Mungu haijui kesho yako

Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na mwisho tofauti na ule anaoujua Mungu kama akiamua kubadilika?
 
Lengo ni hitimisho la maisha yako ya umilele, Mungu hana hasara hata ukipotea,maana ana viumbe wengine mamilioni kwenye sayari zingine wasio na dhambi, anakupa muongozo kwa faida yako Ili uishi vyema hapa duniani na kesho ahera.
Hao viumbe wa Sayari nyingine ni kwanini hawana dhambi? Ila sisi tuwe na dhambi?
 
Kwa hiyo kama Mungu anapanga huo mwisho wako ila ibilisi anaingilia ina maana mungu atakuwa hajui huo mwisho wako utakuaje sababu ibilisi anaweza kuingilia muda wowote sio?
 
Na kama anajua tutafanya dhambi hana uwezo wa kutuzuia tusizifanye
 
Kwa hiyo maisha yangu baada ya kifo mimi ndio naamua yatakuaje na sio kuwa Mungu anayajua tayari?
 
1. Mungu anaijua kesho yetu sana ila achangamani na dhambi kabisa, unafikiri Mungu aliumba wanadamu aliwapangia haya yanayowapata? la hasha alikusudia mwanadamu aishi vyema akitenda yale aliyoyakusudia na kumwagiza rejea wakati adamu na eva waliwekwa kwny bustani ya eden destiny yao ilibadilika baada ya kutenda dhambi.

2. Anaijua kesho yetu kwa sababu kutenda dhambi it's your own choice na kinachokupata huko kwny dhambi yeye hausiki na uzur anakuelekeza ukifanya A utatokewa na matokeo haya na ww ukatenda hivyo so yeye anahusikaje hapo na ujinga wako mwnyw?
 
Hoja yangu ni kwamba kama mungu anajua ya kesho yako au maisha yako yatakavyokuwa hapa duniani basi hakuna haja ya kwepo kwa dhambi maana alishajua kwamba wewe utakuwa mizi

Na pia kama mungu anajua kesho yako basi
Bado hujanielewa vizuri ni hivi inamaana tunawaambia wattoto wetu wawe na bidii masomoni ili iweje, kama ni mungu alipanga mwanangu atakua mwalimu basi akae tu nyumbani
Pia tunawalea watoto wetu kwa maadili mazuri ili iweje maana mungu alishapanga kwamba atakuwa mwema, mtoto umleavyo ndio akuavyo mungu hapo anahusikaje
 
Kwa hiyo kesho yangu basi haijui maana uamuzi wa kutenda ama kutotenda dhambi ni mimi ndio naamua
 
mwenyezi mungu amemuumba binadamu akiwa na free will yani uwezo wa kufanya dhambi na kutofanya dhambi kila alichokupangia kiwe au kisiwe inategemea na matendo yako mwenyewe ..ni elimu pana sana hii yote kwa yote allah ndio mjuzi wa yote kwa akili yangu mimi ya kibinadamu naishia apa..allah atujaalie mwisho mwema amin inshallah[emoji2969]
 
Kwa hiyo kama Mungu anapanga huo mwisho wako ila ibilisi anaingilia ina maana mungu atakuwa hajui huo mwisho wako utakuaje sababu ibilisi anaweza kuingilia muda wowote sio?
hata hayo ambayo ibilisi anayaingilia usifikiri Mungu hayajui anaelewa mnoo yeye yuko so gentle hakuforce ila anakuelekeza tena kwa upendo so anataka ww ufanye on your own will ibilisi ndio anayetumia nguvu kuwaingiza watu kwny dhambi
 
kuna tofauti sana kwa anayeleta hoja flani kwa kutaka kuelewa na mwngine kwa kuleta ubishani hawa ni watu tofauti ukweli unauelewa ila unaamua kuleta kubisha

chief ukweli ww unaujua ila unaleta hoja ili kuleta ubishani. kuna tofauti kubwa ya mtu kuleta hoja kwa kutaka kuelewa na kutaka kuleta ubishani

mithali 26:4 " usimjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake usije ukafanana nae, umjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake asije akawa mwenye hekima machoni pake"

hapa inategemea mpumbavu unae deal nae kuna ya kujibu pale anapohitaji kuelewa mtu kuna wa kukaa kimya pale anapohitaji tufanane kwa upumbavu
 
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na mwisho tofauti na ule anaoujua Mungu kama akiamua kubadilika?
Hapana. Ishu ni kwamba anaziona njia zako, matendo yako, maamuzi yako, mfumo wa moyo wako na matamanio yake hivyo yeye kujua kuwa utabadilika au kuacha unachokifanya ni rahisi, huwezi kumfanyia suprice., mwisho wako anaujua.

Ni kama vile wewe unaangalia movie ambayo ulishaiona, unajua kabisa kitakachotokea sio kwa sababu umekifanya kitokee au umepanga ila ni kwa sababu unajua kitatokea sababu una uzoefu wa hiyo filamu.

Sasa MUNGU anaona matamanio ya moyo wako na anajua matokeo ya hayo matamanio siku zote ni nini kitafuata maana matendo ya binadamu ni yale yale tu hakuna jipya ambalo litakuwa suprice.
 
hata hayo ambayo ibilisi anayaingilia usifikiri Mungu hayajui anaelewa mnoo yeye yuko so gentle hakuforce ila anakuelekeza tena kwa upendo so anataka ww ufanye on your own will ibilisi ndio anayetumia nguvu kuwaingiza watu kwny dhambi
Kwa hiyo ibilisi hapo ndio mwamuzi wa mwisho sababu ndio anaamua akuingize kwenye dhambi ama akuache sio? Na anapoamua Mungu hawezi kumzuia
 
Haimake Sense hata kidogoo...!! Maisha ya mwanadamu kila kinachotokea kina sababu na Mungu anajua sio kesho yako tu hata maisha yako yote hapa duniani mwanzo mpaka mwisho...

Mungu anapenda tufe dhambini?? Kama hapendi kwanini anaruhusu wengine mwisho wao uwe hivyo?
 
Siku ukiwa Mtunzi hata wa simulizi utaelewa ni Kwa namna gani Mungu ndiye anayepanga maisha yako, na anajua mwisho wa kila kitu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…