Mungu akimpenda mja wake humpa mitihani

Mungu Ni Mwema Wakati Wote

Atapata Kujifungua Salama, Kubwa Sana Tunazidi Kumweka Kwenye Maombi Kila Wakati.

Amen Man Of God!!!!
 
Salam Alkam. Mimi Pia nilikuwa na ujauzito nikapitia situation kama anayopitia mke wako sasa hivi. Ikapita siku tatu madaktari wakasema hamna njia nyingine zaidi yakufanyiwa upasuaji. Mimi sio daktari wa nesi ila njia yakuokoa maisha ya mtoto na mama sasa hivi kama njia haifunguki ni operesheni tu.

Si mama na Mungu muombe awape kibali safari hii ongea na manesi wamfanyie mkeo operesheni la sivyo unaweza Poteza mtoto mwingine tena ukijua ni mitihani ya Mungu kumbe ni uzembe wa wanadamu wenyewe.

Maana manesi wa hospital zetu huwa ni washenzi sana watu wengi wanapoteza watoto na wamama kwaajili ya uzembe. Mkono wa Mungu uwe nawe.
 
Mwenyezi Mungu akuvushe salama. Hili litapita na mwanao atakuwa salama Mungu akupe nguvu. Mtegemee yeye siku zote atakupa nguvu na amani
 
Kwahiyo matatizo yote tunayopitia ni Mungu anasababisha kwasababu anatupenda? What a joke!
Ila pole sana mkuu, I can feel your pain.
 
Sasa unayemsifu hapa kwa kukutendea hayo ni Mungu au adui yako namba moja?

Uchawi wa Mwarabu na Mzungu haukutuacha salama kabisa! Zamani mababu zetu walikemea matatizo ya asili kwa vitendo, sisi leo tumeyaona kama ni zawadi nzuri kutoka kwa Mungu mwenye upendo 🤔

Kiranga akiiona hii ataishia kutikisa kichwa
Staha na falsafa za kuchukulia watu wote kwa upendo zinanifanya nitoe pole kwa misiba iliyotangulia na kutaka afya njema kwa mama na mtoto.

Kisha, ningependa watu wafanye chunguzi za matatizo na kuyatafutia ufumbuzi kisayansi zaidi, kuliko kumtegemea Mungu tu.

Nitasikitika sana ikiwa hatari ya kifo itajirudia kwa sababu wazazi wameamua kupata mtoto bila kutatua matatizo yaliyopita awali.

Kufanya hivyo ni kuhatarisha uhai wa mtoto na wa mama mzazi pia.
 
Kisha, ningependa watu wafanye chunguzi za matatizo na kuyatafutia ufumbuzi kisayansi zaidi, kuliko kumtegemea Mungu tu.

Leo nimefurahi sana kumuona yule king pin wa wapinga Mungu kukubali kuwa Mungu yupo isipokuwa tusimtegemee huyo Mungu pekeyake katika shida zetu bali pia tuitegemee sayansi.

Hapo upo sahihi kabisa na ninakuunga mkono juu ya suala hilo, na ndiyo maana huyo ndugu (mleta post) kwanza kampeleka mgonjwa hospitali (kategemea sayansi) na halafu kaomba tumuombe Mungu ili atie nguvu nk, katika juhudi za madaktari ili mgonjwa wake apone, hapo utaona sayansi na Mungu vipo sambamba.

I salute and commend you in this respect, big up Kiranga .
 
Unacholazimisha kwamba nimeandika ni tofauti na nilichoandika.

Jifunze kusoma kwa ufahamu kwanza, labda tutaweza kujadiliana kwa tija.

Kabla ya hapo, hapa kutakuwa na kelele tu.
 
Unacholazimisha kwamba nimeandika ni tofauti na nilichoandika.

Jifunze kusoma kwa ufahamu kwanza, labda tutaweza kujadiliana kwa tija.

Kabla ya hapo, hapa kutakuwa na kelele tu.

Sehemu ya maneno yako ni haya; "Kisha ningependa watu wafanye chunguzi za matatizo na kuyatafutia ufumbuzi wa kisayansi zaidi kuliko kumtegemea Mungu tu".

Hayo ni maneno yako yanayoonyesha kwamba kuna njia mbili ambazo zinazotakiwa kufuatwa na watu ili kukabiliana na matatizo yao, 1- ni njia ya kisayansi (uchunguzi wa kisayansi) na 2- ni njia ya kumtegemea Mungu, na katika njia hizo 2 wewe umetuasa kuyatafutia ufumbuzi matatizo yetu kupitia njia ya Kisayansi ZAIDI kuliko kumtegemea Mungu, na umeweka neno la msisitizo; Mungu TU,

Hivyo ndivyo nilivyokuelewa, kama bado huamini kuwa Mungu yupo basi hakuna haja ya discussion.
 
Pole Sana.
Kupoteza watoto kunauma Sana.
Mungu akafanye wepesi mkeo ajifungue na atoke salama.
 
Back
Top Bottom