Mungiki ndani ya Tanzania!

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
Hii operation inayoendeshwa na jeshi la polisi juu ya uvamizi wa viwanja huko maeneo ya madale limezua jipya baada ya kuonekana kuwa kuna raia wa kutoka kenya wakijihusisha na uvamizi wa viwanja.

Wakati mwingine najiuliza hili jeshi letu la polisi huwa linafanya uchunguzi wa kina kabla ya kuwahusisha watu fulani na kundi fulani isije kuwa kama ya kamanda kova na yule aliyemteka ulimboka mpaka leo hakuna kinachoendelea!
 
Hapa hukuna cha Mungiki wala nini.

Serikali inatafuta sehemu ya kufichia uso wake baada ya kuvuruga sheria za ardhi na kuwafanya watanzania kuishi kama wanyama bila mipaka wala mipango mizuri ya ardhi.

Tunaishi kwenye nyumba zisizo na namba na kwenye makazi yasiyo rasmi. Kesho wakiende kubomoa kigogo watakwambia waliogoma ni raia wa nje.

Waliingiaje na kupata hiyo jeuri ya kuvamia viwanja vya watanzania? Hii ni kashfa kwa wakenya na kama kweli hao wahusika ni raia wa kigeni serikali inachelea nini kuwapumbuzisha Keko au Ukonga?
 
Hawa jamaa wanatafuta jinsi ya kuhalalisha uonezi hao ni raia na wazawa ardhi yote mafisadi wamemiliki tukakae kenya bora vita ije tuheshimiane
 
Hata huyo JWTZ waliyemkamata ambapo waliogopa kutaja jina lake ni raia wa Kenya?
Polisi wetu baada ya kugeuzwa wanasiasa wamekosa kabisa uwezo wa kutumia utashi wao kupambanua mambo.
.
 
Naona wa Kenya...wanatusumbua sana kiakili na intelijensia yetu inashindwa kabisa kwa penetration ya wakenya maana kila tukio wakishindwa ku justify wanakimbilia Kenya au Somalia!!
 
Jamani kwenye ukweli lazima tuseme nitajaribu ku summarize. Mimi nina eneo sehemu za mbopo zaidi ya miaka kumi sasa na huwa ninaenda huko si chini ya mara mbili kila mwezi kwa muda wote huo. Kilichotokea mbopo/madale/nyakasangwe na maeneo jirani ni kuwa kuanzia 2007 kulijitokeza kikundi kidogo cha watu wakazi wa maeneo hayo kuvamia mashamba yaliyokaa muda mrefu kisha wanajikatia vipande mita 20 x 20. Then wanatafutwa wateja wao (wavamiza) wanawauzia. Mwenye shamba akija anakutwa tayari watu wameshajenga wamehamia, wengine wanamalizia nyumba, wengine wamepanda miti. Mwenye shamba anakuwa na kesi na watu hata 40 amabao wameuziwa bila kujua kuwa waliowauzia sio wamiliki halali.

Mwaka 2008 kuna watu (ndio hawa wana hisiwa sio watanzania) wapo kama 200 hivi walikotokea hakujulikana wakaungana na wazawa wachache wa maeneo hayo kisha wakaanza uvamizi wa kutisha. Wanavamia hata shamba linalindwa. Ukija mwenye shamba wanakupiga mapanga na mishale na wanakuua hivi mchana kweupe. Ikija defender ya polisi wanaikimbilia sio kuikimbia. Hawa jamaa ni kwa vile tu nchi yetu haina waandishi wa habari makini lakini mambo waliyofanya ndani ya miaka minne yanatisha na walishaanzisha nchi na serikali yao ndani ya tanzania.

Ukweli ulio wazi polisi na serikali kwa ujumla walizembea (aidha kwa kutokujua au kupuuzia taarifa walizopokea) mpaka hawa jamaa wakajenga himaya yao sehemu inaitwa kaza roho. Hapo kaza roho ukiingia kama sio mwenyeji utarudi kilema kama sio maiti.


Katika suala hili nafikiri vyombo vya habari vinapaswa kwenda mbopo/madale/nyakasangwe kutafuta ukweli. Ni kweli wengi waliovunjiwa sio walivamia ila wameuziwa na wavamizi (mungiki) kwa kutokujua ila wengine walikuwa wanajua. Kwani hakuna kiwanja cha tshs. laki 200,000/300,000 hapo madale/mbopo. Ki msingi walikimbilia urahisi bila kutafuta ukweli halisi nani wamiliki wa maeneo hayo.

Kwa sasa hivi hao Mungiki zaidi ya 200 wapo wamejikusanya kwenye shule bondeni sehemu ya Nyakasangwe na wametishia kumuua mwenyekiti wa mbopo, kuchoma shule za msingi na sekondari mbopo na zahanati ya mbopo.
Kwa hili naipongeza serikali kwa kuchukua hatua japo kwa kuchelewa. Hao mungiki wan roho ngumu na ni makatili kishenzi hata hisia kuwa sio watanzania zinweza kuwa na chembe za ukweli.
 
Back
Top Bottom