"Mume wa mtu mtamu bana" ...


Una mchepuko?
 
ama kweli Dunia imevaa bukta!,naona mambo haramu yanahalalishwa mchana kweupeee...!tusubiri matokeo!
 

Mkuu ninachoongea ninakijua kabisa tena nina mifano ya kutosha,kuna dada alikuwa jirani yangu sehem nilipokuwa naishi alikuwa amepangishiwa chumba kabisa na mume wa mtu,alikuwa anajiheshimu yule mwanamke na sikuwah sikia au kuona akiwa na mwanaume mwingine na huyo mwanaume wake akija alikuwa hataki aondoke,mambo yako tofauti ndugu yangu wewe unapoona maisha magumu kwako na hauwezi kuhudumia familia mbili wenzako wanaweza,kuna wanawake wamejihalalishia kuwa nyumba ndogo
 
ni kweli, lakini kiasilimia wachuna mabuzi ni wengi kuliko wa aina hiyo unayosema
 
Na wakitaka kuolewa wanataka ambaye hajaoa! Wanawake huwa hawajielewi nini wanataka.!
 
Wasiojua thamani ya mili yao ndiyo huigeuza kama kitega uchumi

Mabinti wanashindwa kujishughulisha wajipatie kipato kazi yao imekuwa kuvizia waume za watu.

Hiki ndicho chanzo kikubwa cha migogoro katika familia.

Wakati anamchukua mume wa mtu leo na kusema ni mtamu anajisahau na yeye ipo siku ataingia katika ndoa, atafanyiwa hayo hayo.
 
Cha mtu huliwa na mtu cha chuma huliwa na kutu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…