Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 260
- 712
Usiku wa manane barabarani wamelala wima lakini mikono inataka shilling na mili yao ipo tayari kwa ajili ya kazi, si imeendikwa Mwanaume atakula kwa jasho? Sasa wanafanya kutimiza maandiko.
Usiku mwingi watambeba abiria wasio wajua na wakati mwingine kuwapeleka waasipopajua, pikipiki juu ya barabara, abiria nyuma ya migongo yao ila Mungu yupo ndani yao, chochote katikati ya mapambano ya sarafu ni mipango ya Mungu.
Mwanaume ataaga nyumbani asubuhi, atamwacha Mke na Watoto wake! Maswali pekee kichwani mwake ni nitarudi na roho yangu? Ama nitarudi maiti? Nitarudi na afya yangu ama mahuti huti?
Katikati ya mvua za masika tunaishi na msemo wa popote kambi! Potelea pote Mwanangu akisema nani kama Mama, potelea pote Mama yake atapotuma ujumbe endelea na Malaya wako! Afahamu kuwa Malaya wetu ni mapambano, Lodge yetu ni rizki na kitanda chetu ni mafanikio.
Waache waendelee na mapambano ya Haki sawa lakini kwa ground hii ndio hali halisi, maisha magumu hatuna grisi! Tukiongea mbele yao wanatamani kusema tunafanana na Ngiri, wengine watasema ni Mbuzi kasoro bangiri.
Hii picha ni mapambano, hii picha ni msuguano wa kweli kuhusu rizki, simulizi ambazo haziandikiki na hazisemwi Bungeni, hazitajwi mtandaoni na hazisemeki mdomoni, simulizi za kutisha kuhusu Mwanaume.
Hakuna noma wewe tembea na Mkewe kwakuwa Mwanetu yupo busy mapambano ila hii picha ikukumbushe Ubinadamu, hakuna tabu wewe wafukuze watoto wake ada shule ila Baba yao hajakaa kizembe ameweka maisha mstarini ili atimize ndoto zao.
Mungu atubariki kwenye mapambano WANAUME, hatuna simulizi nzuri mbele yao, hatuna tuzo kwenye majukwaa yao lakini nyuma ya kila simulizi ngumu kuna Mwanaume alipasuka moyo, alivunja misuli na kukinga mishale ili familia iishi[emoji1317][emoji109]