Mume wangu hataki kunipa chakula cha ndoa

Mume wangu hataki kunipa chakula cha ndoa

Kaa nae chini hongea nae maana maisha ya sasa hatari, unaweza kukuta anadaiwa hajarejesha hata mikopo wewe kaa nae chini hongea nae, sio bure anamatatizo na wala usimfikirie vibaya.
 
Labda humpeti peti kama zamani, labda roho inamuuma kuona mapenzi yamehamia kwa mtoto. Mjali yeye, pendeza kwa ajili yake. jipambe, chumba kinukie, mpikie chakula kizuri, kula nae...punguza mahaba kwa mtoto, mpe muda mumeo. yeye alikuwepo kabla ya mtoto na atakuwepo siku zote hata pale mtoto atapokuwa hayupo...( kumbuka atakua. ataenda shule, ataanza kazi) ila hubby atakuwepo siku zote.....Pia usisahau Sala.
 
Habari zenu wapendwa,

Nimeolewa na nina mtoto mmoja na nampenda sana mume wangu.

Mimi na hubby wangu tumekaa ktk relationship for more than five years ndipo tukafunga ndoa.

We were so much into each other hadi nilipofanikiwa kupata mtoto last year mambo yakaanza kubadilika.

Ni mtu ambaye yuko bize sana na kazi.Since niwe na mtoto tumekuwa tunastruggle kwenye tendo la ndoa kwani mwenzangu huwa hajisikii au amechoka like all the time.

Sasa tuna miezi mitatu bila kugegedana na nimejaribu kuzungumza nae kama kuna tatizo anasema anachoka sana na kazi.

Plz nisaidieni kimawazo kama wanaume wakichoka sana hawawezi kuwa na huo uhitaji kwani ndiyo mwanaume pekee niliyewahi kuwa nae.

Asanteni

nenda naye taratibu, inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, usimbake. iko siku utajifunza kitu dhidi ya uchovu wake
 
Kama uko dar ni pm. Tusaidiane, si wajua msaada kwenye tuta
 
Bi mdogo;
Kuna mambo mawili matatu naweza kukusaidia kutokana na maelezo yako.
Moja;
Hivi, biashara yenu imechanua zaidi? Je, Hapo anapofanyia hiyo biashara kuna mazingira yanayo mfanya atumie akili na nguvu nyingi za mwili? Hayo humchosha mtu saana na anapokuja nyumbani anajikuta bado anawaza ya shughuli.
Pili;
Una mtoto mchanga, kumbuka ana hitaji saana usafi. Ni jambo ambalo ni jipya kwako. Una usafi? Mtoto awe msafi, weye uwe msafi, kitanda kiwe kisafi?? Utashangaa, chumba kinajaa nepi chafu au pampas zilizotumila au hata ambazo hazijatumika zinazagaa kila kona ya nyumba.
Mumeo, hili ni jipya kwake.
Tatu;
Sijui weye ni kabila gani, lakini kuna makabila wanapenda kuwatunza wake zao kwenye kipindi hiki cha uzazi. Unaweza ulibugia uji zaidi ukanenepeana, harufu ile ya maziwa yanayovuja etc. Je, upo sawa hapo? Chunga hayo na ujiweke fit. Usijiachie ukajikuta umechepuka
 
Back
Top Bottom