Mimi siyo msomaji mzuri wa biblia. Na pia sioni fahari kutokuwa msomaji mzuri wa hiyo biblia. Pamoja na yote hayo hii hoja iliyoletwa hapa binafsi naona ni moja ya maswali ambayo kibinadamu katika udhaifu wake (ambao kimsingi mimi naona ndiyo ukamilifu wake) tunaweza kujiuliza. Katika kuchangia kwenye swali hili pengine tuanze kwa kujiuliza na kukubaliana kwamba sisi binadamu na shetani kwa pamoja tumeumbwa na Mungu huyo huyo au la? Naamini wengi tutakubaliana kwamba sote ni wana wa Mungu. Na je sisi binadamu katika maisha yetu hatujapata kutenda dhambi tena kubwa kabisa lakini bado tukawa "tunapiga stori" na Mungu (kupitia roho mtakatifu) na hata huyo Mungu akatusaidia katika mambo yetu mengi pamoja na dhambi zetu chafu zinazokuwa zimetuzunguka? Kwa maana hiyo sishangai kuona kuwa Mungu na kiumbe chake shetani waliweza kuonana na "kupiga stori" kwani pamoja na dhambi zake mbaya kabisa huyo shetani bado ni kiumbe chake Mungu. Leo hii ikitokea mwanangu (damu yangu) akanikosea kwa kutenda kosa lolote kubwa kwangu, hata kama nitamfukuza asiishi kwangu siku ikitokea nikakutana nae baada ya miaka mingi sitaacha kumsalimia na hata kumuuliza anakoishi muda huo. Na hapo mimi ni mwanadamu tu mwenye upendo unaopimika hata kwa kibaba. Tofauti na Mungu ambaye upendo wake na pia hasira zake havina kipimo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.