Mume wangu ananinyima unyumba

Monika2

Member
Jan 13, 2016
81
89
Habari zenu,

Mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili na nipo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa.Tumekuwa tukiishi maisha ya ugomvi kwa muda na mume wangu, ila nikaona ni vyema nijishushe na nisihoji chochote.Mimi ndiye ninahangaika na familia na mambo yote hakai kujadili jambo lolote la maana na mimi.

Binafsi niliona nijishushe na nisihoji chochote ila tatizo limekua ni kwenye unyumba. Kwa kweli navumilia sana tunalala pamoja najitahidi kujiweka safi, kubadili mazingira ya chumba, manukato na hata mavazi lakini wapi!

Naweza nikamfanyia vikorombwezo vyote ila atageukia upande wa pili na kukoroma nimemsihi sana yeye anasema anawaza maisha hawezi kuendekeza ngono.Tunaweza kukaa mpaka miezi mitatu hatujakutana,hili swala linanikondesha jamani.

Naombeni njia ya kujinasua katika hili janga.
 
Pole sana Mony..huyo atakuwa haja zake anatimiziwa na nyumba ndogo,ndio maana anakuwa hivyo.
 
ni wakati tu mnapitia hizi ni hali ambazo zipo, mvumilie tu ata Mimi hua napatwa hali kama hiyo
 
Monica kuna vitu kadhaa.

1. Inawezekana anaumwa magonjwa ya huko chini. Kwa sababu hamna utaratibu wa kutumia condom na anakupenda anapotezea. Lini mlienda kupima wote?

2. Inawezekana ana UTI sugu ambayo Mara nyingi ili mwanaume afahamu anaumwa pumbu moja huvimba na kuuma. Mara nyingi hii hukata kabisa steam ya kusex.

3. Inawezekana anawazia maisha. Lakini hii kama ni kweli na mna good communication inatakiwa akuambie.

4. Muulize tatizo ni nini? Muulize kwa sababu wewe una hamu anataka uende wapi kama sio yeye. Kwa hili atajiongeza.
 
Akifuata huo ushauri namba 4, nakuhakikishia atachezea kichapo.
 
habari zenu,
mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili na nipo kwenye ndoa kwa miaka nane sasa,
tumekua tukiishi maisha ya ugomvi kwa muda na mume wangu, ila nikaona ni vyema nijishushe na nisihoji chochote,
mimi ndiye ninahangaika na familia na mambo yote
hakai kujadili jambo lolote la maana na mimi.
binafsi niliona nijishushe na nisihoji chochote ila tatizo limekua ni kwenye unyumba,
kwa kweli navumilia sana tunalala pamoja najitahidi kujiweka safi, kubadili mazingira ya chumba, manukato na hata mavazi lakini wapi!
naweza nikamfanyia vikorombwezo vyote ila atageukia upande wa pili na kukoroma,
nimemsihi sana yeye anasema anawaza maisha hawezi kuendekeza ngono,
tunaweza kukaa mpaka miezi mitatu hatujakutana,
hili swala linanikondesha jamani naombeni njia ya kujinasua katika hili janga.

Fanya jambo 1 kama wewe ni muislamu, nenda Mahakmani kutana na mtu anaitwa kadhi/mufti mueleze hilo tatizo bila shaka atawaita nyote lakini kwa sababu mumeo ataendelea kukutesa hataki mdai talaka yako kama hatakupa talaka kadhi anaweza kufanya hivyo.

mwambie aliyekuwa mumeo kwamba unatafuta mtu akuoe kwa ajili ya #Hapa Kazi tu', na huyo atakae kuoa mueleze hali halisi basi tena hapo utaenda kwa huyu jamaa akikufanyia hiyo shida yako baadae utarudi kulea watoto wako na familia yako nyumbani kwa yule aliyekuwa mumeo. maisha muendeshe kwa utaratibu huo.
 
Pole sana Mony..huyo atakuwa haja zake anatimiziwa na nyumba ndogo,ndio maana anakuwa hivyo.
sijui kwa kweli , nyumbani anarejea kuanzia saa tano wala hanywi pombe, na huwa simuhoji kwa lolote.
 
Monica kuna vitu kadhaa.

1. Inawezekana anaumwa magonjwa ya huko chini. Kwa sababu hamna utaratibu wa kutumia condom na anakupenda anapotezea. Lini mlienda kupima wote?

2. Inawezekana ana UTI sugu ambayo Mara nyingi ili mwanaume afahamu anaumwa pumbu moja huvimba na kuuma. Mara nyingi hii hukata kabisa steam ya kusex.

3. Inawezekana anawazia maisha. Lakini hii kama ni kweli na mna good communication inatakiwa akuambie.

4. Muulize tatizo ni nini? Muulize kwa sababu wewe una hamu anataka uende wapi kama sio yeye. Kwa hili atajiongeza.

kuhusu kupima kwa kweli alikataa na huwa simlazimishi kitu, hata kipindi cha ujauzito aligoma kwenda kupima kabisa hivyo siwezi kufahamu.
kuwazia maisha sifahamu kwa kuwa mambo mengi ya familia nayakamilisha mimi.

nimemuuliza mara nyingi anasema hakuna tatizo, na atabadilika.
 
Fanya jambo 1 kama wewe ni muislamu, nenda Mahakmani kutana na mtu anaitwa kadhi/mufti mueleze hilo tatizo bila shaka atawaita nyote lakini kwa sababu mumeo ataendelea kukutesa hataki mdai talaka yako kama hatakupa talaka kadhi anaweza kufanya hivyo.

mwambie aliyekuwa mumeo kwamba unatafuta mtu akuoe kwa ajili ya #Hapa Kazi tu', na huyo atakae kuoa mueleze hali halisi basi tena hapo utaenda kwa huyu jamaa akikufanyia hiyo shida yako baadae utarudi kulea watoto wako na familia yako nyumbani kwa yule aliyekuwa mumeo. maisha muendeshe kwa utaratibu huo.
nimejitahidi sana nisiweke hili jambo wazi ili kuistiri ndoa yetu,
mpaka nimeandika hapa naona uvumilivu unanishinda,
ahsante sana kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom