Mungu aliyeumba Milkway(kilimia) galaxy na ulimwengu kwa ujumla ni mkuu sana

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Mfumo wetu wa jua na sayari zake vimo ndani ya galaxy inayoitwa milky way(kilimia). Galaxy ya kilimia ina umbo kama sahani iliyogawanyika kwenye mikia (arms)mbalimbali.

Milky-Way-annotated-SMALLMoreanno-948x1024.jpeg

Sahani hiyo ina upana wa 150,000 hadi 200,000 light years(miaka ya mwanga). Hapa maana yake kutoka mwisho mmoja wa sahani hadi ule mwingine mwanga utachukua miaka laki moja na nusu hadi laki mbili kusafiri na mwanga husafiri kilomita 300,000 kila sekunde! Huu ni upana usioelezeka.

Unene wa sahani hiyo ni 1,000 ly. Mwanga unachukua miaka 1000 kutoka juu ya sahani hadi chini.

Galaxy ya kilimia ina nyota billioni 100 hadi 400. Jua letu ni moja ya nyota hizo. Jua letu linapatikana katika mkia unaoitwa Orion. Huu ni mkia mdogo tu kati ya mikia mitano ya Kilimia.

800px-Milky_Way_Arms.svg.png
..
..
800px-Artist's_impression_of_the_Milky_Way_(updated_-_annotated).jpg
...
...
800px-Galactic_longitude.jpeg

Huo mkia wa Orion una urefu wa 20,000 ly na upana wa 3,500 ly. Mkia huu upo umbali wa 27,000 ly kutoka katikati ya galaxy.
Picha tunazoona usiku za milky way galaxy huwa ni picha za nyota zilizomo ndani ya mkia wa Orion. Tupo ndani ya Orion arm lakini tunaweza ipiga picha na kuonekana vizuri. Hii ni sababu ya ukubwa wake. Mtu aliye ndani ya nyumba hawezi kupiga picha nyumba hiyo na kupata picha inayoeleweka.

Picha ya miky way(Orion arm) usiku.

800px-Milky_Way_Night_Sky_Black_Rock_Desert_Nevada.jpg

......
Milky_Way_Arch.jpg

....
800px-ESO-VLT-Laser-phot-33a-07.jpg

Aliyeumba hivi vitu ni mkuu sana
 
Naenjoy sana nikiwa kijijini kwetu kuna msimu wa mwaka unaiona milkyway kuanzia saa 4 usiku mpka saa nane au tisa ila kuna kipindi haionekani.

Nasema kijijini kwakua hakuna taa nyingi zinazoathiri anga usiku hivyo anga linakua tulivu na nyota nyingi zinaonekana hivyo unapata wakati mzuri wa kuiona milkyway tena inapendeza zaidi umeme ukikatika.

Napenda kumuonyesha mwanangu vipindi vinavyozungumzia anga na nyota siku nilipomuonyesha milkyway alifurahi akikaa nje mpka saa tisa kila nikitoka ananionysha inapoelekea mpka akachoka ila ilikua experience nzuri sana kwake
 
Ukishamaliza kuimba pambio za sifa, Nenda kaulize tena kwa mungu wako

Kwanini kafanya tubanane kwenye kisayari hiki kidogo_Wakati kuna masayari ya kumwaga
Unauhakika tunabanana yapo maeneo kibao hayajapata wakazi ww unajibananisha hapo ulipo ila ukitaka nenda kwenye sayari yako si hela zako au kufa tukupeleke sayari ya ardhini kule hutabanana na mtu
 
Naenjoy sana nikiwa kijijini kwetu kuna msimu wa mwaka unaiona milkyway kuanzia saa 4 usiku mpka saa nane au tisa ila kuna kipindi haionekani.

Nasema kijijini kwakua hakuna taa nyingi zinazoathiri anga usiku hivyo anga linakua tulivu na nyota nyingi zinaonekana hivyo unapata wakati mzuri wa kuiona milkyway tena inapendeza zaidi umeme ukikatika.

Napenda kumuonyesha mwanangu vipindi vinavyozungumzia anga na nyota siku nilipomuonyesha milkyway alifurahi akikaa nje mpka saa tisa kila nikitoka ananionysha inapoelekea mpka akachoka ila ilikua experience nzuri sana kwake
Mkuu, uumbaji wake ni wa kiwango kisichoweza kupimwa na akili zetu.
 
Ni kweli kabisa ndugu. Mm nakaaga na dogo nje toka nimemuonyesha hii kitu ananiuliza maswali hadi nabaki nastaajabu uumbaji wa mungu yaani nafurahi sana dogo anapozingatia hasa akiwa mwenyewe nimemnunulia darubini ya 1000× military anajitahidi sana kuangalia anga usiku kila akienda kwa bibi yake hawez acha kifaa chake
 
Naenjoy sana nikiwa kijijini kwetu kuna msimu wa mwaka unaiona milkyway kuanzia saa 4 usiku mpka saa nane au tisa ila kuna kipindi haionekani.

