Mungu, kwanini umeyaruhusu haya?

Mungu, kwanini umeyaruhusu haya?

Kwanini umeyaruhusu bwana, kwanini umeyaruhusu?
Yatusononeshe moyoni, bwana, kwanini umeyaruhusu?

Kwanini Mungu amekubali Magufuli awe rais ilihali anajua hatakimudu hicho cheo?

Bwana, kwanini umeyaruhusu?
Kwanini umeruhusu Magufuli atangazwe rais na sio Lowasa, kwanini umeyaruhusu?

Mungu, Tanzania inateseka, uhuru wa kujieleza unakufa, udikteta unashamiri, Mungu Kwanini umeyaruhusu?

Kwanini vijana wanateseka, ajira hazipo, uchumi umekwama, nchi inateseka, watesi wanashinda, Magufuli anashinda, nia njema inashindwa, baba, kwanini umeyaruhusu?

Baba unajua roho zetu, baba unajua tulivyoumia, baba fanya jambo.
NA MUNGU ULIYE JUU TUANDAE KWA YANAYOKUJA, BABA TUTAPAMBANA KAMA UKITAKA, TUTASHINDA KAMA UKITAKA, TUTASHINDWA UKITUACHA.
Chuki za Kichaga!
 
Hizi ni siasa tu. Acha kabisa kumtaja Mungu kwenye sala zako za kijinga. Wewe mwenyewe umechagua upande wa siasa halafu unakaa unaanza kujiaminisha kabisa kuwa Mungu naye amechagua upande wako wewe. Yaani wewe unajua kuwa mko naye! Bro kama sio upuuzi huo ni nini?
 
Angalau nna uhakika Mungu hapendi watu wake wateseke.
 
Kwanini umeyaruhusu bwana, kwanini umeyaruhusu?
Yatusononeshe moyoni, bwana, kwanini umeyaruhusu?

Kwanini Mungu amekubali Magufuli awe rais ilihali anajua hatakimudu hicho cheo?

Bwana, kwanini umeyaruhusu?
Kwanini umeruhusu Magufuli atangazwe rais na sio Lowasa, kwanini umeyaruhusu?

Mungu, Tanzania inateseka, uhuru wa kujieleza unakufa, udikteta unashamiri, Mungu Kwanini umeyaruhusu?

Kwanini vijana wanateseka, ajira hazipo, uchumi umekwama, nchi inateseka, watesi wanashinda, Magufuli anashinda, nia njema inashindwa, baba, kwanini umeyaruhusu?

Baba unajua roho zetu, baba unajua tulivyoumia, baba fanya jambo.
NA MUNGU ULIYE JUU TUANDAE KWA YANAYOKUJA, BABA TUTAPAMBANA KAMA UKITAKA, TUTASHINDA KAMA UKITAKA, TUTASHINDWA UKITUACHA.
Ungeanza kumuuliza kwanza kwann aliruhusu wakoloni kututawala waafrika then ndo ungemuuliza kuhusu huyo unaemuuliza!

Mungu hasaidiwi kazi anajua anachokifanya.

Nikuulize swali,
kama mambo yangekuwa kama unavyotaka ni lini ungemkumbuka Mungu?

Shida hutuleta karibu zaidi ya Mungu.
Acha huyo unaelalama kwann ameruhusiwa atusongeze Karibu zaidi na Mungu.
Endelea kuomba!
 
Mungu kuna mda anampa mtu kitu ht km hafai ili azidi kuteketea
 
Kama taifa tumepata laana ya kihalaiki kwa kumkubali Magufuli atuongoze
Hiyo laana umepata wewe na wenzio ambao mmeletewa mtu wa kuwakomboa nyie hamtaki mnaanza kumlaumu na kumuuliza maswali ya kijinga yule aliye waleteeni mkombozi. Naona laana km waliyo ipata waisrael jangwani ikirudia kwenu. Wale walikuwa wanamlaumu Mussa kwanini Mungu amewatoa utumwani waende kuteseka jangwani wakati huo chakula kinashuka toka mbinguni wanakula bila kufanya kazi.
 
Ungeanza kumuuliza kwanza kwann aliruhusu wakoloni kututawala waafrika then ndo ungemuuliza kuhusu huyo unaemuuliza!

Mungu hasaidiwi kazi anajua anachokifanya.

Nikuulize swali,
kama mambo yangekuwa kama unavyotaka ni lini ungemkumbuka Mungu?

Shida hutuleta karibu zaidi ya Mungu.
Acha huyo unaelalama kwann ameruhusiwa atusongeze Karibu zaidi na Mungu.
Endelea kuomba!
Viongozi wa dini watusogeze karibu na Mungu.
Rais atuletee maendeleo.
Kuna maana gani ya kuwa na rais wakati mtaani fedha haionekani?
Kuna maana gani ya kuwa na rais wakati vijana hawana ajira ?
Tanzania can do a lot better without the president.
 
Hiyo laana umepata wewe na wenzio ambao mmeletewa mtu wa kuwakomboa nyie hamtaki mnaanza kumlaumu na kumuuliza maswali ya kijinga yule aliye waleteeni mkombozi. Naona laana km waliyo ipata waisrael jangwani ikirudia kwenu. Wale walikuwa wanamlaumu Mussa kwanini Mungu amewatoa utumwani waende kuteseka jangwani wakati huo chakula kinashuka toka mbinguni wanakula bila kufanya kazi.
Naomba ushahidi kwamba tumeletewa mtu wa kutukomboa ( naomba hata ushahidi wa uongo kama unao )
 
Imeandikwa
...Mungu akasema nataka nifanye jambo,ambalo kwa kila atakaye sikia masikio yake yatamuwasha....
Mungu huwa anaghairi sababu DHAMBI zimezidi.
 
Na Mambo anayofanya na kusema mkuu ukiyasikia masikio yanawasha
 
Naomba ushahidi kwamba tumeletewa mtu wa kutukomboa ( naomba hata ushahidi wa uongo kama unao )
Kwani wewe hujasikia habari za yule alietembelea Muhimbili kisha wagonjwa wanalala vitandani?
Hujasikia habari ya yule mtu ambae neno lake tu watoto wa masikini wanasoma bure hadi kidato cha sita?
Huja sikia habari za yule ambae mngurumo wake tu sasa watu wanapata huduma kwa wakati ktk taasisi za umma?
Hujasikia habari zake yule ambae kwa ukali wake tu meli zinazokuja kushusha mizigo bandarini sasa taarifa zake hazipotei kimaajabu?
Hujasikia habari za miujiza ya yule mwana wa Chato ambae kwa ushupavu wake Shirika la ATC sasa lina ndege zaidi ya moja?
Hujasikia maajabu mengine mengi ya kutukomboa toka ktk rushwa na umasikini wa kutisha?
Huu ndio ukombozi ambao ulikuwa unasubiriwa...unaweza kujazia mengine mengi.
 
Jaman MUNGU atusaidie na atupe wepesi,nchi imevamiwa.
 
Back
Top Bottom