Mume wangu ana gubu jamani naombeni msaada wenu

Mume wangu ana gubu jamani naombeni msaada wenu

mollyo

Member
Joined
Apr 26, 2015
Posts
39
Reaction score
6
Kwanza poleni kea majukumu ya Jumatatu,

Jamani ndugu zangu nisaidieni mimi, nina mume ambae mwanzoni mwa ndoa yetu alionyesha kunipenda sana. Lakini kadiri maisha yanavosonga mume wangu amebadilika amekuwa ni mtu wa ugomvi.

Kila kukicha na mkigombana jambo dogo tuu atalikuza na kuwa kubwa, atasusa chakula hata kitandani halali analala chumba kingine au kwenye sofa, nimekata tamaa maana kila ninapojaribu kumsihi na kujishusha haelewi.

Nisaidieni ndugu zangu
 
Anakolala na ww mfuate huko huko mpaka kieleweke
 
wewe ulitaka kuolewa
hizo ndio changamoto za ndoa uvumile ukishindwa rudi kwenu
 
1. Tatizo kubwa la binadamu ni kutoona makosa yake.... a.k.a nyanyi haonagi nduku lake maana lipo mbali na upeo wa macho yake.
2. Siku zote kwenye ugomvi hakunaga mwenye 100% ya makosa yanayopelekea ugomvi.. Ushajiamgalia wewe una asilimia ngapi..??
3. Umeshawahi kukaa na kujiuliza yepi uyatendayo yanayopelekea ugomvi..???
4. Raha ya ugomvi ni kutjibishana.. Hakuna mtu anayeweza kugombana na mtu asiyejibu vibaya... Umeshacheki majibu yako kwa mumeo yapoje..??
 
Pole sana kwa yanayokusibu ulishawagi kukaa nae ili ku solve hizo mis-understandings.! Jee huwa unatafutaga watu i mean ndugu ama rafiki wa kaibu jwa ushauri..! Me nliambiwaga sometimes huwa ni demons wabaya wanasababsha ugomvi kwa wapenzi soo you too need prayers alot.
 
Pole mwaya , uliwahi kukaa Nae mkaliongelea tatizo hili? Unahisi ana mpenzi nje? Mna Watoto wangapi ?
 
Pole mwaya , uliwahi kukaa Nae mkaliongelea tatizo hili? Unahisi ana mpenzi nje? Mna Watoto wangapi ?

mtoto1, yani hata nikijaribu kumuuliza kwa upole kuhusiana na hayo mambo huwa hataki kabisa kuzungumzia tena anaeza akapanga safar ya ghafla ili tuu msiyaongelee
 
Pole bidada mwanaume mwenye gubu analeta kizunguzungu si kidogo
 
Huyo anamtu anayempa jeuri pole sana usichoke kuelewa ujumbe wa pm uzingatie
 
Kakujua una mahaba niue

Akileta ugomvi dawa yake piga kimyaa aongeeee ahame chumbaaaaa anuneeeeeeee wala usimpe sababu
 
njoo shoga mollyo nikupe dawa yake huyo
 
Last edited by a moderator:
Pole mwaya, hilo gubu hadi la kulala kwenye kochi......ni nouma, nahisi atakuwa kapata mchepuko huyo
 
Pole mwaya, hilo gubu hadi la kulala kwenye kochi......ni nouma, nahisi atakuwa kapata mchepuko huyo

Miw navyopenda kubanjuliwa kwenye coach,ningekuwa namkasirisha kila siku aende kochini nimfate nipe haki yangu.
Maisha yenyeww mafupi
 
Miw navyopenda kubanjuliwa kwenye coach,ningekuwa namkasirisha kila siku aende kochini nimfate nipe haki yangu.
Maisha yenyeww mafupi

Ahahahaha, nimechekaje kwa sauti..... Sasa mtu mwenyewe kanuna atakubanjuaje hapo kwenye kochi? Huyo anatafuta sababu za kutokugundulika kama ana mchepuko, anamepata mchepuko hlf analeta gubu home, asubiri na mke aje amuonyeahe side B yake atajuta.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom