakubaliana kwamba shetani akamjaribu Ayubu ila wamwachie roho yake tu!!

Maswali yangu!!

Je Mungu na shetani ni marafiki kiasi cha kukaa na kupanga mipango jinsi ya kumjaribu Ayubu, Kuna mahali nimewahi soma ikidaiwa shetani alitupwa duniana, sasa pale anaposema nimetoka duniani ni wapi huko walikokutana!??

Je kuna haja ya kupiga kelele makanisani za "Shetan toka" ikiwa wao wanakakaa na kupiga story na pia kupanga mikakati??
 
Siyo tu kwa Ayubu hata Yesu ..Mathayo 4:1-11. Kwenye mstari wa 10; Yesu alimfukuzia mbali shetani, kama ambavyo hufanyika makanisani....
 
Hii ni ngumu kumesa...japo wapo wanataalam wataelezea...lakin tafsir yenye maana nionavyo mimi ni kwamba waaandishi walikuwa wanaandika kwaa ajili ya watu wa zama zao...na pengine ni zao la mahubiri ya kufikirika..
 
haina maana kama ilivyo andikwa. hiyo ya Ayubu pamoja na ya Yesu inamaanisha dhamiri binafsi ya mhusika, yaani anajiuliza je amfuate mungu au shetani?
 
Wadau nafikiri wengi tinaifahamu hadithi ya kuhusu Ayubu na yanayoitwa majaribu!!

Katika hicho kitabu (Ayoub 1; 7) Mungu anamuuliza shetani "umetoka wapi?" Shetani anajibu "nimetoka duniani katika kutembea huku na huko"(bado sijajua mahali walipokutana), Hawa wawili wanaendelea kubadilishana mawazo...huku Mungu akimsifu Ayubu huku naye shetani akidai kwamba Ayubu kabarikiwa na kuzingirwa na nguvu za mungu!!

Mwisho wanakubaliana kwamba shetani akamjaribu Ayubu ila wamwachie roho yake tu!!

Maswali yangu!!

Je Mungu na shetani ni marafiki kiasi cha kukaa na kupanga mipango jinsi ya kumjaribu Ayubu, Kuna mahali nimewahi soma ikidaiwa shetani alitupwa duniana, sasa pale anaposema nimetoka duniani ni wapi huko walikokutana!??

Je kuna haja ya kupiga kelele makanisani za "Shetan toka" ikiwa wao wanakakaa na kupiga story na pia kupanga mikakati??
 
Wadau nafikiri wengi tinaifahamu hadithi ya kuhusu Ayubu na yanayoitwa majaribu!!

Katika hicho kitabu (Ayoub 1; 7) Mungu anamuuliza shetani "umetoka wapi?" Shetani anajibu "nimetoka duniani katika kutembea huku na huko"(bado sijajua mahali walipokutana), Hawa wawili wanaendelea kubadilishana mawazo...huku Mungu akimsifu Ayubu huku naye shetani akidai kwamba Ayubu kabarikiwa na kuzingirwa na nguvu za mungu!!

Mwisho wanakubaliana kwamba shetani akamjaribu Ayubu ila wamwachie roho yake tu!!

Maswali yangu!!

Je Mungu na shetani ni marafiki kiasi cha kukaa na kupanga mipango jinsi ya kumjaribu Ayubu, Kuna mahali nimewahi soma ikidaiwa shetani alitupwa duniana, sasa pale anaposema nimetoka duniani ni wapi huko walikokutana!??

Je kuna haja ya kupiga kelele makanisani za "Shetan toka" ikiwa wao wanakakaa na kupiga story na pia kupanga mikakati??

biblia inapingana,fuata imani yako asee!!!
 
wenye uwezo wao sasa wakaseme na roho mtakatifu awape majibu waje watuambie na sisi humu jf...
 
Mtoa mada,fahamu kuwa Mungu na Shetani ni roho na siyo mwili kama sisi.Ndiyo maana tunaomba(tunaongea na Mungu) bila kuonana au kukutana.
 
Mawasiliano yao hufanyika wakati wowote bila msaada wa simu kama sisi.Hivyo Roho hutambua hata fikra zako kabla hujawaza.swala la shetani kuongea na Mungu si ajabu maana roho zinaonana na kuwasiliana mda wote.
 
Kuna siri hapa wengi hawazijui ... Nitakuja kuelezea.

1. Kuna kitu tunaita "Bunge la mbinguni" na shetani anaruhusiwa kuingia kama mshitaki/accuser.
2. Siri nyingine ambayo wengi hawaifahamu ni kuhusu majaribu/mateso. Kuwa Mungu hapendi kuwatesa wanadamu bali humruhusu shetani kufanya hivyo kwa sababu ya Attribute yake mojawapo, "Huruma/compassion."

Labda niseme hivi; shetani alikuwa miongoni mwa malaika wakuu. Na aliitwa "lucifer."

Na habari zake zimeandikwa kwa kina katika kitabu cha EZEKIELI 28 & ISAYA 14. Nitasummarize tu;

Katika aya ya EZEKIELI 28, inaeleza kuwa shetani alikuwa amejaa hekima na alikuwa mzuri kupitiliza. Alikuwa kiumbe mzuri mwenye hekima na akili (maarifa) kuliko wote ambao Mungu aliwaumba, mara elfu zaidi kuliko wanadamu na ndio maana aweza kuwadanganya kwa urahisi sana.

