Mungu kamwe hawachagulii wanadamu kiongozi

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
Hivyo katika kipindi hichi cha uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani,hatunabudi kufanya mambo yafuatayo ili kuweza Kumpata kiongozi bora tunayemtaka:-

1)Katika daftari la kupiga kura,Serikali wanatakiwa watoe elimu ya uraia wananchi wajue umuhumu wa kupiga kura na ni haki yao kikatiba

2)Tume ya Uchaguzi haina budi kuhakikisha Uchaguzi wa mwaka huu unakuwa Huru na wa Haki bila kupendelea Chama chochote Ndipo Tutaweza kuona Amani ikiendelea kutawala Amani na Haki ni marafiki wakubwa wamebusiana Tume ya Uchaguzi/watawala watende haki amani utaiona.

3)Kuhakikisha kila aliyejiandikisha katika daftali la kupiga kura ajitokeze siku ya uchaguzi 25 october 2015 Kutimiza wajibu wake wa kumchagua Kiongozi anayemtaka!!!!

Vinginevyo kama unaishia kuongea sana mitaani na wengine kulia sana kumuomba Mungu bila kujitokeza kupiga Kura,ukidhani MUNGU Ndiye atakuchagulia kiongozi utajidanganya!!!!Jukumu hilo lipo mikononi mwetu hivyo hata kama kweli ulionyeshwa au kufunuliwa fulani ndiye rais ,jambo hilo hata kama Mungu alikusudia hivyo,linaweza kabisa lisitimie Maana IMANI BILA MATENDO IMEKUFA!Tena Mungu hufanya kazi na wanadamu katika kulitimiza kusudi lake!!!!Sasa kama wewe hujitokezi litatimiaje?

4)Kuachana na dhana hii potofu kudhani kuwa rais au mbunge tunachaguliwa na Mungu.
Mungu amewapa uhuru wanadamu kuchagua viongozi wa kuwatawala.Mungu kamwe hawachagulii wanadamu kiongozi bali huwaacha wachague wenyewe.Tukiacha kwenda kupiga kura tunaweza kupata kiongozi mbovu na hata kama tukiomba juu ya kiongozi huyo mbovu kamwe Mungu hatajibu maombi yetu

5)Tuachane na mawazo potofu kuwa kuwa kura moja haina athari,hofu ya kuibiwa kura hivyo kuacha kushiriki kupiga kura.Tuachane na mawazo haya kwani kwa sheria za Tanzania mgombea anatangazwa kwa wingi wa kura.Hivyo tuachane na msimamo wa kutokujitokeza kwa kuona kura yako haina thamani

6)Tusichague viongozi kwa vigezo vya Biblia au uumini wao bali tuangalie uwezo wao wa utendaji katika kusimamia misingi ya katiba.
"Kwenye uchaguzi mkuu hatuchagui malaika wa kutupeleka mbinguni bali kiongozi wa kuliongoza taifa.Hivyo tuwe makini kwenye kuchagua sifa ya mtu tusipime kwa mambo binafsi au wa dini gani atuchagui kiongozi wa kutujengea makanisa au Misikiti wala siyo wakutuongoza kwenda mbinguni bali wa kututoa kwenye umasikini tulionao.


Hivyo kuyazingatia hayoyote tunaweza Kupata kiongozi bora wa kutuletea maendeleo ambaye tumemchagua sisi wenyewe Sio Mungu.
Mtu asilete porojo kwamba tumchague huyu ni chaguo Mungu,Mungu hatuchangulii viongozi hata mke sembuse kiongozi!!

 
Kufuru dhidi ya mungu hazitakiwi kijana!mungu ndiye ajuae raisi wa tanzania 2015 tokea enzi.unaweza kuandika kitu kwa "nia njema"ila kwa kutojua au kujua ukawa umemkufuru mungu.unapoandika neno "mungu"jifikirie mara mbili mbili.
 
Labda 'mungu' unayemuamini wewe, ila Mungu ninayemuamini mimi anachagua viongozi wa taifa. Mfano mzuri ni Musa na Daudi walichaguliwa na Mungu
 
Ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu. Serikali zote zinazochaguliwa kwa mifumo ya kibinadamu hazina baraka ya Mungu
 
Back
Top Bottom