Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,052
- 12,906
Miaka ile bado nasali/naamini uwepo wa personal God au Mungu anaehusika moja kwa moja na maisha ya binadam nilikua najiuliza baadhi ya maswali ila sikuwahi kupata majibu yake. Kwa kua imani inakufundisha kuamini kila kitu bila kuhoji ikanibidi niwe nakubali tu au naamini tu.
Baada ya kuachana na mambo ya kuamini uwepo wa mungu anaehusika na maisha ya binadam moja kwa moja, bado nimekua najiuliza, Mungu anafaidika nini na vitu vifuatavyo toka kwa binadam.
1. Kuomba. Mungu anafaidika nini na watu kumuomba wakati anajua maisha yao na anajua shida zao. Hii ni sawa na mzazi kujua kabisa mwanao hajala siku mbili na ana njaa na chakula unacho ila tu unangoja uombwe, je huu ni uwajibikaji au uzembe?
2. Kufunga. Mungu anafaidika nini na kuona watu wanashinda njaa au kushinda bila kula. Furaha yake ni nini watu wasipokula?
3. Sadaka/Zaka. Mungu ambae anadai yeye ni tajiri bado anataka pesa za watu eti wamtolee, mungu anafurahia nini kuomba watu hela zao tena watu choka mbaya lakini bado anakomaa umpelekee hela, ili iweje?
Mnaweza kunisaidia mungu anafurahia au anafaidika na nini na hivi vitu?