Sifa za shetani kabla ya kufanya dhambi/uasi ni;

1. Alivaa vizuri sana.
2. Aliumbwa na Mungu kama malaika na viumbe wengine (mfano mwanadamu)
3. Nafasi yake katika mbingu ilikuwa chini tu ya Mungu mwenyewe akiwa malaika mkuu “Arch-Angel” pamoja na Mikaeli-malaika wa vita. Yeye shetani aliitwa Lucifer-Inavyosemekana alikuwa malaika wa sifa na kuabudu (ibada), sehemu muhimu zaidi katika ufalme wa Mungu japokuwa biblia haijalielezea hili kwa uwazi.
4. Aliruhusiwa kutembea katikati ya mawe ya moto (katika chumba na kiti cha utukufu na enzi cha Mungu, alitembelea ulimwengu wote, mlima mtakatifu wa Mungu, na katika uwepo wa Mungu mwenyewe)
5. Mungu aliumba malaika mkamilifu na mtakatifu ambaye kwa sababu zake akabadilika na kuwa mwovu na ibilisi, hivyo Mungu hakumwumba ibilisi/malaika aliyeasi, ila aliumba malaika aliyekuwa mkamilifu na mtakatifu.

Katika ISAYA 14, inasema maana ya Lucifer ni "nyota ing'aayo sana" Uzuri wake ulikuwa mkubwa.

Katika EZEKIELI 28:15 inatuambia vitu ambavyo vilimpelekea Lucifer kuwa shetani;

1. Alikuwa na kiu ya kuwa na nguvu kuliko Mungu mwenyewe aliyemuumba (desire to have greater power)
2. Alijiona kuwa na utajiri mkubwa(wealth)
3. Alijisikia hadhi kuu, fahari na heshima kuu(prestige)
4. Alikuwa mroho/mlafi na alikuwa na majivuno(self centered, greed and pride).

1 YOHANA 3:4“Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.”

Alianza kujivunia uzuri na akili zake (beauty&intelligence), na akaanzisha propaganda kule mbinguni ambazo baadaye alizieneza ulimwenguni mwote.

Siku moja, nitawaeleza kwa nini Mungu hakumwangamiza shetani baada ya uasi, na badala yake alimpa nafasi ya kuwa adui wa wanadamu.

Angalia maandiko haya chini;

UFUNUO WA YOHANA 12:12 “…ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”

Kwa nini? Kwa sababu, “Anajua ataangamizwa kwa moto” - EZEKIELI 28:18

1 PETRO 5:8 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa maana mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.”

Kwa hiyo shetani anaruhusiwa kuwa mshtaki wa wanadamu & anaruhusiwa kuingia katika Bunge la mbinguni. Angalia hapa chini;

2 MAMBO YA NYAKATI 18:18-21 “18 Mikaya akasema, Sikieni basi neno la Bwana; Nalimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi na jeshi lote la mbinguni wamesimama mkono wake wa kuume na wa kushoto.19 BWANA akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramoth-gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 20. Akatoka pepo, akasimama mbele za BWANA, akasema, Mimi nitamdanganya, BWANA akamwambia, Jinsi gani? 21Akasema, Nitaondoka,na kuwa, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wote.Akasema, Utamdanganya, na kuduriki pia; ondoka, ukafanye hivyo.”

Kwa hiyo anachokifanya ni kuwadanganya watu, kwa sababu ya maarifa yake. YESU anatuonya katika MATHAYO 24 kuwa "Adui mkubwa wa wanadamu atakuwa uongo."

UFUNUO WA YOHANA 12:7-9 “7 Kulikuwa na vita mbinguni;Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka, Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa , Yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye ibilisi na shetani, audanganye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”

1 MAMBO YA NYAKATI 21:1,7 “Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.7Neno hilo likawa baya machoni pa Mungu; kwa hiyo akawapiga Israeli.”

AYUBU, ni mfano wa watu waliodanganywa na adui ili wakumkufuru ama kumwasi Mungu. AYUBU NI MFANO WA WATU WALIOMSHINDA SHETANI.

ADAMU NA MKEWE, waliingia katika mtego huo lakini tunalo tumaini katika KRISTO YESU. Tunazo nguvu kupitia YESU za kumshinda shetani (Luka 10).

Maandiko yanasema;

YAKOBO 4:7-8 “7 Basi mtiini Mungu, Mpingeni shetani, naye atawakimbia. 8Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia…”

1 PETRO 5:9 “Nanyi mpingeni huyo mkiwa thabiti katika imani…”
“Resist him, Steadfast in faith.”

WAEFESO 6:12,13 “Vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kuweza kuzipinga hila za shetani.”

Nina mengi ya kuelezea, kwa leo naomba nikomee hapa. Mungu na azidi kutupigania.
 
Last edited by a moderator:
Mimi mkristo ila nasoma pia Quran sana kujua ukweli,biblia na Quran zote zatoka kwa MUNGU MKUU na ndio maana mamlaka ya MUNGU MKUUhayaojiwiii kbsaa,Quran inasema hao malaika hawajawia kumuona MUNGU MKUU kbsa pia ata biblia nayo inasema kuwa Siku ya mwisho anaoijua ni MUNGU MKUU nadhani ili tusipate matatizo tumuachie mola
 
Back
Top Bottom