Nasema kijijini kwakua hakuna taa nyingi zinazoathiri anga usiku hivyo anga linakua tulivu na nyota nyingi zinaonekana hivyo unapata wakati mzuri wa kuiona milkyway tena inapendeza zaidi umeme ukikatika.

Napenda kumuonyesha mwanangu vipindi vinavyozungumzia anga na nyota siku nilipomuonyesha milkyway alifurahi akikaa nje mpka saa tisa kila nikitoka ananionysha inapoelekea mpka akachoka ila ilikua experience nzuri sana kwake
Kwa hiyo kumbe macho yanaona hayo makilometa yote hayo ya mwanga?
 
Ni kweli kabisa ndugu. Mm nakaaga na dogo nje toka nimemuonyesha hii kitu ananiuliza maswali hadi nabaki nastaajabu uumbaji wa mungu yaani nafurahi sana dogo anapozingatia hasa akiwa mwenyewe nimemnunulia darubini ya 1000× military anajitahidi sana kuangalia anga usiku kila akienda kwa bibi yake hawez acha kifaa chake
Hicho kifaa kinauzwa wapi?
 
Kuna watakaodai kwamba eti hayo yote ni kwa sababu ya Bing bang theory,,,ambayo Bado haijawa Bing bang law... Nadhani wanaendelea kujiridhisha na Bing bang kama inaweza kuwa law au ipigwe chini kama Darwin theory of evolution
 
Mfumo wetu wa jua na sayari zake vimo ndani ya galaxy inayoitwa milky way(kilimia). Galaxy ya kilimia ina umbo kama sahani iliyogawanyika kwenye mikia (arms)mbalimbali.

View attachment 1742950

Sahani hiyo ina upana wa 150,000 hadi 200,000 light years(miaka ya mwanga). Hapa maana yake kutoka mwisho mmoja wa sahani hadi ule mwingine mwanga utachukua miaka laki moja na nusu hadi laki mbili kusafiri na mwanga husafiri kilomita 300 kila sekunde! Huu ni upana usioelezeka.

Unene wa sahani hiyo ni 1,000 ly. Mwanga unachukua miaka 1000 kutoka juu ya sahani hadi chini.

Galaxy ya kilimia ina nyota billioni 100 hadi 400. Jua letu ni moja ya nyota hizo. Jua letu linapatikana katika mkia unaoitwa Orion. Huu ni mkia mdogo tu kati ya mikia mitano ya Kilimia.

View attachment 1742953..
..
View attachment 1742954...
...
View attachment 1742955

Huo mkia wa Orion una urefu wa 20,000 ly na upana wa 3,500 ly. Mkia huu upo umbali wa 27,000 ly kutoka katikati ya galaxy.
Picha tunazoona usiku za milky way galaxy huwa ni picha za nyota zilizomo ndani ya mkia wa Orion. Tupo ndani ya Orion arm lakini tunaweza ipiga picha na kuonekana vizuri. Hii ni sababu ya ukubwa wake. Mtu aliye ndani ya nyumba hawezi kupiga picha nyumba hiyo na kupata picha inayoeleweka.

Picha ya miky way(Orion arm) usiku.

View attachment 1742962
......
View attachment 1742963
....
View attachment 1742964

Aliyeumba hivi vitu ni mkuu sana
Nadhani nami pia nahitaji elimu zaidi juu ya malimwengu (galaxies)
1. Tofauti ya universe, galaxy, constellation, star, some sort of those nebula and star dusts ni kipi na kipi siyo kipi.
2. Ni kweli Milky way Galaxy (njia ya maziwa ndiyo seven sisters constellation (kilimia)?
3. Our universe ( Milky way Galaxy) with 9 planet (entirely solar system) including our home Earth is the same to kilimia (seven sisters constellation)
4. Je hiyo Orion/Lion (Simba mwindaji) constellation iko hapa kwenye solar system au iko kwenye galaxy nyingine km vile spiral galaxy, au Andromeda ( our neighboring galaxy?
5. Je kuna ulimwengu/malimwengu/ universe ngapi? Na kila universe is it equal or same as galaxy or equal to constellation or star?
6. Vipi kuhusu makundi nyota hizi (constellation) dubu, nge, vigor, msalaba wa kusini, Orion vs Betelgeuse (the giant star in constellation) , kilimia nk?
7. Je Orion vs Betelgeuse deep hole concerp of heaven place ikoje boss?

Mi sijakupata Mzee baba naomba ongeza nyama kwenye huu Uzi km bado upo kwenye hili jukwaa.

Ahsante sana
 
Back
Top Bottom