Mume wangu ananinyima unyumba

Mume wangu ananinyima unyumba

sijui kwa kweli , nyumbani anarejea kuanzia saa tano wala hanywi pombe, na huwa simuhoji kwa lolote.
Usijali endelea kua mvumilivu na kuchukua ushauri sahii ili usivunje ndoa yako kwa majaribu madogo,kipindi tunakua tuliona changamoto zote wanazopitia mama zetu juu ya baba zetu alkadharika baba zetu juu ya mama zetu,baba zetu wa mjini engine walipenda kushinda kwa warabu tu kula mirungi huku warabu wakiingiza pesa yeye anashinda tu bila faida,ile iliwapeleke kukosa hamu ya kula,kuwa karibu na famili hata kusuasua katika utaftaji,lakini mama zetu walikomaa na kipindi kile cha mpito kikapita na familia ikawa na furaha.YASHINDE MAJARIBU.
 
Kwanza hongera miaka nane ya ndoa umejitahidi wengine miezi4 tayari ndani hakukaliki Lea watoto mpotezee tu ana matatizo yake au amepata shida Fulani anaogopa kukumbia fanya uchunguzi utagundua
 
Monica;
Jilinde dada. Ni ndoa yako hiyo tu inatafutwa. Ulijisahau mda mrefu sasa, tangu alipoanza kukuachia matuizi ya nyumbani ujisakanyie alikuwa keshaanza kukudharau.
Suluhisho, anza kuzima matumizi. Mwambie kuwa hali ya maisha ni ngumu hivyo akusaidie angalao siku moja moja. Akitikisa kibiriti weye mchome kabisa. Yaani goma na weye kununua. Huenda amezidiwa na wivu kiasi kwamba anaona kuwa kuna dume jenza linamlisha.
Kipato chako chanzo chake ni nini au wapi? Lazima huyu kazidiwa wivu kiasi kwamba hawezi kujieleza. Anachelewa kurudi home si kwa sababu nyingine, amebana sehem kukuchungulia aone ukitoka au kidume kikiingia
 
pole hayo ni matatizo tu ya kisaikolojia tu,ila naamini mwanzo alikuwa vizuri tu japo hujasema hilo.
 
Habari zenu,

Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili na nipo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa.Tumekuwa tukiishi maisha ya ugomvi kwa muda na mume wangu, ila nikaona ni vyema nijishushe na nisihoji chochote.Mimi ndiye ninahangaika na familia na mambo yote hakai kujadili jambo lolote la maana na mimi.

Binafsi niliona nijishushe na nisihoji chochote ila tatizo limekua ni kwenye unyumba. Kwa kweli navumilia sana tunalala pamoja najitahidi kujiweka safi, kubadili mazingira ya chumba, manukato na hata mavazi lakini wapi!

Naweza nikamfanyia vikorombwezo vyote ila atageukia upande wa pili na kukoroma nimemsihi sana yeye anasema anawaza maisha hawezi kuendekeza ngono.Tunaweza kukaa mpaka miezi mitatu hatujakutana,hili swala linanikondesha jamani.

Naombeni njia ya kujinasua katika hili janga.
Inawezekana ana ugonjwa ambao hataki kukuambukiza. Hata hivyo pole. Kama mlifunga ndoa kanisani nenda kamweleze mchungaji wako.
 
Habari zenu,

Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili na nipo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa.Tumekuwa tukiishi maisha ya ugomvi kwa muda na mume wangu, ila nikaona ni vyema nijishushe na nisihoji chochote.Mimi ndiye ninahangaika na familia na mambo yote hakai kujadili jambo lolote la maana na mimi.

Binafsi niliona nijishushe na nisihoji chochote ila tatizo limekua ni kwenye unyumba. Kwa kweli navumilia sana tunalala pamoja najitahidi kujiweka safi, kubadili mazingira ya chumba, manukato na hata mavazi lakini wapi!

Naweza nikamfanyia vikorombwezo vyote ila atageukia upande wa pili na kukoroma nimemsihi sana yeye anasema anawaza maisha hawezi kuendekeza ngono.Tunaweza kukaa mpaka miezi mitatu hatujakutana,hili swala linanikondesha jamani.

Naombeni njia ya kujinasua katika hili janga.
Jihadhari asijekuwa anakuepusha na jambo baya alilonalo na anaogopa kukueleza. Najua ni mateso kwako lakini.. take care!
 
92340eed16e04e5320c50079125669fc.jpg
 
usiendelee kuteseka kwa hofu ya ndoa,waoneni walezi wenu wa kiroho ie mchungaji/padre/sheikh,.ikishindikana kama ni wakatoliki pelekeni ombi la talaka kwa askofu,hiyo ni sababu ya msingi ya kuvunja mahusiano,unyumba muhimu .

nb:ushahuri huu uchukue kama wa mwisho,maana kuwa single mama ni shughuri,unaelewa wanavyo taabika na jamii inavyowachukulia
 
tatizo ni we kuwaza ngono, mpe muda mwenzio apumuwe.
he is a human being and not a sex machine, and the first sexual organ is the mind - mwenye masikio na asikie kile Roho ayaambia makanisa
Unampotosha mwenzio
 
"Mume na ampe mkewe haki yake,na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe,vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe(2 korintho 7:3-4)

Mwambie mumeo tumeagizwa tusinyimane
ww
 
Back
Top Bottom