Mungu ameniponya ajali hii mbaya!!


Mkuu pole sana na shukrani nyingi zimwendee Mungu Mwenyezi.
Walimu wangu wa dini wamenifundisha kuwa Mungu anafanya mambo yasiyowezekana ili kupitia hayo tuweze kumpa yeye utukufu.Endelea kuwakumbusha watu wampende sana Mungu kwani ndiye muweza yote.
 
daa mkuu kweli Tumshukuru MUNGU! Pole sana!
 
Pole my dear teacher,nashukuru umepona,ningepata wapi mwalimu mwingine mie???
Mshukuru sana Mungu.......:clap2:
 
Pole sana mkuu. Tunamshukuru Mungu wetu Aliye Hai kwa kukutoa salama kwenye ajali hiyo. Ni Yeye pekee Anayestahili kupewa sifa na shukrani. Ubarikiwe!
 
Pole sana mkuu dah nimechelewa sana kuona hiii thread pole zangu zikufikie popote pale ulipo
 
Mshukuru Mungu ndg yangu tena katoe sadaka unaposali whether ni kanisani au msikitini, pole na hongera
 
Mungu anaweza, huwa anafanya mambo makuu ili wanadamu tuzidi kumwamini na kutambua ukuu wake, jina la bwana libarikiwe
 
Hakika nimefarijika sana na mioyo yenu ya huruma na maneno mema ya faraja,hakika waote mlionipa pole na kunitia moyo sina namna zaidi ya kuwashukuru nawashukuru pia waliorudisha ki-senksi maana kimenifanya nipate kazi rahisi ya ya kuwashukuruni nyote na kwa niaba ya ambao kwa sababu moja ama nyingine hawajapata nafasi kupitia thread hii
Namshukuru mola wangu kwa kunijaalia uzima na nawapenda nyote
God Bless u all!!
 
Nimechelewa kuona hii. Pokea pole yangu mkuu. Tunatakiwa kushukuru kwa kila jambo. Mshukuru mungu.
 
mkuu inkoskaz pole sana!!mungu akuzidishie maisha marefu na afya njema mkuu
 
Pole sana Inkoskazi, ni kawaida kwamba inapotokea ajali ya barabarani huwa inakuwa imesababishwa mara nyingi na makosa ya dereva mmoja, kwa hiyo humu barabarani huwa tunasalimika kwa uwezo wa Mungu, unaweza kuwa makini sana lakini akatokea mzushi akakuletea, kwa hiyo hili ni jambo la kushukuru sana,

'kesheni mkiomba maana hamjui siku wala saa'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…