Mungu akimpenda mja wake humpa mitihani

Alkam Alkam

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
602
509
Nimejaaliwa uzima namshukuru Mungu kwa hili, pia nataka kushea na viumbe wenzangu jambo kidogo Mungu humpa mtihani mja kulingana na imani yake kwa imani yangu.

Mwaka 2017 mwezi wa 11 nilibaatika kupata mtoto wa kike ambaye muda mchache baadae alifariki.

Mwaka 2018 mwezi wa 4 pia nilibahatika kupata mtoto wa kike ambae aliishi kwa miezi 8 akafariki.

Leo siku ya tatu mke wangu yupo hospitali kwa ajili ya kujifungua anapata uchungu lakini njia bado ndogo inasentimeta 2 wanasema mpaka zifike 10 na sasa ni masaa 72 bado iko vile vile.

Anatoka tu na maji leo tumeambiwa twende kwenye utralsound aangalie kwenye mfuko wa mtoto maji kama bado yapo au Lah.

Maombi yenu Kila mtu kwa imani yake Mungu afanye wepesi.

Update:

Mgonjwa yupo hospitali ya wilaya ya kateshi,12:25 nimepigiwa simu wametoa go ahead ya kufanyiwa operation
 
Sasa unayemsifu hapa kwa kukutendea hayo ni Mungu au adui yako namba moja?

Uchawi wa Mwarabu na Mzungu haukutuacha salama kabisa! Zamani mababu zetu walikemea matatizo ya asili kwa vitendo, sisi leo tumeyaona kama ni zawadi nzuri kutoka kwa Mungu mwenye upendo 🤔

Kiranga akiiona hii ataishia kutikisa kichwa
 
Nilikuwa na uhakika

Watu dizaini yako lazima mgetokea katika huu uzi! We mtu ameshajielezea kutokana na imani yake, pia bado tu unataka kuleta ubishi na akasisitiza wadau tumuombee kila mmoja kwa imani yake so we kama unaona hicho unachoamini ndo sahihi muombee.
 
Sasa unayemsifu hapa kwa kukutendea hayo ni Mungu au adui yako namba moja?

Uchawi wa Mwarabu na Mzungu haukutuacha salama kabisa! Zamani mababu zetu walikemea matatizo ya asili kwa vitendo, sisi leo tumeyaona kama ni zawadi nzuri kutoka kwa Mungu mwenye upendo 🤔

Kiranga akiiona hii ataishia kutikisa kichwa
Enthusiasts mna matatizo sana yeye anaamini katika MUNGU MMOJA ni kama wewe unavoamini kua una maarifa mapana katika kufikiri japo ukiambiwa yalete hayo maarifa tuyaone kamwe hutofanya hivo

Kingine ni kwamba the way unavofikiria wewe walishafikiria sana kabla yako/yenu kwahiyo wewe endelea kuamini tu kua unayo akili isiyoonekana/kushikika na yeye aendelee kumuamini MUNGU wake wa kweli asieonekana na asieshikika
 
Back
Top Bottom