Mungu anafaidika/anafurahia nini vitu hivi kutoka kwa binadam?

Ila Mungu ni zuzu jamani! eti wakati wa kusali, tumpe misifa ndio atajibu maombi yetu kwa wakati!
Hata kama humuamini ila si kwa hatua hii uliyofikia.....astaghfirullah!!!! Ndugu wewe nakuona kama uliyechanganywa na vile vitopic vya philosophy form 5&6 nothing else!!....usitutukanie Mungu wetu please...na umelaaniwa wewe pamoja na kizazi chako chote
 
Maswali ya msingi sana Mungu anawaumba watu kama maria na consolata halaf wanaishi kwa tabu tu jamani

Ndio utambue uwepo wake, anaumba anavopenda iwe rahisi sisi kuamini uwepo wake. Amewaumba waja wake apendavo iwe mfano kwetu, ikitujia imani tukumbuke uwepo wake.na ujue kwamba vyovyote tulivo anaweza akatunyima tukawa zaidi ya hao walioungana. Sisi alotujalia neema zake tumshukuru kama anavopenda. Mungu ametutaka tutoe sadaka ili iwe kinga na tiba kwenye maisha yetu. Anapenda tusali ili kuijaza imani nafsi zetu na kujitengenezea mazingira mazuri siku ya hukumu. Mwenyezi Mungu tumshukuru na kumsifu kila mara ni mwingi wa rehema na mwenye kurehemu. Tumsifu na kumshukuru kwa neema zake alizotupa haziwezi kuhesabika unazozijua, usizozijua.
 
kama hachoki mbona anawaumba mapacha walioungana. hiyo ni dalili ya kuwa alikosea kuumba na 98% inaonesha alikuwa mchovu
hahhaa....usikute alikuwa ana umba huku anasinzia..."" kwamujibu wa essay ya jamaa lakini "" maana haiwezekani " muweza wa yote ashindwe kuumba kitu ambacho ni timilifu
 
Miaka ile bado nasali/naamini uwepo wa personal God au Mungu anaehusika moja kwa moja na maisha ya binadam nilikua najiuliza baadhi ya maswali ila sikuwahi kupata majibu yake. Kwa kua imani inakufundisha kuamini kila kitu bila kuhoji ikanibidi niwe nakubali tu au naamini tu.

Baada ya kuachana na mambo ya kuamini uwepo wa mungu anaehusika na maisha ya binadam moja kwa moja, bado nimekua najiuliza, Mungu anafaidika nini na vitu vifuatavyo toka kwa binadam.

1. Kuomba. Mungu anafaidika nini na watu kumuomba wakati anajua maisha yao na anajua shida zao. Hii ni sawa na mzazi kujua kabisa mwanao hajala siku mbili na ana njaa na chakula unacho ila tu unangoja uombwe, je huu ni uwajibikaji au uzembe?

2. Kufunga. Mungu anafaidika nini na kuona watu wanashinda njaa au kushinda bila kula. Furaha yake ni nini watu wasipokula?

3. Sadaka/Zaka. Mungu ambae anadai yeye ni tajiri bado anataka pesa za watu eti wamtolee, mungu anafurahia nini kuomba watu hela zao tena watu choka mbaya lakini bado anakomaa umpelekee hela, ili iweje?

Mnaweza kunisaidia mungu anafurahia au anafaidika na nini na hivi vitu?
Naamini maswali yako naweza kuyajibu ila kwa imani yangu. Na ntakujibu kwa kutumia ushahidi Kitabu, hadithi na dalili japo najua hutataka masuala ya kitabu wala hadithi hivyo KUJIKITA ZAIDI KATIKA DALILI ambazo hata scientifically unaweza kuprove. Hakika MWENYEZI MUNGU ANAJUA ZAIDI
Naaahidi nitarudi Nikijaaliwa. Muda huu sio rafiki kwangu
 
hivi Mungu wetu kawa na tabia kama za jiwe hadi tuanze kutishana humu juu yakumjadili na kutaka kujua ukweli wake?
Nafuu ya jiwe "" maana hajawahi kusema kuwa ana uweza wa yote "" halafu akashindwa kuamua vita ya wamasai na wakulima "" wanaopigana kila siku kule KILOSA
 
Mkuu unapozungumzia Mungu nnadhani unajua kwenye ulimwengu huo wa Mungu(au ulimwengu wa roho) kuna pande mbili, peponi na jehanam.

Kila upande una taratibu zake na wakuu wa jehanam wanahangaika kuwavutia watu/roho za watu katika upande wao.

Maombi(pamoja na kufunga) na sadaka ni baadhi ya mambo yanayotuweka karibu zaidi na Mungu na kutukinga na mipango ovu ya ibilisi dhidi yetu.
Muweza ya yote anashindwaje kumuweka lockup ibilisi.., acheni hizo si amtie hata uchizi tu wanadamu tubaki salama..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom