Mungu Mlinde Dr. Slaa Aiokoe Tanzania

Mungu Mlinde Dr. Slaa Aiokoe Tanzania

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
Nimekuwa mwana CCM maisha yangu yote. Nakiri kwamba chama changu kimeleta umasikini na matatizo ya kutisha kwa Watanzania. CCM imekuwa ni hatari kuliko hata Ukimwi, kwani inawaua na kuwatesa raia wake bila huruma. CCM na serikali yake inatumia Polisi kungoa watu kucha bila ganzi. Wokovu tulionao leo, ni Dr Slaa au Mwakyembe. Katika dhoruba tuliyonayo ndani ya CCM, Dr. Mwakyembe hana ujanja kuweza kuliongoza nchi. Nyangumi ndani ya CCM watammeza. Tafadhalini watanzania wapenda amani. Tushirikiane, kuakikisha Dr. Slaa tunamlinda asidhuriwe na CCM.
 
ni wazo zuri hata mimi ni mwana CCM tangu mwaka 1983 lakini sasa mhuuuuu.... sina hamu.
 
mungu liepushe taifa hili na watembea na sumu, wauwaji na wateka watu...mungu nakemea watembea na sumu hadi bar kwa jina lako ee muumba wa mbingu na ardhi..aaaimen
 
Mi naona kama unamtegemea Slaa basi unamahaba naye makubwa sana na huyu mtu. Sasa sijui kama unafuatilia ilani ya chama na kama ungefuatilia basi ungetakiwa kuona matumaini kupitia sera za chama na sio mtu.
 
Nimekuwa mwana CCM maisha yangu yote. Nakiri kwamba chama changu kimeleta umasikini na matatizo ya kutisha kwa Watanzania. CCM imekuwa ni hatari kuliko hata Ukimwi, kwani inawaua na kuwatesa raia wake bila huruma. CCM na serikali yake inatumia Polisi kungoa watu kucha bila ganzi. Wokovu tulionao leo, ni Dr Slaa au Mwakyembe. Katika dhoruba tuliyonayo ndani ya CCM, Dr. Mwakyembe hana ujanja kuweza kuliongoza nchi. Nyangumi ndani ya CCM watammeza. Tafadhalini watanzania wapenda amani. Tushirikiane, kuakikisha Dr. Slaa tunamlinda asidhuriwe na CCM.

kwa hiyo unataka tujadili dr slaa vs mwakyembe au una maana gani
 
Da amakweli dunia imejaa wendawazimu,walio na akili zao wa kuhesabu,tangu lini simba jike amezaa mbuzi? Dr slaa ni mwanasiasa wa Tanzania,mwenye fikira za Kitanzania,hanajipya na haitatokea akawa na jipya.Inawezekana tunatumia hisia kumuona anafaa kuliko uhalisia.Na pia sisi tumekuwa washabiki wa wanasiasa badala ya kuwa wenyenchi.Na inawezekana pia hatuna vigezo vya kupima uwezo na weledi wa wanasiasa wetu tunaishia kushabikia muonekano wa nje wa watu badala ya ukweli kuhusu wao.Kila mmoja wetu afikiri mwenyewe asimpe mtu fursa ya kufikiri kwa niaba yako hatari hiyo.Fikiri peke yako,wewe mawazo uliyo nayo yako au ya kupewa? na kwanini na mpaka lini.Tafakari
 
dr slaa hana uwezo wa kuongoza. ameshindwa kuongoza kanisa, akashindwa kuongoza familia mpaka katelekeza mke kwa sababu ya josephine (sijui atajibu nini kwa Mungu) na kashindwa kuongoza chadema. ataweza nchi?
 
CCM imelaaniwa duniani hadi mbinguni na anayeichagua CCM pia amelaaniwa.

haya matusi unatukana humu tu jf au hata ukiwa nyumbani kwenu unafanya hivyo,hongela endeleza matusi yatakusaidia yawezekana utanenepa kwa kutukana big up.
 
safi kabisa mkuu mungu yu pamoja nae milele amina
 
Mungu epusha taifa hili na ndoto ya dr slaa kuingia ikulu huku akivitukana vyombo vyote vya dola, polisi, jwtz hadi usalama wa taifa
 
safi kabisa mkuu mungu yu pamoja nae milele amina

unafikiri dr slaa atabaki milele? ona ile mimvi, au kwa vile kapora mke juzi unafikiri ataendelea kuwa naye
 
kila mtu anauhuru wa kutoa maoni yake lakini mawazo mengine kiboko kwamba slaa ndiye mwokozi wa tanzani hapana hivyo vigezo hana kwa zile hasira zake atauwa watu.
 
Not to be a Red comrade or anything.

Mentality nzima ya "Mungu Mlinde Dr. Slaa Aiokoe Tanzania" ina matatizo lukuki, neno kwa neno.

Ukianza kwa mungu tu una deal na a hoax. Mungu hayupo. Kwa hiyo habari nzima ya mungu kutoa ulinzi ni ushairi shayiri tu.

Tanzania ina umaskini mkubwa kwa sababu ya kukataa uchunguzi na kwenda na imani imani tu, mojawapo ya msingi kabisa inayotufanya tuwe masikini ni hii ya mungu.

Watu wanaoamini kuwapo kwa mungu ni rahisi zaidi kukubali kuwa katika utawala dhalili usioheshimu haki za msingi za binadamu, kuliko wale ambao hawaamini kuwapo kwa mungu. Mungu analeta excuses kibao za kukubali udhalili. Kuanzia "utapewa malipo peponi" mpaka "watiini watawala maana wamewekwa na mungu".

Kwa hiyo kama unataka Tanzania iendelee ondoa habari za mungu katika mawazo kwanza. Mungu ni tatizo Tanzania, si suluhisho.

Mlinde? Of course kama mungu hayupo hawezi kumlinda, lakini hata kama angekuwapo. Asipomlinda - short of against death- na kumpa majaribu zaidi ndo tutamjua kama ni kiongozi bora au anaelea kwa sababu ya hali nzuri tu. Ayubu hakuthibitisha imani yake na uthabiti kwa kulindwa na mungu, alithibitisha hayo kwa kutolindwa na mungu.

Aiokoe? Kwa nini Tanzania itake mtu wa kuiokoa? Huyu Dr. Slaa ni nani mpaka aiokoe Tanzania? Yeye ni Masiha au Mahdi gani huyu?

Uongozi wetu hauhitaji charismatic figures wa kutuokoa, hatuhitaji top down leadership. Hii ina introduce a single point of failure. We have been there, done that, bought the T-Shirt to show. It is written "Nyerere, baba wa Taifa" aka Mchonga aka Haambiliki.

Kwa nini tutake strongman mwingine badala ya kutaka a grassroots empowerment? Kwa nini tusitake ushirikishwaji wa umma zaidi? Kwa nini tusitake wabunge machachari zaidi wanaohuishwa na jumuiya thabiti zenye uelewa wa mamabo zaidi?
 
atubu kwanza dhambi zake za kutelekeza familia, kupora mke wa mtu, kuvunja ndoa ya mtu, na kuasi kanisa ndipo umpe hizo sifa
 
Back
Top Bottom